We Africans, do we always have to learn it the hard way?

We Africans, do we always have to learn it the hard way?

Mara nyingi, mtu anazaliwa na tabia fulani ambazo ni asili yake. Lakini anavyozidi kukua, anaanza kubadilika taratibu kulingana na mazingira, watu wanaomzunguka, au matokeo ya mambo anayokutana nayo.

Ni kwanini maisha ya baadae yanatubadilisha wengi? Mtu anazaliwa mwenye upendo na huruma ila mahusiano na ndoa au watu wabaya wanamkomaza anakuwa na roho ngumu hata kuua anaweza!

Kwa mfano, mtu anaweza asiwe mtu wa mazoezi kabisa. Lakini kwa sababu anataka kuvutia kundi fulani la watu, anaamua kuanza kufanya mazoezi ili kujenga mwili au kuonekana mwenye lifestyle fulani.

Kwanini watu wanashindwa kuwa na hobbies zao wenyewe? Kwa nini mpaka waige maisha ili waonekane wanapenda kusoma, kusikiliza muziki, au kuangalia michezo?

Matokeo yake, unakuta binti au kijana anapofikia kiwango fulani, ili kufit kwenye jamii aliyopo, anaanza kuiga tabia mpya na za ajabu, mwishowe anaharibu maisha yake.

Hapo ndipo ninapojiuliza, hatuwezi kujifunza bila kupitia matokeo magumu? Kwa mfano, mtu anaweza kuugua au kukutana na changamoto fulani, ndipo tunapoanza kusikia ushauri kila kona ya mtandao: "Jamani, jitahidini kufanya 1, 2, 3, mnaona kilichotokea sehemu fulani."

Leo nimeona mada kuhusu trolls, wale wanaobully wenzao mitandaoni ikapelekea binti wa south kujiua ndioo ikageuka mjadala ili iwe funzo lakini nina uhakika hii sio mara ya kwanza, hii changamoto iko moka kwa wenzetu lakini kidogo wao wanabebana baadhi ya matatizo ya kujitakia yanapungua kwa asilimia fulani, ukilinganisha na hali yetu sisi! Tumeathirika na malezi ya utotoni au?

Ni kama taharuki iliyotokea wiki jana kuhusu wale mabinti waliomaliza shule. Ghafla kila mtu anatoa ushauri kuhusu malezi. Utadhani ni jambo geni kufanya malezi ili watoto wawe na tabia njema bila kusubiri matokeo mabaya ndio tujifunze?

Je, ni lazima tujifunze kwa njia ngumu kila wakati?
Mjadala una maana sana na hii ndio jamiiforums tunayoitaka, na wale madogo wanaopenda kulia lia wakihisi njaa inabidi mijadala kama hii ndio darasa kwao.

Nadhani kuna jambo moja tunapaswa kulitambua: binadamu habadilishwi na umri pekee yake, bali pia na uzoefu, mazingira na namna anavyokabiliana na matukio ya maisha.

Mtu anaweza kuzaliwa akiwa na upendo, huruma na moyo wa kujali wengine, lakini akapitia usaliti, mahusiano yenye maumivu, kukataliwa au mazingira magumu kiasi cha kujenga ukuta wa kihisia. Mwishowe anakuwa mtu tofauti na yule aliyekuwa awali. Hii haimaanishi kila anayepitia maumivu lazima awe na roho ngumu; watu huitikia changamoto kwa namna tofauti.
Pia, kuhusu kuiga maisha ya wengine, naamini sehemu ya tatizo ni kutafuta kukubalika katika jamii. Watu wengine hawafanyi mambo kwa sababu wanayapenda, bali kwa sababu wanataka kuonekana wanaendana na kundi fulani. Hapo ndipo mtu anapoanza kupoteza utambulisho wake ili kupata validation kutoka kwa wengine

Pia maisha yanaenda kwa kasi, na si kila mtu ana uwezo sawa wa kuyamudu mabadiliko

Nakumbuka mfano wa kijana aliyefaulu Kibaha Secondary miaka ya 2000, lakini leo amefikia hatua ya kuombaomba vizinga mpaka watu wamemchoka. Hapo unajiuliza, ni nini kilitokea kati ya mafanikio yake ya zamani na hali yake ya sasa? Elimu, akili na mafanikio ya wakati fulan havitoi guarantee ya maisha mazuri milele.

Wakati mwingine tunatamani kuishi maisha fulani bila kutambua kwamba huenda kabla ya kuyafikia tutalazimika kupitia vipindi vigumu ambavyo hatukuwa tumejiandaa navyo

Kwa hiyo, swali sio kwa nini watu wanabadilika tu, lakini pia wanawezaje kujenga uwezo wa kisaikolojia (resilience) wa kukabiliana na mabadiliko bila kupoteza utu wao?

Kujifunza kupitia makosa, naamini hatupaswi kusubiri mtu aumie, augue, apoteze maisha au familia ivunjike ndipo tuanze kutoa elimu. Jamii inapaswa kujifunza kupitia uzoefu wa wengine kabla haijakumbwa na madhara hayo
 
Mjadala una maana sana na hii ndio jamiiforums tunayoitaka, na wale madogo wanaopenda kulia lia wakihisi njaa inabidi mijadala kama hii ndio darasa kwao.
Kabisa!
Nadhani kuna jambo moja tunapaswa kulitambua: binadamu habadilishwi na umri pekee yake, bali pia na uzoefu, mazingira na namna anavyokabiliana na matukio ya maisha.
Kweli
Mtu anaweza kuzaliwa akiwa na upendo, huruma na moyo wa kujali wengine, lakini akapitia usaliti, mahusiano yenye maumivu, kukataliwa au mazingira magumu kiasi cha kujenga ukuta wa kihisia. Mwishowe anakuwa mtu tofauti na yule aliyekuwa awali. Hii haimaanishi kila anayepitia maumivu lazima awe na roho ngumu; watu huitikia changamoto kwa namna tofauti.
Pia, kuhusu kuiga maisha ya wengine, naamini sehemu ya tatizo ni kutafuta kukubalika katika jamii. Watu wengine hawafanyi mambo kwa sababu wanayapenda, bali kwa sababu wanataka kuonekana wanaendana na kundi fulani. Hapo ndipo mtu anapoanza kupoteza utambulisho wake ili kupata validation kutoka kwa wengine

Pia maisha yanaenda kwa kasi, na si kila mtu ana uwezo sawa wa kuyamudu mabadiliko

Nakumbuka mfano wa kijana aliyefaulu Kibaha Secondary miaka ya 2000, lakini leo amefikia hatua ya kuombaomba vizinga mpaka watu wamemchoka. Hapo unajiuliza, ni nini kilitokea kati ya mafanikio yake ya zamani na hali yake ya sasa? Elimu, akili na mafanikio ya wakati fulan havitoi guarantee ya maisha mazuri milele.

Wakati mwingine tunatamani kuishi maisha fulani bila kutambua kwamba huenda kabla ya kuyafikia tutalazimika kupitia vipindi vigumu ambavyo hatukuwa tumejiandaa navyo
Kila usemacho ni sahihi mkuu
Kwa hiyo, swali sio kwa nini watu wanabadilika tu, lakini pia wanawezaje kujenga uwezo wa kisaikolojia (resilience) wa kukabiliana na mabadiliko bila kupoteza utu wao?
Hii ni ngumu sana!
Kujifunza kupitia makosa, naamini hatupaswi kusubiri mtu aumie, augue, apoteze maisha au familia ivunjike ndipo tuanze kutoa elimu. Jamii inapaswa kujifunza kupitia uzoefu wa wengine kabla haijakumbwa na madhara hayo
Kwa jamii yetu ya africa unafkiri inawezekana pia? Au ni kwaajili ya watu wachache tu!
 
Sijui nielezeje
😂😂😂 Nimelog in kwenye PC

Nilikuwa namaanisha kwamba maisha yana changamoto nyingi zinazoweza kumbadilisha mtuUnaweza kusalitiwa, kukataliwa, kufilisika au kupitia mahusiano yenye maumivu.

Je, baada ya kupitia hayo yote, unawza kuendelea kuwa mtu mwenye utu, huruma na busara bila kuruhusu maumivu yako yakufanye uwe mtu mbaya kwa wengne?

Wakati mwingine kwa watu wasio na mental resilience ni ngumu sana lakini maumivu yapo kwa ajili ya kutufunza na ndio hapo unasema hiyo ni ngumu sana
 
Kuna sister mmoja akimdate mtu ni wa kishua sana so mwanaume akigombana nae basi kesi inaenda kwa mzee jamaa anaitwa ana semwa weee na baba mkwe basi imekua hivyo jamaa imebidi azoee tu hana namna watoto wakushua hao,ila ndiyo maana kuna muhimu wakati wa kuoa chunguza mwenza wako amekua na makuzi gani ili ujue unaenda kuishi na mtu wa aina gani
Baada ya kusemwa na baba mkwe kwanini ameendelea kuwa na mahusiano na huyo binti?. Mimi wa kike tu nisingekubali huo ujinga.
 
😂😂😂 Nimelog in kwenye PC

Nilikuwa namaanisha kwamba maisha yana changamoto nyingi zinazoweza kumbadilisha mtuUnaweza kusalitiwa, kukataliwa, kufilisika au kupitia mahusiano yenye maumivu.

Je, baada ya kupitia hayo yote, unawza kuendelea kuwa mtu mwenye utu, huruma na busara bila kuruhusu maumivu yako yakufanye uwe mtu mbaya kwa wengne?

Wakati mwingine kwa watu wasio na mental resilience ni ngumu sana lakini maumivu yapo kwa ajili ya kutufunza na ndio hapo unasema hiyo ni ngumu sana
Sawa sawa
 
Waliogeuka kitu kingine baada ya matokeo fulani!
Sawa ikawe kheri kwako kwenye kubadilika na uwe na muelekeo mzuri pia.
Lakini kukosea sio ujinga na kurudia kosa sio ujinga pia kwahiyo mtu anaweza kurudia kosa ili apate uhakika je alichojifunza kwenye kosa la kwanza ni kitu sahihi au sio sahihi. Ni hvy tu
 
Sijui kama jibu limekuridhisha, that's is according to my life experiences 🙏
Kuna zile experience naongelea anakuwa nazo mtu hata kama atajitahidi kuishi kulingana na jamii aliyopo ila kuna ile ndani alishabaki na majeraha tu!

Mfano mimi zamani nilikuwa nna tabia ya kuamini sana watu, mtu akilia shida kidogo tu niko radhi nitoe pesa yote nimsaidie yeye, ila kwenye kudai sasa unaonekana msumbufu unajibiwa we naye kwani nimekwambia sikulipi! Tangu hapo nmekuwa sina tu!

Mtu anakwambia anakupenda ilihali sio kweli, matendo yake hayaendani na maneno, ikijirudia mara mbili au tatu, unafikiri itakuwa rahisi kwa anayefuata ukamuelewa haraka?

Hiki ndicho ninachomaanisha! Tunabadilishwa kulingana na matokeo na experience tunazozipata!
 
Sawa ikawe kheri kwako kwenye kubadilika na uwe na muelekeo mzuri pia.
Lakini kukosea sio ujinga na kurudia kosa sio ujinga pia kwahiyo mtu anaweza kurudia kosa ili apate uhakika je alichojifunza kwenye kosa la kwanza ni kitu sahihi au sio sahihi. Ni hvy tu
Unaweza kufanya majaribio ukageuka kuwa mfano! Huwa sirudii makosa najifunza kutokana nayo! Huwa mwepesi sana kukimbia ninapokutana na hali kama ile naikwepa!
 
Kuna zile experience naongelea anakuwa nazo mtu hata kama atajitahidi kuishi kulingana na jamii aliyopo ila kuna ile ndani alishabaki na majeraha tu!

Mfano mimi zamani nilikuwa nna tabia ya kuamini sana watu, mtu akilia shida kidogo tu niko radhi nitoe pesa yote nimsaidie yeye, ila kwenye kudai sasa unaonekana msumbufu unajibiwa we naye kwani nimekwambia sikulipi! Tangu hapo nmekuwa mnyimi tu!

Mtu anakwmabia anakupenda ilihali sio kweli,’atendo yake hayaendani na maneno, ikijirudia mara mbili au tatu, unafikiri itakuwa rahisi kwa anayefuata ukamuelewa haraka?

Hiki ndicho ninachomaanisha! Tunabadilishwa kulingana na matokeo na experience tunazozipata!
Hapanimekuelewa. Kweli experience zina nguvu kubwa katika kutengeneza mtazamo na tabia za watu

Lakini kuna tofauti kati ya kujifunza kutokana na maumivu na kuruhusu maumivu ya zamani yaamue namna utakavyowachukulia watu wote watakaokuja kwenye maisha yako

Kwa mfano, ni haki kabisa kujifunza kutokopesha bila utaratibu baada ya kuumizwa, lakini sio lazima uwe na mtazamo kwamba kila anayekuomba msaada ana nia mbaya.

Hata kama mtu akikusababishia maumivu kwenye mahusiano, ni busara kuwa makini kwenye mahusiano mapya lakini si haki kumhukumu mtu mpya kwa makosa ya mtu aliyekutangulia.

Kwa hiyo, uzoefu unatakiwa kutufundisha kuwa na busara zaidi, sio kutufanya tupoteze uwezo wa kuamini, kupenda na kuwa na huruma.

Its not easy, lakini hapo ndipo tofauti ya kupona na kuishi ndani ya majeraha ya zamani inapojitokeza
 
Back
Top Bottom