We Condemn: Calling for A National Day of Mourning

Kwa wataalamu wa sheria je kwa matumizi ya nguvu iliyooneshwa na polisi kwenye maandamano yaliyopelekea vifo vya ndugu zetu wawili. Jeshi la poplisi haliwezi kushtakiwa? Au wao wako juu ya sheria na kila wasemacho sie akina yakhe lazima tukubali tu?
 
Mimi pia tatizo langu ni hawa Polisi kuwakamata viongozi wetu na kuwalaza selo.Hivi kweli wameshindwa kuwa na busara hata kidogo?Hivi wangekuwa ni viongozi wa CCM wangewakamata na kuwaweka selo?IGP,Andengenye mngefanya hivi kweli?Hivi kweli upolisi ni kutumia nguvu tu,hakuna kutumia akili?Mmelidhalilisha jeshi la polisi.Mbona mataifa yaliyoendelea hayafanyi hivi?hivi polisi maana yake nini?

Sitaki kuamini kuwa hili ndilo kubwa zaidi uliloliona Regia..
 
Katika nchi ya kidemokrasia neno la Polisi si la mwisho. Polisi hawawezi kutoa amri tu kwa vile ni polisi na wananchi watii tu kama is unreasonable and immoral. Polisi hawakuwa na sababu ya kusitisha maandamano hayo. Walisitisha kwa sababu wao "ni polisi" na si kwa sababu kulikuwa na sababu ya kuyasitisha. Mtu mwenye dhamira safi hakupaswa kutii maana tukikubali tu kuwa polisi wakiamuru chochote kwa vile wao wani polisi basi watu wakubali maana yake tunauza uhuru wetu na haki yetu ya kupinga.
Mzee Mwanakijiji!
Hapo Nchi ulipo polisi akitoa amri usiandamane na ukaendelea kuandamana huku nyumba zinavunjwa,biashara za watu mitaani zinakuwa mashakani kweli watakuacha uandamane tu kwasababu ni nchi ya kidemokrasia? Hapo Nchi ulipo polisi sio akisema bali hata akikuwashia taa tu weka gari pembeni halafu ikitokea hata hiyo ishara hukielewa au hukuona nini kinaendelea nini kitatokea? Na endapo umetii au bado unashangaa amri ya weka mikono ionekane nini kinafuatia?Au hiyo si nchi ya demokrasia?Pili sheria za Tanzania zinasema nini kuhusu maandamano?Labda kabla ya kwenda mbali tuelewe sheria ya kuandamana kwa mujibu wa katiba inasemaje kwa Tanzania na Kanuni za utekelezaji wake zinaainisha ni nini kifanyike ili maandamano yawepo na yakubalike kuwa ni ya kisheria.
 
1. KNKU, kabla ya hayo matukio ya uvunjaji wa sheria (ambayo uhalifu ni uhalifu tu) waandamanaji Arusha walikuwa wamefanya vurugu gani?

2. Je Polisi hawakuweza kutoa ulinzi wa kutosha wa kuhakikisha kuwa maandamano yanaenda vijwanjaji kwa amani? Huku hawawezi kuzuia maandamano kirahisi rahisi tu ati kwa sababu hawataki. Ukizuia maandamano hapa unashtakiwa ili ukatoea sababu zako na usipokuwa na sababu uanweza hata kulipiishwa.

3. Kusema "sheria" siyo jambo la kurukia hivi hivi. Wakati wa civil rights movement sheria ilisema watu wasifanye hivi au vile na maeneo mengine serikali ya jimbo na mahali waliipiga marukufu maandamano. Guess what watu waliandamana na kupigwa risasi kwa sababu haikuwa amri halali. Hakukuwa na sababu ya msingi ya kuzuia watu kuandamana Arusha, wakati ilikuwepo sababu ya msingi ya wanasiasa kuandamana.
 
We are a land of laws, rules, and regulations. This is an example of disgruntled politicians, using their rhetorical prowess to push the public to the limit and argue them to disobey the law.

Kama polisi walisema maandamano hakuna, kwanini muandamane?

Inalilahi waina lillah rajiun (Hakika sisi ni wa Allah, na kwake tutarejea)

Kwa vile polisi wamesema maandamano hakuna, hivyo atakayekiuka hilo ni KUUAWA?

Think again!

Kwa IGP kutangaza ati Maandamano yasiwepo lakini mkutano uendelee kama kawaida inaleta ushawishi kuwa huyu IGP hana uwezo wa kufikiri na hana taadhima na busara. Mkutano uwepo, utahudhuriwa na watu, je hawa watu watakwendaje kwenye mkutano na kutumia njia gani? Kwa kutembea au kwa magari, baiskeli au la mmoj mmoja au makundi?

La pili, ambalo linafuta kabisa uhalali wa IGP na polisi statement zote ni kuwa kama Raia hawakufanya fujo kabla polisi ya kuanza kuwapiga, je ni uhalali gani wa kulinda amani, wakati mlinzi wa amani anaanzisha fujo kwa kupiga watu. Logic ni kuwa polisi walizuia maandamano yasifanyike kwa sababu ya "intelligensia" kutatokea fujo. Vijana hawakuleta fujo, lakini polisi walileta fujo kabla hata vijana hawajaleta fujo.

La tatu, kama mie ni mlinzi wa amani I must know my clients, to whom I am rendering these services. Polisi si ubabe tu, bali na akili vile vile itumike. Kama IGP na Polisi wangekuwa karibu na vyama vyote, wangewajua vema wateja wao, wananchi vyama vya siasa nk. Kwenye real polls Dr. Slaa anakubalika na WaTanzania zaidi ya 50% meaning that Dr. Slaa ni among the biggest clients of peace in this country. Polisi lazima wawe na "dialogues" na such people and political parties. Hawa polisi hata Baada ya mandamano kwisha kwa amani wangekuwa na wakati mzuri zaidi kuongea zaidi na DR Slaa na Chadema kuhusu future peace. Polisi Hawaawezi tu kufanya kazi za CCM muda wote. They are not the sole clients of peace of this country, they are part of it.

This sitting president has proved failure, and must be condemned, anaharibu nchi socially, politically and economically, nchi yetu imekwisha otherwise vijana simameni msiogope!
IO!
Kwenda mkutanoni si lazima uandamane, kwenda sehemu ya mkutano bila ya kuandamana inawezekana kabisa na wala tusitake kuyafanya haya mambo mawili tofauti kuwa moja.Tatizo ni viongozi wa chadema ambao wanaelewa kabisa ajenda yao ni kuandamana na si kufanya mkutano tu sasa tusijaribu kupotosha ukweli.
Sielewi unaposema Dr Slaa ni mteja wa amani nchi hii, inakuwaje mteja wa amani anaruhusiwa kufanya mkutano na yeye anaitisha maandamano huku akielewa kabisa yataleta mfarakano na jeshi la polisi ambayo limeshasema kwasababu za kiusalama wasiandamane siku zote ninasema wanasiasa waliowengi ni wabinafsi na Kwa hili Dr Slaa ameingia kwenye kundi hilo kwani anaposema hataki damu ya watanzania imwagike ni maneno mazuri na yenye busara lkn anapowaongoza watanzania waende kituo cha polisi ili wakawatoe baadhi ya wanachama ambao wametiwa mbaroni na jeshi la polisi hata kama kwa mtazamo wao si kihalali hiyo ni fujo na nia aibu kwa mtu ambaye alimanusura angekuwa amiri jeshi wetu mkuu.Kwanini asifuate njia za kisheria kwenda kuwatoa kama kuwachukulia dhamana na baadae waiachie mahakama ifanye kazi ya kuona uhalali wa kukamatwa kwao na kama kisheria wana hatia au laah.
Maandamano kwenye nchi zetu siku zote yanawalakini na mojawapo ni kujumuisha wenye kuandamna kwa lengo zuri na vibaka na waharibifu wa mali za wananchi.Huu ndiyo ukweli sasa kuna wanaopinga ni haki yao lkn maandamano kwenye nchi za dunia ya tatu ni fujo mara nyingi.
 
KNKU, kwanini Polisi walizuia maandamano na kuyatawanya wakati yalikuwa yanaenelekea uwanjani kwa njia ya amani?
 
We are a land of laws, rules, and regulations. This is an example of disgruntled politicians, using their rhetorical prowess to push the public to the limit and argue them to disobey the law.

Kama polisi walisema maandamano hakuna, kwanini muandamane?

Inalilahi waina lillah rajiun (Hakika sisi ni wa Allah, na kwake tutarejea)
Inasikitisha sana, watu wanajua kabisa Polisi wa Tanzania hii leo wanataka kufanana na wale wa SA enzi za kaburu lakini wanatia pamba masikioni. Je hawa wanasiasa wanataka tufe tuishe kwa jina la ukombozi kisha watamtawala nani? Tunahitaji watu wao wanawapeleka kwenye maafa... sielewi
 
1. KNKU, kabla ya hayo matukio ya uvunjaji wa sheria (ambayo uhalifu ni uhalifu tu) waandamanaji Arusha walikuwa wamefanya vurugu gani?

2. Je Polisi hawakuweza kutoa ulinzi wa kutosha wa kuhakikisha kuwa maandamano yanaenda vijwanjaji kwa amani? Huku hawawezi kuzuia maandamano kirahisi rahisi tu ati kwa sababu hawataki. Ukizuia maandamano hapa unashtakiwa ili ukatoea sababu zako na usipokuwa na sababu uanweza hata kulipiishwa.

3. Kusema "sheria" siyo jambo la kurukia hivi hivi. Wakati wa civil rights movement sheria ilisema watu wasifanye hivi au vile na maeneo mengine serikali ya jimbo na mahali waliipiga marukufu maandamano. Guess what watu waliandamana na kupigwa risasi kwa sababu haikuwa amri halali. Hakukuwa na sababu ya msingi ya kuzuia watu kuandamana Arusha, wakati ilikuwepo sababu ya msingi ya wanasiasa kuandamana.
Mzee Mwanakijiji!
Sababu za msingi kwa jeshi la polisi zilikuwepo na ndiyo maana waliruhusu mkutano na si maandamano.Sababu za msingi za wanasiasa kuandamana ni zipi?Kama ni uchaguzi wa meya si waliamua kususia na baada ya kuzidiwa kete na CCM ndiyo wakaja na hoja mbadala ambayo ina uzito kama watafuata mkondo wa sheria kumuengua huyo meya na si maandamano.Siasa za Jazba na kila kukicha maandamano yasiyokuwa na uhakika wa kuisha kwa amani wala hayana tija.
 
Sulemani una akili mgando kama huna mtindio wa akili.
Hakuna mtu aliye lazimishwa kuandamana na viongozi wa Chadema. Baadhi ya Viongozi walitoka mikoanai na kufikia hotelini. Walikuwa wanatoka Hotelini kwenda kwenye mkutano.... je hayo ni maandamano? Hata kama ni maandamano kwa tafsiri yako, yalikuwa na athari gani kwa watu wengine na mali zao?
Kuwa na fikra bora ingawa najua ubongo wako hauwezi kufikiria vizuri.
Kwanini viongozi wa Chadema walishinikiza wananchi waandamane wakati dola ya nchi ilipiga marufuku? Hebu jiulize hilo kwanza. Chadema leadership is responsible kwa kushinikiza wananchi to be involved in an illegal act. Tukubaliane hilo kwanza.
 
IO!
Kwenda mkutanoni si lazima uandamane, kwenda sehemu ya mkutano bila ya kuandamana inawezekana kabisa na wala tusitake kuyafanya haya mambo mawili tofauti kuwa moja.Tatizo ni viongozi wa chadema ambao wanaelewa kabisa ajenda yao ni kuandamana na si kufanya mkutano tu sasa tusijaribu kupotosha ukweli.
Sielewi unaposema Dr Slaa ni mteja wa amani nchi hii, inakuwaje mteja wa amani anaruhusiwa kufanya mkutano na yeye anaitisha maandamano huku akielewa kabisa yataleta mfarakano na jeshi la polisi ambayo limeshasema kwasababu za kiusalama wasiandamane siku zote ninasema wanasiasa waliowengi ni wabinafsi na Kwa hili Dr Slaa ameingia kwenye kundi hilo kwani anaposema hataki damu ya watanzania imwagike ni maneno mazuri na yenye busara lkn anapowaongoza watanzania waende kituo cha polisi ili wakawatoe baadhi ya wanachama ambao wametiwa mbaroni na jeshi la polisi hata kama kwa mtazamo wao si kihalali hiyo ni fujo na nia aibu kwa mtu ambaye alimanusura angekuwa amiri jeshi wetu mkuu.Kwanini asifuate njia za kisheria kwenda kuwatoa kama kuwachukulia dhamana na baadae waiachie mahakama ifanye kazi ya kuona uhalali wa kukamatwa kwao na kama kisheria wana hatia au laah.
Maandamano kwenye nchi zetu siku zote yanawalakini na mojawapo ni kujumuisha wenye kuandamna kwa lengo zuri na vibaka na waharibifu wa mali za wananchi.Huu ndiyo ukweli sasa kuna wanaopinga ni haki yao lkn maandamano kwenye nchi za dunia ya tatu ni fujo mara nyingi.
Ndio maana ninasema hapa tena HATUPASWI KUMUAMINI MWANASIASA YEYOTE HATA KAMA NI MZAZI AMA NDUGU YETU. KWANI SIASA NA UONGO NI MAPACHA. Mwanasiasa atamlaghai mteja wake na yanapotokea yanayotokea basi yeye hupata msamiati mpya kutokana na tukio. Mwisho wa siku mwanasiasa huyohuyo hupeana mikono na kucheka na adui yake.

Watanzania wenzangu... Hapa turejee yale ya Mkwere.. Za mbayuwayu tuchanganye na zetu kwa Tanzania tuitakayo.
 
Sulemani una akili mgando kama huna mtindio wa akili.
Hakuna mtu aliye lazimishwa kuandamana na viongozi wa Chadema. Baadhi ya Viongozi walitoka mikoanai na kufikia hotelini. Walikuwa wanatoka Hotelini kwenda kwenye mkutano.... je hayo ni maandamano? Hata kama ni maandamano kwa tafsiri yako, yalikuwa na athari gani kwa watu wengine na mali zao?
Kuwa na fikra bora ingawa najua ubongo wako hauwezi kufikiria vizuri.
Walitoka mikoani....!!! Na wengine walitoka nchi jirani!!!
 
KNKU, kwanini Polisi walizuia maandamano na kuyatawanya wakati yalikuwa yanaenelekea uwanjani kwa njia ya amani?
Mzee Mwanakijiji!
Kwanini Uandamane wakati ulishaambiwa kibali cha kuandamana kimesitishwa na waliokitoa lkn kama mnataka kufanya mkutano fanyeni.Pili kama Chadema leo hii wanatuambia kwamba kuandamana hakuhitaji kibali kwanini basi walikiomba ilihali wakijua kwamba hakihitajiki? Hivi hawa chadema mbona kule kigoma ambapo kulikuwa na mzozo kama wa Arusha baada ya kufuataa taratibu mbona walifanikiwa.Mafanikio hayaletwi na
Maandamano YA KILA KUKICHA.huko wanapotaka kutupeleka sipo Uchaguzi umeisha na hakuna njia ya mkato wanachotakiwa wajipange kujenga msingi imara wa kuleta mabadiliko na waache siasa za post election fever za kutaka kuligharimu taifa wanataka kuipinga serikali waipinge kwa hoja na ktk njia zenye kueleweka na maandamano ya dunia tatu ambayo hayana uhakika ya kuisha kwa amani hata kama yataanza kwa amani kwani historia ya maadamano Bongo kila yanapopita na vibaka, wafanya fujo na wavunja amani nao hujitumbukiza kwa jina la maandamano.
 
Ni mwendawazimu tu anaeweza kukubali kuwa nguvu ya polisi ya kuyalinda maandamano yawe ya amani ni kubwa kuliko ile ya kuzuia maandamano. Kadhalika, ni mwendawazimu tu anaeweza kukubali kuwa gharama ambayo taifa linalipa baada ya kujaribu kuzuia haya maandamano ni ndogo kuliko ambayo tungelipa kama maandamano yangeruhusiwa. Ni mwendawazimu tu, ambaye anaweza kukubali kuwa Jeshi la polisi halipaswi kuwajibika ila chadema.

Nailaani serikali ya CCM na jeshi lake kwa kitendo hiki.
 
To show u that the Police went beyond their legal power Mr. Mwema and Andengenye will be prosecuted in their personal capacities to be a lesson to other public officials ambao wanafikiri wanauwezo na haki ya kuamuru lolote hata kama ni kinyume cha sheria.
Asante Mzee Mwanakijiji kwa hili. Mimi nina mawili, naanza la la pili halafu nitamalizia la kwanza.
Pili: Siku za nyuma tuliwahi kujadili mahali humu humu jf kuhusu watu wenye mamlaka za ajabu, zaidi ya rais, nilimtaja mtu anayeitwa DPP, huyu ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kukubali shitaka la jinai lifunguliwe au la, na hakuna mamlaka nyingine yoyote, hata rais, hana uwezo wa kuihoji mamlaka ya DPP.
Ili kumshitaki Mwema na RPC wa Arusha, lazima upate kibali cha DPP ndipo ufungue shitaka la jinai. Hata kufanya tuu uchunguzi wa jinai, private presecution, lazima upate kibali cha DPP. Hivyo ni ngumu sana kuwashitaki hawa jamaa kwa mashitaka ya kawaida unless kama ni kuwafungulia mashitaka ya madai na sio jinai.

Wanasheria wa Chadema, wanaweza kupeleka mashitaka dhidi ya watendaji wa serikali not at their personal capacity but at their official capacity kwa kutumia hati tatu za dharura 'certiorary', 'mandamus' na 'prohibition' ambazo huweza kusikilizwa na mahakama sio kwa yaliyotokea Arusha, bali kwa kuizuia serikali, isizuie tena maandamano ya Chadema na mikutano ya Chadema, au jeshi la polisi, kuamriwa kutimiza wajibu wake bila kuvuruga amani, ila the burden of proof lies with the prosecution kwa Chadema kuithibitishia mahakama 'beyond reasonable doubt' kuwa chanzo cha vurugu ni ile intarvention ya Jeshi la Polisi na sio wana Chadema, kwamba wao walikuwa wakiandamana kwa amani mpaka wapoingiliwa na jeshi la polisi ndipo vurugu zikafuatia.

Narudi kwenye la kwanza: Kilichotokea Arusha, kwa maoni yangu, kuna kitu zaidi ya hiki kinachoonekana. Sababu za polisi kuyazuia maandamano kwa kisingizio cha taarifa za kiiteligensia ni 'scapegoat' tuu za kupata kisingizio, there must be other undeliying motives behind, sasa hizi 'motive behind' ndizo wapenda haki na tusio na ushabiki wa upande wowote, ndio tunatakiwa kuzifanyia kazi, kama imefikia hatua ya polisi kutumia risasi za moto, sio bure kuna jambo la zaidi ya maandamano, au mkutano wa hadhara.

Kama RPC Arusha alitoa kibali, aliyetakiwa kukifuta kibali ni huyo huyo RPC na sio kamanda Mwema tena kwa kutumia media. Nilipomuona tuu Saidi Mwema mwenyewe anazungumzia kuzua maandamano ya Chedema, yaani Mkuu wa Polisi mwenyewe!, hisia zangu zilinituma kuna jambo polisi wamepanga kulitenda, hivyo taarifa ya Mwema kuzuia was just 'caveat' ili likitokea la kutokea, asema tusilaumiane tuliwaambia!.

Kuna wanabalozi wa nchi fulani, wana hasira sana na serikali ya Tanzania kwa upuuzi uliofanywa na jeshi la polisi huko Arusha, wametumia mamilioni ya fedha kuwaelimisha polisi wetu jinsi ya ku-deal na political ralies na demos, wamewapeleka nchini kwao kuwapika kuanzia huyo kamanda Mwema mwenyewe mpaka maofisa wake, kumbe kule walikuwa wanakwenda kula per diem tuu na kufanya shopping ya wake na vimada wao!.

Sheria za polisi ziko wazi kabisa, usitumie nguvu kubwa than necesary to contain riot, polisi wametumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji wasio la silaha!. This is an acceptable!.

Ila na viongozi wa Chadema, next time, don't try patience ya serikali vichaa!, wewe umeshaijua serikali yako, inaongozwa na viongozi wenye vichaa, totally insane!, unamuona kichaa mbele yako kashika rungu anatishia kukupiga nalo!, wewe kama una akili timamu, si utamuepuka!.
Wewe ndio kwanza unaendelea kumfuata huku ukimwambia jaribu tuone!...

Mambo mengine yanatia hasira, uchungu na maumivu makubwa ya nafsi!

RIP Damu zilizomwagika Arusha, hazitapotea bure, someone must pay kwa kutumia law of the 'karma'!.
 
Ni mwendawazimu tu anaeweza kukubali kuwa nguvu ya polisi ya kuyalinda maandamano yawe ya amani ni kubwa kuliko ile ya kuzuia maandamano. Kadhalika, ni mwendawazimu tu anaeweza kukubali kuwa gharama ambayo taifa linalipa baada ya kujaribu kuzuia haya maandamano ni ndogo kuliko ambayo tungelipa kama maandamano yangeruhusiwa. Ni mwendawazimu tu, ambaye anaweza kukubali kuwa Jeshi la polisi halipaswi kuwajibika ila chadema.

Nailaani serikali ya CCM na jeshi lake kwa kitendo hiki.
Ni mwendawazimu vile vile anayeweza kukubali kwamba kama hayo mandamano yangesitishwa kama ilivyoamriwa na aliyetoa kibali na kuzuia baadaye na kuruhusu mkutano yangetokea yaliyotokea ikiwemo kupoteza maisha ya binaadamu wenzetu.Kama kweli Chadema walikuwa na la maana la kuwaeleza wananchi kuna lipi lingeshindikana kuzungumzwa kwenye mkutano ulioruhusiwa na si maandamano.Hapa ndiyo unapoona wazo la kuandamana lilikuwa ni poor judgement kwa upande wa uongozi wa chadema nafikiri wangeweza kupata faida zaidi kama wangeweza kufanya mkutano walioruhusiwa na vile vile kusingekuwa na majeruhi wala vifo.
 
Asante Mzee Mwanakijiji kwa hili. Mimi ni na mawili, naanza la la pili halafu nitamalizia la kwanza.
Pili: Siku za nyuma tuliwahi kujadili mahali humu humu jf kuhusu watu wenye mamlaka za ajabu, zaidi ya rais, nilimtaja mtu anayeitwa DPP, huyu ndiye mwenye mamlaka ya mwisho ya kukubali shitaka la jinai lifunguliwe au la, na hakuna mamlaka nyingine yoyote, hata rais, hana uwezo wa kuihoji mamlaka ya DPP.
Ili kumshitaki Mwema na RPC wa Arusha, lazima upate kibali cha DPP ndipo ufungue shitaka la jinai. Hata kufanya tuu uchunguzi wa jinai, private presecution, lazima upate kibali cha DPP. Hivyo ni ngumu sana kuwashitaki hawa jamaa kwa mashitaka ya kawaida unless kama ni kuwafungulia mashitaka ya madai na sio jinai.

Wanasheria wa Chadema, wanaweza kupeleka mashitaka ndidi ya watendaji wa serikali not at their personal capacity but at their official capacity kwa kutumia hati tatu za dharura 'certiorary', 'mandamus' na 'prohibition' ambazo huweza kusikilizwa na mahakama sio kwa yaliyotokea Arusha, bali kwa kuizuia serikali, isizuie tena maandamano ya Chadema na mikutano ya Chadema, kwa Chadema kuithibitishia mahakama kuwa chanzo cha vurugu ni ile intarvention ya Jeshi la Polisi na sio wana Chadema, kwamba wao walikuwa wakiandamana kwa amani mpaka wapoingiliwa na jeshi la polisi ndipo vurugu zikafuatia.

La kwanza: Kilichotokea Arusha, kwa maoni yangu, kuna kitu zaidi ya hiki kinachoonekana. Sababu za polisi kuyazuia maandamano kwa kisingizio cha taarifa za kiiteligensia ni 'scapegoat' tuu za kupata kisingizio, there must be other undeliying motives behind, hizo ndizo tuzitafute na kuzifanyia kazi, kama imefikia hatua ya polisi kutumia risasi za moto, sio bure kuna jambo la zaidi ya maandamano, au mkutano wa hadhara.

Kama RPC Arusha alitoa kibali, aliyetakiwa kukifuta kibali ni huyo huyo RPC na sio kamanda Mwema tena kwa kutumia media. Nilipomuona tuu Saidi Mwema mwenyewe anazungumzia kuzua maandamano ya Chedema, yaani Mkuu wa Polisi mwenyewe!, hisia zangu zilinituma kuna jambo polisi wamepanga kulitenda, hivyo taarifa ya Mwema kuzua ni just 'caveat' ili likitokea la kutokea, asema tusilaumiane!.

Kuna wanabalozi wa nchi fulani, wana hasira sana na serikali ya Tanzania kwa upuuzi uliofanywa na jeshi la polisi huko Arusha, wametumia mamilioni ya fedha kuwaelimisha polisi wetu kudeal na political ralies na demos, wamewapeleka nchini kwao kuwapika kuoanzia huyo kamanda Mwema mwenyewe mpaka maofisa wake, kumbu kul;e walikwenda kula per diem tuu na kufanya shopping ya wake na vimada wao!.

Sheria za polisi ziko wazi kabisa, usitumie nguvu kubwa than necesary to contain riot, polisi wametumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji wasio la silaha!. This is an acceptable!.

Ila na viongozi wa Chadema, next time, don't try patience ya serikali vichaa!, wewe umeshaijua serikali yako, inaongozwa na viongozi wenye vichaa, totally insane!, unamuona kichaa mbele yako kashika rungu anatishia kukupiga nalo!, wewe kama una akili timamu, si utamuepuka!.
Wewe ndio kwanza unaendelea kumfuata huku ukimwambia jaribu tuone!...

Mambo mengine yanatia hasira, uchungu na maumivu makubwa ya nafsi!

RIP Damu zilizomwagika Arusha, hazitapotea bure, someone must pay kwa kutumia law of the 'karma'!.
Pasco!
Mimi sikuelewi hivi ulitaka hawa Polisi wafanye nini wakati Dr Slaa akiwaongoza umati wa watu wenye hasira kuelekea kituo cha polisi kwa kile wanachodai kuwatoa wanachama wenzao.Tunapoangalia mambo tuangalie pande zote husika kabla ya kutupia lawama pande moja.Waandishi wote wanakiri jeshi la polisi kuzidiwa nguvu kutokana na idadi yao kuwa ndogo.Sasa fikiria wewe ni polisi unazidiwa nguvu na waandamanaji na una bunduki yenye risasi za moto na unaona watu wanakuja kama kundila nyuki unafikiri ni nini kitafuatia kuokoa maisha yako?
 
Tatizo ni kuwa kwako wewe umefumba macho hutaki kuona makosa ya serikali; kwa kufumba kwako macho uko tayari kuacha serikali ifanye lolote kwa mtu yoyote si kwa sababu ni haki au ni sawa bali ni kwa sababu ni serikali. Wakati wa utawala wa ...makaburu kulikuwa na watu waliotaka ANC wasiupinge utawala huo na kuwasihi wakubaliane nao au wauelewe. Ndicho ninachokiona unachokifanya. Kwako wewe, serikali haiwezi kufanya jambo baya. Mawazo yangu yaweza kuwa ni ya unafiki, lakini msimamo wako ni wa hatari kwa taifa letu na ni wajibu wa watu wenye dhamira zao kuwapinga.
 
Hakuna mtu asiyeliona tatizo la polisi lililotokana na mfumo mbaya wa sheria kandamizi, hili ni tatizo la upande mmoja LAKINI naona pia lazima tuliangalie pia tatizo la busara ya Chadema kung'ang'ania kufanya maandamano bila ya kujali athari zake ukizingatiwa kuwa kulikuwa bado na nafasi ya kufanya mkutano na kuyawasilisha yote yaliyotakiwa kuwasilishwa kwa umma mkutanoni bila tatizo lolote, kama wanatambua dhamana waliyonayo kwa wanachama wao iliwapasa kufanya uchambuzi wa faida na hasara ya kufanyika kwa maandamano hayo kabla ya kufikiwa kwa uamuzi huo.

Na kwa upande mwingine yatupasa pia tulione na kulikemea kosa la kauli ya Dr. Slaa kuwaagiza vijana kwenda katika kituo cha polisi baada ya mkutano kuwatoa kwa nguvu viongozi waliokamatwa na hivyo kupelekea vijana kupambana na polisi na kupelekea wengine kuuawa. Dr. Slaa anapaswa kujua kuwa kauli moja mbovu ya kiongozi wa kisiasa inaweza ikaleta madhara makubwa kwa nchi yake na kwa watu wanaomuamini na kumpenda sana, nategemea Dr. Slaa atajifunza katika hili.
 
Pasco!
Mimi sikuelewi hivi ulitaka hawa Polisi wafanye nini wakati Dr Slaa akiwaongoza umati wa watu wenye hasira kuelekea kituo cha polisi kwa kile wanachodai kuwatoa wanachama wenzao.Tunapoangalia mambo tuangalie pande zote husika kabla ya kutupia lawama pande moja.Waandishi wote wanakiri jeshi la polisi kuzidiwa nguvu kutokana na idadi yao kuwa ndogo.Sasa fikiria wewe ni polisi unazidiwa nguvu na waandamanaji na una bunduki yenye risasi za moto na unaona watu wanakuja kama kundila nyuki unafikiri ni nini kitafuatia kuokoa maisha yako?
Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu, naomba kwanza nijibainishe wazi, mimi sio mshabiki wa Chadema wala sishabii fuja, bali ni mtetezi wa haki.
polisi wetu wanatakiwa kufanya kazi sio tuu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, bali pia kwa kutumia common sense. Kwa kilichotokea Arusha, ni polisi imejidhalilisha na sasa naana kum doubt uwezo wa Kamanda Mwema. Enzi za Mahita, hata kwa kumtazama tuu usoni, alionekana empy, lakini ukimtaza Mwema, he has substance, jana nilimshangaa sana alivyotetea vijana wake!.

Njolay akiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Alhamisi moja mwaka 1995, vingozi wa kimila wa Kimasai, Ma Algwanani, waliamuru Morani wao, wachome moto ofisi ya CCM na Nyumba ya Mwenyekiti wa kijiji fulani huko Ngaramtoni, huku wao wakisimamia na ofisi na nyumba ya mwenyekiti wa kijiji zikachomwa.

Ijumaa, Defender ya polisi ikawasomba hao wazee wanne na kusweka polisi Arusha walalala ndani Ijumaa hiyo, Jumamosi na Jumapili,
Jumatatu asubuhi, imji wa Arusha ukavamiwa na Morani wa Kimasai toka pande zote, wameshika shime, ngao na mikuki, wamajipaka yale marangi yao makundu na midomoni kama wamekunwa damu mbichi, hawaongei lolote zaidi ya kuhema kwa mingurumo.

Moja kwa moja mpaka ofisini kwa Njolay pale Regional Bldg. Viongozi wao huku wakizungumza kwa Lugha ya Kimasai, walimuamuru, wanawataka wale Ma Lagwanan wao wanne waachiliwe pale saa hiyo hiyo vinginevyo wataigeuza Arusha nzima dimbwi la Damu within no time!.
Njolay akawashauri, wamsubiri, aitishe kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama, wakajadiliana, Njolay akaishauri kama, wazee wa Kimasai, waachiliwe, Mkuu wa polisi akagoma, kuwa wale ni wahalifu hawawezi kuachiwa, Njolay akaondoka in person mpaka kituo kikuu cha polisi na kuamuru wazee waachiwe, atajibu mbele ya safari, wazee wale waliachiwa, na Wamasai wakarejea nao umasaini.

Hawa si ni walikuwa wahalifu kabisa tena wametenda jinai ya wazi mbele ya kadamnasi ya watu, walifanywa nini?. Huyo Mbowe na wafuasi wake wangeachiwa kuandamana kwa amani mpaka pale uwanjani, huku wakisindikizwa na polisi just ku guarantee usalama, wangepata athari gani?.

Amini nakuambia, hakuna cha habari za inteligensia wala nini, bali baada ya IGP kutangaza wameyazuia maandamano, Chadema waliokataa kutii, polisi wakaamua kuwaonyesha nani zaidi ili kuwakomoa!. Mbele ya jumuiya ya kimataifa hao vijana wa Mwema, wanamuiaibisha nani?, wanawakomoa Chadema, ama wanautia najisi mji wa Arusha ambao ndio kitovu cha utalii?. Hivi hao polisi wana akili timamu kweli?.

Kama Njoolay alipoasses situation aliamua kuwaachia wale wazee wa Kimasai, huyo Andengenya alishindwa nini kua asses?. Lengo la kumshikilia mtu ni kujiridhisha asipotee, people of no fixed abode, unamjua kabisa Godbless Lema ni Mbunge wa Arusha, Mbowe na Slaa ni viongozi wa Chadema, hivi kweli polisi walikuwa na haja ya kuwashikilia usiku kucha kwa kuhofia watatoroka!. Walitakiwa wakishaandika maelezo waawachie na kuwaambia siku ya kuja mahakamani.

Risasi za moto ni kwa wahalifu ama wanaotaka kutoroka, kwanini risasi za moto zinatumika kuwasambaza waandamaji ili hali rubber bullets zipo?.

Kama rais Kikwete atalipongeza jeshi la polisi kwa kazi mzuri iliyofanyika Arusha, sio siri, sitamshangaa, ila nitaamini kuwa kumbe ni kweli, uwezo wake wa kiakili ni ule wa GPA ya below 2.0!.
 
Back
Top Bottom