Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,275
- 104,193
Mara nyingi, mtu anazaliwa na tabia fulani ambazo ni asili yake. Lakini anavyozidi kukua, anaanza kubadilika taratibu kulingana na mazingira, watu wanaomzunguka, au matokeo ya mambo anayokutana nayo.
Ni kwanini maisha ya baadae yanatubadilisha wengi? Mtu anazaliwa mwenye upendo na huruma ila mahusiano na ndoa au watu wabaya wanamkomaza anakuwa na roho ngumu hata kuua anaweza!.
Kwanini watu wanashindwa kuwa na hobbies zao wenyewe? Kwa nini mpaka waige maisha ili waonekane wanapenda kusoma, kusikiliza muziki, au kuangalia michezo?
Matokeo yake, unakuta binti au kijana anapofikia kiwango fulani, ili kufit kwenye jamii aliyopo, anaanza kuiga tabia mpya na za ajabu, mwishowe anaharibu maisha yake.
Hapo ndipo ninapojiuliza, hatuwezi kujifunza bila kupitia matokeo magumu? Kwa mfano, mtu anaweza kuugua au kukutana na changamoto fulani, ndipo tunapoanza kusikia ushauri kila kona ya mtandao: "Jamani, jitahidini kufanya 1, 2, 3, mnaona kilichotokea sehemu fulani."
Leo nimeona mada kuhusu trolls, wale wanaobully wenzao mitandaoni ikapelekea binti wa south kujiua ndioo ikageuka mjadala ili iwe funzo lakini nina uhakika hii sio mara ya kwanza, hii changamoto iko mpaka kwa wenzetu lakini kidogo wao wanabebana baadhi ya matatizo ya kujitakia yanapungua kwa asilimia fulani, ukilinganisha na hali yetu sisi! Tumeathirika na malezi ya utotoni au?
Ni kama taharuki iliyotokea wiki jana kuhusu wale mabinti waliomaliza shule. Ghafla kila mtu anatoa ushauri kuhusu malezi. Utadhani ni jambo geni kufanya malezi ili watoto wawe na tabia njema bila kusubiri matokeo mabaya ndio tujifunze?
Je, ni lazima tujifunze kwa njia ngumu kila wakati?