Wazungu wana chuki mno na Lamine Yamal. Ni kutokana na rangi yake tu

Wazungu wana chuki mno na Lamine Yamal. Ni kutokana na rangi yake tu

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
15,774
Reaction score
35,994
Zimekuwepo tabia za wazungu kuwabagaza wachezaji wenye asili ya Africa kutokana na wivu walionao tu na ubaguzi wa rangi

Nakubali Lamine Yamal ni kijana mdogo japo ni star, Kwa umri wake laZima bwana mdogo afanye makosa mengi ila kama watu wazima ilitakiwa kumsimamia na kumsaidia vizuri

Nilishangaa Jana baba mzima Dani Carvajaal kumshambulia bwana mdogo miaka 17 tu, yaani kama mtoto wake wa kumzaa

Kumbuka Carvajaal na Lamine Yamal wanacheza timu Moja ya taifa, naamini haikuwa poa

Hii sio mara kwanza Kwa wachezaji wenye asili ya Africa walivopitia magumu wakiwa Spain na Europe

Mfano
Neymar, aliandamwa sana hadi akapotea kila alichofanya kilioneka a kibaya

Vini Jr anatafutiwa skendo

Baloteli, huyu jamaa wazungu walimwandama

Etoo alizomea na kubaguliwa mno

Manson Greenwood, huyu dogo alikuwa na talent kubwa, akaandamwa na kupewa kesi za kijanga za ngono ambayo imerudisha nyuma kipaji chake

Bwana mdogo Yamal anapitia magumu
Screenshot_20251027-090538.png
Screenshot_20251027-090341.png
 
Shida yote ilianzia kwa Vini boya yule. Inaonyesha aliipania sana mechi ndo maana hakupenda alivyotolewa. Wakati wameamuliwa yeye akawa anamfata tena Yamal wapigane hadi raphinha kaingilia kati wazichape...Carvajal nae boya kweli Team mate wake Spain anataka kupigana nae ahead of World Cup kick off.

NB. Yamal apunguze mambo mengi nje ya uwanja
 
Mkuu emu tulia utuelezee vizuri jana umesema Kilian Mbappe kakosa penati ya wazi kabisa yeye na kipa kachomesha?
 
Waafrika tuache kulia lia..
Hapo uneongelea mengi.

1. Neymar hakupotezwa, alijipoteza mwenyewe, starehe za kupitiliza, majeraha ya mara kwa mara, ngumu kudumu kwenye ubora...
Gaucho, de lima mbona waliheshimika!?

2. Ugomvi kwa wachezaji wa timu moja, haswa barca na madrid sio kesi kabisa, ramos aliwahi kumsukuma usoni puyol, na puyol ni mtu anaeheshimika kabisa.

3. Lamine kama ni kujipoteza qtajipoteza mwenyewe... akifata tabia za ki neymar neymar.

4. Mtu kama vinicius jr., kwa tabia zake zile unadhani nani anampenda, wakati mwingine mpaka mashabiki wa madrid huwa wanakereka na mambo yake.

Kipaji pekee hakitoshi kukufanya uwe bora, bali ni nidhamu,juhudi na kujitunza.. mfano katika hili ni cr7
 
Huyu dogo mnamtetea kwa ujinga waku lakini apunguze kamdomo, yeye sio kwamba anabaguliwa kwa rangi yake hapana ni maisha na maneno yake ya kutokua na heshima nje ya uwanja ndo vinafanya watu waendelee kumchukia siku hadi siku, kuna wachezaji wengi tu weusi ambao wanautwanga fresh tu na hawabaguliwi mfano Raphinha lakini kwanini wabaguliwe yeye na vini? Aache kamdomo acheze mpira umri wake bado mdogo sana
 
Waafrika tuache kulia lia..
Hapo uneongelea mengi.

1. Neymar hakupotezwa, alijipoteza mwenyewe, starehe za kupitiliza, majeraha ya mara kwa mara, ngumu kudumu kwenye ubora...
Gaucho, de lima mbona waliheshimika!?

2. Ugomvi kwa wachezaji wa timu moja, haswa barca na madrid sio kesi kabisa, ramos aliwahi kumsukuma usoni puyol, na puyol ni mtu anaeheshimika kabisa.

3. Lamine kama ni kujipoteza qtajipoteza mwenyewe... akifata tabia za ki neymar neymar.

4. Mtu kama vinicius jr., kwa tabia zake zile unadhani nani anampenda, wakati mwingine mpaka mashabiki wa madrid huwa wanakereka na mambo yake.

Kipaji pekee hakitoshi kukufanya uwe bora, bali ni nidhamu,juhudi na kujitunza.. mfano katika hili ni cr7
Lamine Yamal Bado ni teenager
Amezaliwa 2007
Kwa umri wake laZima awe anafanya makosa ya ujana
Hivi unadhani hao kina Mesi, Ronaldo, Rooney, Lampard hawakuwa na vituko vyao, mbona hawakuandamwa

Nambie Lamine Yamal amefanya kosa Gani
Amebaka?
Amekunywa pombe?
Ameendesha gari Kwa fujo?
Amepigana?
Yani bwana mdogo atie bleach kichwani na avae zake mlegezo liwe suala la kuwaudhi watu wazima
 
Lakini Wana tabia za usela hasa Vini.
 
Vipi kuonekana mshangazi!?

Ila lakini ustar alionao yeye si cr7 wala messi alikuwa hivi wakiwa na miaka 17.

Lamine miaka 17 anategemewa na team.. messi at 17 anakuwa, sio tegemezi kuna gaucho, cr7 nae hakuwq tegemezi rasmi.. hawakuwa mastar wa team,
Hivyo lamine ajue yeye ni star camera hazitakaa mbali nae, wala midomoni mwa watu
 
Lakini Wana tabia za usela hasa Vini.
Wewe usela wa hao vijana unakuumiza Nini?
Yaani kijana anaishi maisha yake lakini anazingatia ratiba ya mazoezi na match anatwanga fresh Sasa Mimi litanikera nini hilo jambo
 
Wewe usela wa hao vijana unakuumiza Nini?
Yaani kijana anaishi maisha yake lakini anazingatia ratiba ya mazoezi na match anatwanga fresh Sasa Mimi litanikera nini hilo jambo
Hebu fikiria Jana kocha kamtoa ona reaction ya Vini! Utapendwa vipi? Yeye ni nani asitolewe?
 
Hebu fikiria Jana kocha kamtoa ona reaction ya Vini! Utapendwa vipi? Yeye ni nani asitolewe?
Hiyo ni temper ya mchezo
Ukiwa mchezoni unaweza Fanya matukio mabaya na ukaja kukuta baadae,
Vini sio wa kwanza kufanya vile
Akitulia atamwomba msamaha coach Xabi Alonso na maisha yanaendelea
 
Sio kweli kwamba Lamine anabaguliwa kwasababu ya rangi yake. Msitafute kichaka.

Carvajal alikuwa anamuonya dogo apunguze mdomo kwasababu interview ya juzi dogo alionesha dharau na nni kitu ambacho kiliwaudhi wengi.
 
Mentality kama hizi zinafanya watu weusi tuonekane dhaifu sana.

Kitu kidogo tu "because he's black."

Wewe ni shabiki wa Yanga na bila shaka umeona mashabiki walichomfanyia yule mchezaji Uchizi Vunga. Vipi naye ni kwasababu ya rangi yake?

Kwanini usiangalie haya mambo katika angle ya kimpira?
 
Back
Top Bottom