Wedding Anniversary

Hongera sana FP kwa kutimiza miaka 13 ya ndoa. Kwa kweli unastahili sifa na pongezi maana si wote ambao wamebahatika kupata wenzi bora wa maisha na wakadumu nao kwa mda mrefu huku wakiishi kwa amani, afya na furaha...Lakini pamoja na hayo yote, sifa na shukrani ziende kwa Mungu muweza wa yote aliyekujalia hekima na akili ya kuweza kuchagua mwenzi bora wa maisha.

Sina mengi ya kusema zaidi ya kukutakia mema na baraka tele katika safari yako ya maisha ya ndoa...Mungu awaongoze katika safari hii ya maisha yenu, kila mfanyalo mlifanye pamoja naye...awajalie muweze kujenga familia bora na yenye kumpendeza Mungu...Hongereni sana katika kusherehekea siku hii ya leo...na ninawatakia kila heri na baraka tele katika safari hii ya maisha yenu ya duniani...Mungu awabariki sana.
Nashukuru sana rafiki yangu kwa haya maombi yako, naamini Mungu atatujalia yote uliyotuombea.... Asante sana
 
Nashukuru sana rafiki yangu kwa haya maombi yako, naamini Mungu atatujalia yote uliyotuombea.... Asante sana
Pamoja sana dada angu...Cheeeerss!!!!
champagne.jpg
 
FP your name tells where you are.

nakutakia kila heri mamii. Mungu awe ndio msaada wenu kila uchwao. awakuzie wanenu nanyi muwalee vyema waje wawafae baadae
 
Last edited by a moderator:
waaaaoh hongera sana FP am so proud of you! Ni wachache sana wanaoweza kukaa miaka hiyo bila kutetereka . Jambo la Kumshukuru Mungu na sababu ya kuparty leo kwa saaana tu!

Hawa wa siku hizi wakikaa mwaka mmoja miwili tayari mambo yameanza....bora 'siye wa zamani' lol
The Boss upo arifu?
 
Last edited by a moderator:
hakika mwastahili pongezi,miaka 13 ktk ndoa si mchezo,lakini kwenu imewezekana,mmebaki kuwa mwili mmoja na mmesimamia lengo lenu.upendo umekuwa chachu ya umri huu wa ndoa na kuvumiliana kumewajengea heshima katika jamii,hongereni sana!hakika ndoa iheshimiwe na watu wote nanyi mmekuwa dira ya kweli ktk kujenga heshima nasi twaiheshimu ndoa hii na kumwomba MWENYEZI MUNGU azidi kuwabariki,kuwapeni umri mrefu zaidi wa ndoa,afya njema ktk roho,miili yenu na afya njema ya ndoa,upendo uzidi kukua na katu msimuache anaewafanya kuwa ninyi ktk dunia hii.mbarikiwe sana na kila jema ktk safari yenu ya kupigiwa mfano.be blessed!
 
Hongera sana rafiki hiyo ni hatua kubwa hivyo mna kila sababu ya kumshukuru Mungu. Mwenyezi Mungu na aendelee kuwabariki mzidi kudumu katika agano lenu, awajalie amani, upendo na afya njema siku zote za maisha yenu.
 
Ndugu zangu wapendwa, leo tarehe 9/10 ni kumbukumbu ya agano langu la ndoa kati yangu na mpenzi wangu miaka 13 iliyopita.

Namshukuru sana Mungu wangu kwa kunipa huyu rafiki yangu kuwa mwenzangu. Ni jambo ambalo sijawahi kulijutia katika miaka yote 13 niliyoishi naye. Nazidi kumwomba Mungu tuzidishe upendo katika haya maisha tuliyoyachagua.

Nawaomba pia rafiki zangu wenye mapenzi mema mzidi kutuombea maisha yenye Upendo, Baraka na Neema.

Hongeraaa Bibie!!!! Mi ushauri wangu ni NGANGANIA ZAIDI NA ZAIDI HAPO HAPO ZAIDI YA LUBA!!! Kitaa hali si shwariii! UKISHIKWA SHIKAMANA BIBI!!! Naomba wimbo wa Naomba kibao NO. 1 cha ENRIQUE IGLESIAS, END OF THE ROAD cha BOYS II MEN, Na MY HEART WILL GO ON cha CELINE DION VIWABURUDISHE SIKU YA LEO!!!!!

NANI KANUNAAAAAA!!!!!!!!! (NYUMBA NDOGO, VIMADA, SECRETARY, NA VIZABIZABINA WOTE MNAONGEJEA KITU KISAMBARATIKE!!!! HAKIVUNJIKIIII KITU!!! MPO HAPO! MTANGOJA MIAKA 1000000000000000000000000000000)

Chonde chonde shosti unganganie, sio hapa najitia SHABIKI MAANDAZI KUWEKWA AMIRA KIJIKO KIMOJA NA KUUMUKA BESENI ZIMA! Usije kusema humu Kitu Chaliiiii! LITANISHUKAJE!!!!!
 
nakumbuka clearly this was our first dance wedding song
Shania Twain - From This Moment On - Lyrics - YouTube
Kila nikisikiliza hayo maneno, najua hatukukosea kuuchagua and we both meant every word BAK unawekaje zile link zako?
all the best my dear
the way navokuonaga u deserve the best
nakumbuka siku moja ulisema uligundua kakusaliti ukaingia nae room ukalia hadi mwenyewe akakuonea huruma...from that day nilijua wewe ni mtu wa aina gani..
but mwambie asicheat tena eeeh!
 
all the best my dear
the way navokuonaga u deserve the best
nakumbuka siku moja ulisema uligundua kakusaliti ukaingia nae room ukalia hadi mwenyewe akakuonea huruma...from that day nilijua wewe ni mtu wa aina gani..
but mwambie asicheat tena eeeh!
Asante rafiki,
Umenichekesha sana unavyokumbuka mastori ya hapa na pale. kwa kweli haijawahi tokea tena, hata jana alikumbusha alivyonifanya nilie ile siku na kuijutia sana. kila mwaka siku kama ya leo, pamoja na mengi tunayoyafanya, huwa tunaulizana ni kitu gani ambacho uliwahi kumfanyia/kufanyiwa na mwenzio na uka-regret. Huwezi amini kila mwaka hiyo ndo regret yake............ Namshukuru Mungu kwa hilo
 
Back
Top Bottom