Biashara ya gereji na changamoto zake

SuperEnthusiasis

New Member
Feb 4, 2023
3
3
Habarini wakuu,

Natumai mnaendelea vizuri pia poleni na majukumu.

Mimi ni kijana wa miaka 22 na pia ni mwanafunzi wa chuo nikisoma kozi ya Mechanical engineering ngazi ya degree na pia naingia mwaka wa tatu katika mwaka ujao wa masomo unaoanza mwezi novemba.

Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiwaza kuwa naweza kujiajiri katika jambo gani baada ya kumaliza chuo na majibu ambayo nimeyapata kwa asilimia kubwa ni kufungua gereji.

Kwa hesabu nilizonazo ni kuwa naweza kuwa na kiasi cha shilingi milioni tano baada ya miaka miwili kulingana na jinsi nilivyowekeza vipesa vyangu vya boom katika sehemu fulani, na kwamba hapo sasa ndio nitakuwa namaliza chuo na kuingia mtaani.

Ombi langu kwa wanaJF wenye ujuzi kuhusu kazi ya gereji ni majibu ya maswali haya machache,


1. Je, mtaji wa 5M unatosha kuanzia kufungua ofisi?

2. Changamoto katika kazi hii ziko vipi?

3. Location nzuri ni katikati ya mji ama hata pembeni kidogo ya mji?, mji ninaoulenga ni Dar es salaam.

Ni hayo tu wanaJF na naomba majibu kwa faida yangu na faida ya vijana wengine wengi watakaosoma uzi huu.

MUNGU AWABARIKI!

Asanteni.
 
Mafundi hawafugiki. Ukitaka kuweza wapike vijana wako tu. Ucje ukachukua fundi sehemu.pika vijana wako tu. Narudia tena pika vijana wako tu.
Asante
 
Back
Top Bottom