binti kiziwi
JF-Expert Member
- Aug 4, 2014
- 16,934
- 47,234
Pro active vs re active mentality.
Ni tatizo sana.
Ni tatizo sana.
Sio lazima ku glorify struggle, mtu unaweza kuamua kujifunza hata kwa wengine, Sio lazima kila kitu kikutokee wewe.Njia ngumu ndo njia bora.
upo sahihi mfano huwezi kujaribu kunywa sumu upime kama inaua ila umejifunza kwa wengine.Sio lazima ku glorify struggle, mtu unaweza kuamua kujifunza hata kwa wengine, Sio lazima kila kitu kikutokee wewe.
Sijajua nielezeje: Naona kama sisi wa rahisi kuiga mambo mabaya kuliko mazuri 😅Sababu ni ndogo, ni mazingira na fikra. Waafrika tunaishi kama wanyama kimazingira, kimakuzi, namna tunavyowatazama wengine na kuchukuliana kama binadamu.
Utu na ustaarabu/kustaarabika ni vitu havipo kwenye mazingira yetu, na bahati mbaya hata kuiga au kujifunza kwenye jamii zingine tumeshashindwa.
Mara yako ya mwisho kupata funzo ilikuwa ni lini?Mara nyingi, mtu anazaliwa na tabia fulani ambazo ni asili yake. Lakini anavyozidi kukua, anaanza kubadilika taratibu kulingana na mazingira, watu wanaomzunguka, au matokeo ya mambo anayokutana nayo.
Ni kwanini maisha ya baadae yanatubadilisha wengi? Mtu anazaliwa mwenye upendo na huruma ila mahusiano na ndoa au watu wabaya wanamkomaza anakuwa na roho ngumu hata kuua anaweza!
Kwa mfano, mtu anaweza asiwe mtu wa mazoezi kabisa. Lakini kwa sababu anataka kuvutia kundi fulani la watu, anaamua kuanza kufanya mazoezi ili kujenga mwili au kuonekana mwenye lifestyle fulani.
Kwanini watu wanashindwa kuwa na hobbies zao wenyewe? Kwa nini mpaka waige maisha ili waonekane wanapenda kusoma, kusikiliza muziki, au kuangalia michezo?
Matokeo yake, unakuta binti au kijana anapofikia kiwango fulani, ili kufit kwenye jamii aliyopo, anaanza kuiga tabia mpya na za ajabu, mwishowe anaharibu maisha yake.
Hapo ndipo ninapojiuliza, hatuwezi kujifunza bila kupitia matokeo magumu? Kwa mfano, mtu anaweza kuugua au kukutana na changamoto fulani, ndipo tunapoanza kusikia ushauri kila kona ya mtandao: "Jamani, jitahidini kufanya 1, 2, 3, mnaona kilichotokea sehemu fulani."
Leo nimeona mada kuhusu trolls, wale wanaobully wenzao mitandaoni ikapelekea binti wa south kujiua ndioo ikageuka mjadala ili iwe funzo lakini nina uhakika hii sio mara ya kwanza, hii changamoto iko moka kwa wenzetu lakini kidogo wao wanabebana baadhi ya matatizo ya kujitakia yanapungua kwa asilimia fulani, ukilinganisha na hali yetu sisi! Tumeathirika na malezi ya utotoni au?
Ni kama taharuki iliyotokea wiki jana kuhusu wale mabinti waliomaliza shule. Ghafla kila mtu anatoa ushauri kuhusu malezi. Utadhani ni jambo geni kufanya malezi ili watoto wawe na tabia njema bila kusubiri matokeo mabaya ndio tujifunze?
Je, ni lazima tujifunze kwa njia ngumu kila wakati?
Sisi..😢Sisi ni wanafiki braza, ndio naweza sema ni hulka yetu.
Sisi sio wakweli,
Sisi sio wawajibikaji kwa makosa yetu,
Sisi sio watu tunaokubali makosa,
Sisi sio watu ambao tupo tayari kujishusha,
Sisi ni watu ambao tunapenda kuonekana tupo njema kila sekta,
Sisi sio wapenda kujifunza kulingana na makosa,
Sisi sio watu wa kujifunza kutoka kwa waliotuzidi au tuliowazidi.
Sisi ni watu wa excuses
Sisi..........
Sisi.....
Sisi.....
Being observant ni inate...Hivi being observant ni learned behavior au mtu anazaliwa hivyo?
Like kila kitu kishatokea kwanini watu wasiangalie wajifunze.
Professor wangu wangu mmoja alikuwa anatuambia kwenye social life ukisoma literature, Bible na saikoloji utakuwa mtu bora sana, Sina hakika na alichosema ila somehow namuelewa.
Yaah wengi tupo humo Robert Heriel Mtibeli huwa anasisitiza mambo ya kujenga familia huwa tunadharau ila ukweli kuna tatizo linaanzia huku.Sisi..😢
Babu sijaelewa hapa tafadhali!