Our lives were meant to be this way.

Our lives were meant to be this way.

an alpha male

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2022
Posts
1,037
Reaction score
2,246
Hivi ushawahi kujiuliza kuhusu huu mfumo wa kwamba....Kwanza tunahitaji pesa ili kwenda chuo...kisha tunahitaji chuo ili kupata kazi.....kisha tuna hitaji kazi kwaajili ya kupata pesa.

Pesa → Chuo → Kazi → Pesa halafu unarudia tena.
Kama panya kwenye gurudumu. Unaenda mbio, lakini hubadiliki mahali 😵‍💫

Kanuni zake kuu:
1. Unaambiwa upate elimu ili ufanikiwe. Unaingia chuo, madeni yanazidi.
2. Ukihitimu, unaambiwa tafuta kazi ili ulipe madeni na uishi. Kazi inakula masaa 8-10 kwa siku.
3. Mshahara unaopata unakwenda kwenye kodi, rent, chakula, usafiri. Mwezi unaisha kabla hujaonja pesa.
4. Halafu unaambiwa oa ili mtoto wako aje arudie mzunguko huo huo.

Trap yake kubwa:
Inakuuzia uhuru wa baadaye kwa gharama ya wakati wako wa sasa "Vumilia sasa, utapumzika uzeeni."_ Lakini uzee ukifika, mwili umechoka

  • Unaogopa Jumatatu kuliko chochote
  • Unahesabu siku hadi mshahara, halafu siku 3 umeisha
  • "Weekend" ndio maisha yako halisi - masaa 48 kati ya 168
  • Unajiuliza "Mimi nafanya kazi kuishi, au naishi kufanya kazi?"

tunacheza game ambayo rules zake hatukuziandika. Na ukijaribu kutoka, watu wanakuita "mvivu" au "mwotaji".

Nikawa najiuliza ni nani genius aliyetengeneza hii system.....ila nikaja kugundua hakuna mtu mmoja aliyekaa akatengeneza "system" hii

Ilijijenga yenyewe kwa hatua, kwa miaka 300+. Kama mvua inayonyesha kidogo kidogo hadi ikaleta mafuriko.

Nani hasa aliiweka?

1. Mapinduzi ya Viwandani - 1700s hadi 1800s
Hapo ndipo game ilibadilika. Kabla ya hapo, watu walikuwa wakulima. Unalima, unakula.
Alipokuja James Watt na steam engine, matajiri wakajenga viwanda. Wakahitaji watu wengi kufanya kazi masaa 12 kwa siku.

Matokeo: Wakaanza kusema "mtu bila kazi ni mvivu". Mfumo wa mshahara ukaanza.

2. Serikali na Mashule ya Lazima
Karne ya 1800s, nchi kama Prussia na Uingereza zikaona: "Tukitaka wafanyakazi watiifu viwandani, tuwape elimu ya msingi wote."
Ndipo shule za umma zikaanzishwa. Sio kukufanya mbunifu, bali kukufundisha kufika saa 8, kusikiliza amri, kufanya mitihani.

Matokeo: Chuo = Kazi. Formula ikaingia rasmi.

3. Mabenki na Deni
Mfumo wa pesa wa sasa ulipangwa na mabenki makuu. Ukikopa kusoma, unakuwa na deni kabla hujapata kazi. Ukipata kazi, unalipa deni miaka 10-20.

Matokeo: Unazaliwa kwenye mfumo tayari una deni la kutumia pesa. Lazima ucheze game.

4. Makampuni Makubwa na Utangazaji
Baada ya Vita Kuu ya 2, makampuni yakagundua: "Tukitengeneza vitu vingi, nani atanunua?"
Ndipo utangazaji ukawa mkali. Ukauzwa wazo kwamba "furaha = vitu". Gari, nyumba kubwa, simu mpya.

Matokeo: Unafanya kazi zaidi ili ununue vitu usivyovihitaji, kuwavutia watu usiowajali.

Mwisho kabisa matajiri wakanufaika nayo. Serikali zikaiendesha. Wazazi wakaitumia kwa watoto wao kwa sababu "ndio njia pekee". Na sisi tukakubali kwa sababu hatukuona njia nyingine.

Sehemu inayouma System haina "bosi" wa kupigana naye. Ni kama upepo. Unauhisi, unakuzuia, lakini huwezi kuupiga ngumi.

Sasa hiyo ilikuwa ni kama utangulizi wa mfumo wenyewe.

Mfumo wenyewe upo hivi:

"Maisha = shule 👉 kazi 👉 familia 👉 kufa"
Huenda huu ndio mstari mbaya zaidi kuwahi kuandikwa. Kwa sababu ni kweli kwa 90% ya watu lakini pia ni uongo mkubwa ukiangalia kwa jicho la mtu aliyeamka.

Kwanini iwe hivi? Sababu 3 za msingi:*

1. System inapenda utabirifu
Kama kila mtu anafuata mstari huo huo, basi serikali inajua kodi itakusanya lini. Mabenki yanajua nani atakopa lini. Makampuni yanajua nani atanunua gari akiwa 30. Wewe unakuwa ni namba kwenye Excel yao. Mfumo hautaki chaos - unataka kila mtu acheze wimbo ule ule.

2. Hofu inauzika vizuri
Wazazi wanakuogopesha: "Usiposoma utakufa maskini." Shule inakuogopesha: "Usipofanya vizuri hutapata kazi." Kazi inakuogopesha: "Ukifukuzwa utakula nini?"

Matokeo: Unaishi maisha ya kukwepa maumivu, sio kufuata furaha. Na hapo ndipo unajikuta una miaka 45 unauliza "niliishia wapi?"

3. Hatukuwahi kupewa manual nyingine
Tangu utoto tunaambiwa "Soma, oa/olewa, zaa, pumzika mbinguni". Hakuna somo la "Jinsi ya kuishi nje ya mstari". So tunaurithi mzunguko kama magonjwa ya ukoo. Tunafanya kwa sababu "ndio inavyotakiwa" sio kwa sababu tumetaka

Mfumo huu wa shule → kazi → familia → kufa umetengenezwa kwa ajili ya watu wasiouliza maswali. Ukianza kutafakari, ukianza kuona patterns, ukianza kuona vitu "zaidi ya upeo" huwezi tena kutoshea kwenye kisanduku.

Unaweza ukajiuliza ni kwanini ikawepo hii system?...jibu ni hivi

Kwanini mfumo wa shule → kazi → familia → kufa upo?

Sababu 3 za Msingi Zilizofanya Uwepo:

1. Kuli-control Kundi Kubwa la Watu
Fikiria: Uko na nchi yenye watu milioni 60. Kila mtu akifanya anachotaka, akitafakari "zaidi ya upeo" kama mimi, nani atalima, atajenga, atabeba mizigo?

Serikali na wafalme wa zamani waligundua mapema: Ukitoa "script" moja kwa kila mtu, jamii inakuwa tulivu.
  • Shule = inakufundisha kutii muda, kutii amri, kutohoji sana
  • Kazi = inakufanya uwe predictable. Jumatatu hadi Ijumaa upo hapo
  • Familia = inakufunga. Ukiwa na watoto na deni, huwezi kuasi kirahisi

System haijawahi kutengenezwa ili wewe ufurahi. Imetengenezwa ili jamii isianguke. Furaha yako ni bonus sio lengo.

2. Uchumi Unahitaji Watumwa wa Kisasa
Hii ni kali, lakini ni ukweli: Uchumi wa dunia unafanya kazi kwa sababu watu 95% wanafanya kazi wasizozipenda ili wanunue vitu wasivyovihitaji.

Chuo kinakuingiza kwenye deni kabla ya mapato. Unaanza maisha 10 bila

Kazi inakupa mshahara wa kutosha kuishi lakini sio wa kutosha kuacha kufanya kazi

Familia inakuongezea gharama, nyumba, karo, bili. Sasa lazima ufanye kazi zaidi

Tangazo linakuambia unahitaji vitu vipya ili ujisikie umefanikiwa

Matokeo: Unakua kama hamster kwenye gurudumu. Unaendesha uchumi, lakini huwezi kushuka. Ukishuka, system inaporomoka. So inakulazimisha ubaki.

3. Tunaiga Tulichoona kwa Wazazi Wetu
Hii ndio software ya akili. Ubongo wa mtoto unaiga.

Baba aliamka 5 asubuhi kwenda kazini miaka 30. Mama alipika na kulea. Babu alisema "soma mwanangu upate kazi serikalini". Hujawahi kuona model nyingine. So ubongo wako unafikiri "hii ndio maisha".

Ni kama dini. Huulizi kwanini. Unafanya kwa sababu wote wanafanya hivyo. Na ukijaribu kutoka, familia yako yenyewe inakushangaa: "Unataka kuwa tofauti na watu?"

Hofu ya kukataliwa na ukoo inakufanya urudi kwenye mstari. System inajilinda yenyewe kupitia watu tunaowapenda.

Ukweli Mchungu Sana:
Mfumo huu ulifanya kazi miaka 100 iliyopita.Wakati huo kazi ilikuwa shambani au kiwandani. Ulikuwa na uhakika ukisoma utapata kazi miaka 40. Ukioa, mke anakaa nyumbani. Ukizeeka, watoto wanakutunza.

Leo system imeharibika, lakini script haijabadilika.
  • Chuo hakihakikishii kazi tena
  • Kazi moja haikutoi kwenye umaskini tena
  • Familia inavunjika kwa pressure ya pesa
  • Ukiwazeeka, watoto nao wanakimbizana na system

So tunafuata ramani ya miaka 1950, kwenye dunia ya 2026.Ndio maana unaumia. Unacheza game ambayo rules zake zimepitwa na wakati.

Leo acha niishie hapa....always next time.
 
Back
Top Bottom