Biashara kweli haina changamoto cha msingi ni kutafuta namna ya kuweza kupunguza changamoto hizo.Hakuna biashara inayokosa changamoto, serikali yenyewe inakusanya kodi tu kwa wafanyabiashara lkn changamoto zipo. Wewe kama umeona kuna fursa hiyo piga kazi, usisikilize mawazo ya watu walioshindwa, watu tunaishi, tumejenga tunasomesha kwa pikipiki. Ila nivema ziwe za mikataba ya mwaka 1 na jitaidi uziongeze zifikie 10 na kuendelea utaona mambo yanaenda
Muhimu kuweka GPs na kukatatia bima kubwa afu gharama hizo unaongeza mwezi mmoja mbele
Kiukweli Bodaboda sio biashara ya kudumu na kuitegemea kwa miaka yote bali unaweza kuifanya Kama daraja wakati unafikiria vitu vingine vya kufanya.
Kwa mfano biashara ya bodaboda huwa naipenda inapotokea nimepata hela za ghafla na sijajipanga kibiashara akilini mwangu huwa nawahi kununua bodaboda ili nipate pesa za kujikimu na kuulinda mtaji wangu.
Kwa mfano Kama nimepata milioni 10 Sasa hivi nitanunua bodaboda 2 fasta kwa mil 4 ili nipate hela za kula na milioni 6 zinatulia benki wakati huo natafuta biashara nyingine ya kufanya.
Safi kabisa umemalizaMkuu mimi nafanya kazi ya Bajaj toka nimalize chuo kikuu mwaka 2016, mpaka sasa mafanikio ni makubwa sana. Kama ilivo kawaida changamoto ni nyingi mno lakini jitahidi uzikabili wala usikate tamaa! Bajaj nunua TVS King+ ni nzuri sana...zingatia Service kila week, mwaga oil kama ilivoelekezwa! hiyo ni ajira ya kudumu na wala hutatamani tena zile zingine kutoka Tamisemi. Mwisho kabisa itakuwa vyema ukiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mana wataila kabla hata haijarudisha pesa
Kila biashara ina changamoto zake lkn kabla fanya Research hasara haikosekani na faida haikosekani muhimu upate madereva wazuri na ukiweza usitoe mkataba ukitoa mkataba kila kitu juu yake haitengenezi anaua injini mwisho wa siku anaua chombo na mkatab hamalizi mm nakwambia ivo nilipita apa apa sasa ivi nna pikipiki zaidi ya 10 na bajaj kadhaa nna uzoefu mzuri tu.Umeongea ukweli kaka.
kama hatakuamini afanye kama ana bet tu itampunguzia stress!Kama huendeshi wewe bora hizo hela uzitunze
Kama huendeshi wewe bora hizo hela uzitunze
mpk leo sijui pikipiki iko wapi nimemuachia munguYaani hizi biashara ujitoe ufahamu aisee ila return yake inataka moyo sana,
kumbe bora mm jmn pole lknJambo si kutishana ila tunaelezea uhalisia wake.. Biashara hii inalipa endapo ukipata kijana mzuri na mwenye kujali chombo
Mimi mwenyewe niliingiza 7m ila kilichotokea sina hamu
dahUmenena vyema kabisa. Laki 8 faida kutoka 2.2mil ni kama 3% tu kwa mwezi. Heri hata ukaange mihogo stand aisee.
Ila unasahau kuwa service na matengezo mengine ni juu yako .....ukute Huna knowledge yeyote ..huko gereji utapigwa hela mpakaLakini kumbuka hiyo staili ya mkataba sio lazima.
Ni wamiliki wa pikipiki ndio walibuni hvyo baada ya kuona madereva ni wasumbufu kuleta hesabu.
Kwa hyo ukiona staili ya mkataba huipendi unaweza kutumia ile staili nyingine ya bila mkataba ambayo unapokea 7000 kwa siku bila kikomo yaani pikipiki inabaki kuwa yako miaka yote.
Nimecheka sana aisee,hapo kwenye serviceLengo la biashara ya bodaboda libaki tu kuwa ni kuwainua vijana wanaoendesha sio faida kwa BOSS, kwa style ya mkataba unapata kama 1M faida kwa mwaka (say 10k kila siku) baada ya hapo boda sio yako tena.... bila mkataba utapokea kama elfu 7 kila siku bila kikomo ila service ni juu yako na utajuta kwa maana dereva ni kama atataka kukukomoa.