We Africans, do we always have to learn it the hard way?

Mara nyingi, mtu anazaliwa na tabia fulani ambazo ni asili yake. Lakini anavyozidi kukua, anaanza kubadilika taratibu kulingana na mazingira, watu wanaomzunguka, au matokeo ya mambo anayokutana nayo.

Ni kwanini maisha ya baadae yanatubadilisha wengi? Mtu anazaliwa mwenye upendo na huruma ila mahusiano na ndoa au watu wabaya wanamkomaza anakuwa na roho ngumu hata kuua anaweza!

Kwa mfano, mtu anaweza asiwe mtu wa mazoezi kabisa. Lakini kwa sababu anataka kuvutia kundi fulani la watu, anaamua kuanza kufanya mazoezi ili kujenga mwili au kuonekana mwenye lifestyle fulani.

Kwanini watu wanashindwa kuwa na hobbies zao wenyewe? Kwa nini mpaka waige maisha ili waonekane wanapenda kusoma, kusikiliza muziki, au kuangalia michezo?

Matokeo yake, unakuta binti au kijana anapofikia kiwango fulani, ili kufit kwenye jamii aliyopo, anaanza kuiga tabia mpya na za ajabu, mwishowe anaharibu maisha yake.

Hapo ndipo ninapojiuliza, hatuwezi kujifunza bila kupitia matokeo magumu? Kwa mfano, mtu anaweza kuugua au kukutana na changamoto fulani, ndipo tunapoanza kusikia ushauri kila kona ya mtandao: "Jamani, jitahidini kufanya 1, 2, 3, mnaona kilichotokea sehemu fulani."

Leo nimeona mada kuhusu trolls, wale wanaobully wenzao mitandaoni ikapelekea binti wa south kujiua ndioo ikageuka mjadala ili iwe funzo lakini nina uhakika hii sio mara ya kwanza, hii changamoto iko moka kwa wenzetu lakini kidogo wao wanabebana baadhi ya matatizo ya kujitakia yanapungua kwa asilimia fulani, ukilinganisha na hali yetu sisi! Tumeathirika na malezi ya utotoni au?

Ni kama taharuki iliyotokea wiki jana kuhusu wale mabinti waliomaliza shule. Ghafla kila mtu anatoa ushauri kuhusu malezi. Utadhani ni jambo geni kufanya malezi ili watoto wawe na tabia njema bila kusubiri matokeo mabaya ndio tujifunze?

Je, ni lazima tujifunze kwa njia ngumu kila wakati?
Uzi makini sana , ukiwa na akili kama loose Nut lazima ukose cha kuchangia humu .

Heading uandishi wake 🔥 na kingereza kimenyooka na ime match perfectly na content .

Nikipata muda nipitie maoni yote Kisha niweke ya kwangu Inshallah
 
Kuna sister mmoja akimdate mtu ni wa kishua sana so mwanaume akigombana nae basi kesi inaenda kwa mzee jamaa anaitwa ana semwa weee na baba mkwe basi imekua hivyo jamaa imebidi azoee tu hana namna watoto wakushua hao,ila ndiyo maana kuna muhimu wakati wa kuoa chunguza mwenza wako amekua na makuzi gani ili ujue unaenda kuishi na mtu wa aina gani
Hahha na wakati wengine ukipeleka kesi unageuziwa mwenyewe kibao duhh huyo jamaa yako ataishi muda mfupi sana!
 
Silika
Ni hali ya asili, tabia, au haiba ambayo kiumbe (mnyama au binadamu) anayozaliwa nayo au hisia za ndani zinazomwongoza bila kufikiri kwa kina.

Nimegugo maana ya silika.
Ooh nilijua typo asante babu kwa fafanuzi!

Naona uko sahihi zaidi kwa maelezo yako ya mwanzo!
 
Uzi makini sana , ukiwa na akili kama loose Nut lazima ukose cha kuchangia humu .

Heading uandishi wake 🔥 na kingereza kimenyooka na ime match perfectly na content .

Nikipata muda nipitie maoni yote Kisha niweke ya kwangu Inshallah
Aww karibu sana adriz🥰
 
Na hatuna mpango wa kubadilika kizazi na kizazi wnajifunza mambo yaleyale kutoka kwa waliowatangulia!🤦🏽‍♀️
Fikiria hichi unachokiongelea leo ni kitu ambacho Aristotle, Kant, na Socrates walikipigania enzi zao kutaka watu waishi kwa uhalisia wao. Sasa fikiria imepita miaka mingapi tangu hao watu wayapiganie haya, na kwanini tumeendelea kupuuza ilihari matokeo tunayaona?

Aristotle alionya sana juu ya mifumo ya elimu ambayo inamfanya mtu kuwa mbobevu intellectually, lakini akafeli kwenye ethics and emotional intelligence.

Aristotle aliamini elimu ambayo haimjengi mtu katika misingi ya maadili na uthabiti wa kihisia hiyo sio elimu.

Namnukuu "Education without ethics is no education at all. Teaching the mind without teaching the heart is meaningless"

Leo watu wana elimu na vyeti vizuri, lakini hawana misingi mizuri ya uadilifu na uthabiti wa kihisia. Ukikosea kwenye haya mambo mawili unakosea kwenye kila kitu.

Ndio maana utaona watu wana mpaka PhD ila wanafanya mambo ya hovyo, wansheria wanapindisha sheria, daktari bingwa anajinyonga kisa msongo wa mawazo, mtu ana elimu yake nzuri ila gadhabu na hasira, hofu na wasiwasi, woga nk vimeathiri uelekeo wa maisha yake
 
Sijajua nielezeje: Naona kama sisi wa rahisi kuiga mambo mabaya kuliko mazuri 😅

Je mambo mazuri ni magumu na mabaya ni rahisi? I doubt!

Mambo mazuri ni rahisi kuyatenda kuliko mabaya/magumu.

Kinachotukumba waafrika na kuonekana kama ni jamii ya kishenzi ni kukosekana kwa ustaarabu na kistaarabika.

Sisi mazingira yetu hayatukuzi na kutulea kistaarabu. Ustaarabu ni kiwango kikubwa cha jamii kwenye Adabu, Nidhamu, Usafi, Utu (kuona binadamu wenzio kama binadamu) na usafi. Kinyume na ustaarabu ni ushenzi,ujeuri na vurumai.

Ukifika Norway utakubali kwamba wenzetu ni wastaarabu kwa asili na kimazingira na ni jadi yao.

Nakupa kisa; Nikiwa Norway sehemu inaitwa Telemark, mwenyeji wetu (Mtanzania), jirani yake (Mzungu), ni mkulima wa apples, anazilima ndani hapo hapo (backyard), mbele ya nyumba yake (getini pembeni) amepanga meza yenye apples za rangi tofauti vimifuko vya transparent, kila kimfuko kina apples kama tano au sita hivi za rangi tofauti; nyekundu, kijani au njano. Kila siku amekuwa akipanga vimifuko vile vingi vingi.
Baada ya kama siku tatu, nikagundua kila tukitoka nje matembezini au kwenye mgahawani au kufanya manunuzi, mwenyeji wangu alikuwa anachukua kimfuko kimoja kila siku pale asubuhi au jioni. 😊
Ukabidi, siku moja nimuulize, zile apples pale zinauzwa au namna gani? Akanijibu jirani yake (Mzungu mwanamke), analima apples, kwa hiyo kila siku anaweka apples zile ili kila mhitaji achukue. Nikamwambia mbona wewe sasa unachukua kimfuko kimoja, kwanini usichukue viwili au vitatu. 😁
Akacheka sana, akanambia ukichukua vingi kupita mahitaji unakuwa hujawajali wenzio, hujastaarabika na mbinafsi na hizo ni tabia za kibongo/kiafrika. Alikuwa ananieleza kama utani, lakini mimi nilikuwa nawaza hivi, ingekuwa bongo zile apples zingekuwa zinachukua hata dakika 10!! Si mhuni mmoja angekuwa anapita nazo zote chap tuu. 😁

Nikagundua kumbe nipo Ulaya, na nipo Norway. Sehemu ambayo ustaarabu na generosity ni jadi watu wanazaliwa wanakua nayo.
 
Sio lazima ku glorify struggle, mtu unaweza kuamua kujifunza hata kwa wengine, Sio lazima kila kitu kikutokee wewe.
Unachosema ni kweli tunaweza kujifunza kupitia uzoefu wa watu wengine. Na hapo tunaona uzito wa hoja ya muleta mada.

Some pains/experiences cannot be well understood until you experience them.

Wanadamu tuna tatizo moja KUPUUZA,, kwa maana ya kwamba tunaweza kuona wenzetu wanateseka kwa matokeo ya makosa yaliyofanyika kutokana na njia au maamuzi yao na bado tukakaza fuvu. Mpaka upitie ndo akili inakukaa sawa KUMBE HALI INAKUWAGA HIVI!

Ni watu wenye hekima pekee wanajifunza kupitia watu wengine.
 
Mambo mazuri ni rahisi kuyatenda kuliko mabaya/magumu.

Kinachotukumba waafrika na kuonekana kama ni jamii ya kishenzi ni kukosekana kwa ustaarabu na kistaarabika.

Sisi mazingira yetu hayatukuzi na kutulea kistaarabu. Ustaarabu ni kiwango kikubwa cha jamii kwenye Adabu, Nidhamu, Usafi, Utu (kuona binadamu wenzio kama binadamu) na usafi. Kinyume na ustaarabu ni ushenzi,ujeuri na vurumai.

Dah
Ukifika Norway utakubali kwamba wenzetu ni wastaarabu kwa asili na kimazingira na ni jadi yao.

Nakupa kisa; Nikiwa Norway sehemu inaitwa Telemark, mwenyeji wetu (Mtanzania), jirani yake (Mzungu), ni mkulima wa apples, anazilima ndani hapo hapo (backyard), mbele ya nyumba yake (getini pembeni) amepanga meza yenye apples za rangi tofauti vimifuko vya transparent, kila kimfuko kina apples kama tano au sita hivi za rangi tofauti; nyekundu, kijani au njano. Kila siku amekuwa akipanga vimifuko vile vingi vingi.
Baada ya kama siku tatu, nikagundua kila tukitoka nje matembezini au kwenye mgahawani au kufanya manunuzi, mwenyeji wangu alikuwa anachukua kimfuko kimoja kila siku pale asubuhi au jioni. 😊
Ukabidi, siku moja nimuulize, zile apples pale zinauzwa au namna gani? Akanijibu jirani yake (Mzungu mwanamke), analima apples, kwa hiyo kila siku anaweka apples zile ili kila mhitaji achukue. Nikamwambia mbona wewe sasa unachukua kimfuko kimoja, kwanini usichukue viwili au vitatu. 😁
Akacheka sana, akanambia ukichukua vingi kupita mahitaji unakuwa hujawajali wenzio, hujastaarabika na mbinafsi na hizo ni tabia za kiafrika.

Nikawaza; Ingekuwa bongo kwanza apples angekuwa anachukua mtu mmoja anatembea nazo zote kila asubuhi. 😁
Anachukua zote zingine anaenda kuuza kama za kwake kabisa 😅
 
Unachosema ni kweli tunaweza kujifunza kupitia uzoefu wa watu wengine. Na hapo tunaona uzito wa hoja ya muleta mada.

Some pains/experiences cannot be well understood until you experience them.

Wanadamu tuna tatizo moja KUPUUZA,, kwa maana ya kwamba tunaweza kuona wenzetu wanateseka kwa matokeo ya makosa yaliyofanyika kutokana na njia au maamuzi yao na bado tukakaza fuvu. Mpaka upitie ndo akili inakukaa sawa KUMBE HALI INAKUWAGA HIVI!

Ni watu wenye hekima pekee wanajifunza kupitia watu wengine.
Sahihi sana, Huu uzi wa Bi mrembo Seran ni mzuri sana umenipa kutafakari na kuwakumbuka baadhi ya walimu wangu.
 
Fikiria hichi unachokiongelea leo ni kitu ambacho Aristotle, Kant, na Socrates walikipigania enzi zao kutaka watu waishi kwa uhalisia wao. Sasa fikiria imepita miaka mingapi tangu hao watu wayapiganie haya, na kwanini tumeendelea kupuuza ilihari matokeo tunayaona?

Aristotle alionya sana juu ya mifumo ya elimu ambayo inamfanya mtu kuwa mbobevu intellectually, lakini akafeli kwenye ethics and emotional intelligence.

Kuna argument huko mtandao mwingine mtu alisema the highest form of intelligence is emotional intelligence, bado natafakari.
Aristotle aliamini elimu ambayo haimjengi mtu katika misingi ya maadili na uthabiti wa kihisia hiyo sio elimu.

Namnukuu "Education without ethics is no education at all. Teaching the mind without teaching the heart is meaningless"
🔥

Hawa wana falsafa wa mwanzo wangekuwepo sasa wangesema nini kuhusu capitalism?
 
Fikiria hichi unachokiongelea leo ni kitu ambacho Aristotle, Kant, na Socrates walikipigania enzi zao kutaka watu waishi kwa uhalisia wao. Sasa fikiria imepita miaka mingapi tangu hao watu wayapiganie haya, na kwanini tumeendelea kupuuza ilihari matokeo tunayaona?

Aristotle alionya sana juu ya mifumo ya elimu ambayo inamfanya mtu kuwa mbobevu intellectually, lakini akafeli kwenye ethics and emotional intelligence.

Aristotle aliamini elimu ambayo haimjengi mtu katika misingi ya maadili na uthabiti wa kihisia hiyo sio elimu.

Namnukuu "Education without ethics is no education at all. Teaching the mind without teaching the heart is meaningless"

Leo watu wana elimu na vyeti vizuri, lakini hawana misingi mizuri ya uadilifu na uthabiti wa kihisia. Ukikosea kwenye haya mambo mawili unakosea kwenye kila kitu.

Ndio maana utaona watu wana mpaka PhD ila wanafanya mambo ya hovyo, wansheria wanapindisha sheria, daktari bingwa anajinyonga kisa msongo wa mawazo, mtu ana elimu yake nzuri ila gadhabu na hasira, hofu na wasiwasi, woga nk vimeathiri uelekeo wa maisha yake
Umeandika nilichotaka kusikia sikuona namna ya kukiweka!Umegusia hoja muhimu kwamba elimu inapaswa kuunganisha maarifa na maadili pamoja na uthabiti wa kihisia. Aristotle alisisitiza juu ya umuhimu wa elimu inayojenga akili na moyo, akionya kwamba bila maadili, elimu inaweza kuwa hatari.

Changamoto ya sasa ni kwamba watu wengi wenye elimu nzuri wanakosa maadili na udhibiti wa hisia, jambo linaloathiri maisha na kazi zao. Tunahitaji mabadiliko katika mfumo wa elimu ili kuunganisha mafunzo ya maadili na ustawi wa kihisia ili kujenga jamii yenye wasomi wenye maadili mema na uwezo wa kudhibiti hisia.

Asante sana kwa maoni yako mkuu!
 
Sijajua nielezeje: Naona kama sisi wa rahisi kuiga mambo mabaya kuliko mazuri 😅

Je mambo mazuri ni magumu na mabaya ni rahisi? I doubt!
Hapo ndo nilishindwa kuelewa akili ya mwanadamu.

Mwanadamu anachukia uongo na anapenda ukweli katika hali ya kawaida, ila ukija kwenye maisha yetu tunachukia kuambizana ukweli/uhalisia na kukubali kujifariji kwa upotoshi.

Kila mtu atakwambia sipendi watu waongo, ila ukimweleza ukweli munakuwa maadui.

People would rather choose the easy wrong path than chosing the right harder path
 
Back
Top Bottom