Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema watendaji wa Rais Jakaya Kikwete wanamwangusha katika utendaji wake na kumfanya aonekane kama mbabaishaji.
Akijenga hoja yake, Lipumba alitoa mfano wa wasaidizi wa karibu wa rais wanaotakiwa kuchapisha hotuba zake katika tovuti kuwa hawajawahi kufanya hivyo tangu Juni mwaka huu.
Alisema kutokuwekwa kwa hotuba hizo za Rais Kikwete kwa miezi minne, kunawanyima fursa watu ya kufahamu hali ya maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Tanzania kupitia tovuti hiyo ya serikali.
Alisema hotuba ya mwisho ya Rais Kikwete iliyochapwa katika tovuti ya serikali, ni ya Juni 20, iliyotolewa wakati wa hafla ya kuchangisha fedha za kusaidia taasisi ya kuhifadhi misitu na wanyamapori.
Pia hotuba ya kiswahili ya mwisho, ni ile aliyoitoa mkoani Dodoma wakati akifungua jengo jipya la Bunge Juni 12 na taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari ya mwisho iliyoko kwenye tovuti hiyo ni ya Juni 23, mwaka huu, inayozungumzia "China imeipatia Tanzania Yuan milioni 80".
"Kasi mpya ya wanamtandao haijafika kwenye mtandao wa elektroniki. Hili siyo jambo la mzaha...viongozi wa nchi ambazo Rais anatembelea wanatayarishiwa maelezo ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa hotuba za Rais.
Hivi katika miezi ya Julai, Agosti, Septemba, Oktoba na Novemba, Rais hajatoa hotuba inayostahili kubandikwa kwenye tovuti ya serikali. Wachambuzi wa nje wanaweza kufikiria kuwa Rais wetu ni mbabaishaji tu kumbe anaangushwa na wasaidizi wake," alisema.
................
Full article at:
http://www.habaritanzania.com/articles/1670/1/Wasaidizi-wa-Rais-Kikwete,wasaidizi-wake-wakosolewa