We mbaba unaacha ngapi ya mezani?

We mbaba unaacha ngapi ya mezani?

Labda kila watu wana utaratibu,suala la kuacha kodi ya meza kila siku sina uzoefu nayo,baba anafanya hivi anatoa kama laki tatu au nne kuna kinotebook hiyo hela inakaa ko ukitaka kununua kitu unachukua hapo hela,haijalishi una stock ndani,na baada ya mda anakuwa anaongeza hela.
NOTE.Nadhani anafanya vile kwa sababu mimi sina matumizi ya hovyo(kwa kweli mi ni bahiri)na pia sina shida na hela ndogo ndogo.Sasa jichanganye kwa hawa vichwa maji eti unaacha keshi laki ngapi utajuta mbona.
 
Weka mambo hadharani.

Ukweli utakuweka huru

Hivi wamama na wao wanaacha ya mezani au tuwaache kwanza?
"Kuacha hela ya kula" Ni mipango ya maisha ya uswahilini sana isee!

Na mkeo usipomshirikisha kutengeneza bajeti tu ndogo ya chakula hapo nyumbani, mpaka uache cash kila siku unamuandalia dhahama kubwa sana katika future yake.

Wee mwanaume hivi unaijua kesho yako?

Let say umegongwa barabarani huko umekata moto, umezolewa na patrol kwa uzurulaji wako umeenda kuswendemwa ndani na mambo yafananayo na hayo, huyo mkeo na watoto kwa siku hiyo usiyokuwepo ghafla wataishije?

"Kuacha hela ya kula" ni maisha ya kishamba shamba na uswahili swahili ambapo mtu aliyestaarabika hauwezi kuona comment yake hapa akijadili chochote, maama ni maisha ya aibu sana hata kuyaongelea.

Maisha ya namna hiyo hayaendani na kipato bali ni tabia ambayo makabila mengine huita 'ubhanzi', tabia ya kuhesabu finyango za nyama jikoni na kuelekeza mke asipike chakula cha ziada ya ulichokitoa hata kama mgeni kaja hadi kwa kibali chako!
 
Kumbe nikioa kuna suala la kuacha kitu mezani asee 🙌, Zoezi la kuoa nimelisogeza mbele miaka saba tena ili nifanye mazoezi ya kuacha mezani kwanza.
 
15k-20k(ya dharula)
Unga wa sembe, mchele, ngano, viazi mviringo, viazi rishe, nyanya, carrots, Hoho, mafuta ya kula, gas, ndimu, tangawizi, vitunguu swaumu, vitunguu maji
Vyote vipo
 
"Kuacha hela ya kula" Ni mipango ya maisha ya uswahilini sana isee!

Na mkeo usipomshirikisha kutengeneza bajeti tu ndogo ya chakula hapo nyumbani, mpaka uache cash kila siku unamuandalia dhahama kubwa sana katika future yake.

Wee mwanaume hivi unaijua kesho yako?

Let say umegongwa barabarani huko umekata moto, umezolewa na patrol kwa uzurulaji wako umeenda kuswendemwa ndani na mambo yafananayo na hayo, huyo mkeo na watoto kwa siku hiyo usiyokuwepo ghafla wataishije?

"Kuacha hela ya kula" ni maisha ya kishamba shamba na uswahili swahili ambapo mtu aliyestaarabika hauwezi kuona comment yake hapa akijadili chochote, maama ni maisha ya aibu sana hata kuyaongelea.

Maisha ya namna hiyo hayaendani na kipato bali ni tabia ambayo makabila mengine huita 'ubhanzi', tabia ya kuhesabu finyango za nyama jikoni na kuelekeza mke asipike chakula cha ziada ya ulichokitoa hata kama mgeni kaja hadi kwa kibali chako!
mkuu hayo ndo maisha ya kawaida kabisa ya zaidi ya 90% ya watzania wanaoishi chini ya dola moja.

Kama umezaliwa ushuani hauwezi kujua
 
Kumbe nikioa kuna suala la kuacha kitu mezani asee , Zoezi la kuoa nimelisogeza mbele miaka saba tena ili nifanye mazoezi ya kuacha mezani kwanza.
ndio mkuu. Oa bana upikiwe na mtoto wa watu.
 
mkuu hayo ndo maisha ya kawaida kabisa ya zaidi ya 90% ya watzania wanaoishi chini ya dola moja.

Kama umezaliwa ushuani hauwezi kujua
Siyo kukulia ushuani wala nini, isipokuwa kunyofoa kila siku toka mfukoni hela ya chakula, wewe unaona ni njia sahihi ya kuhandle familia?

Hata ukiwa na kipato kidogo kiasi gani lazima ujue kuna magonjwa, uzima na kifo.

Tengeneza mazingira ambayo, familia yaweza kusimama hata bila kutegemea pesa za kila siku za mfukoni mwako.

Na pia familia isikushinikize kutoa hela ya kula kila siku, maana siku zote siyo jumapili, kuna kupata, kukosa pamoja na majanga mengine niliyoyaeleza hapo juu.
 
Pesa inayoachwa mezani ni Kwa ajili ya dharura ndogo ndogo, baada ya kuhakikisha chakula kimo ndani, mboga nk nk.
 
Back
Top Bottom