Wazoefu wa biashara ya boda boda na bajaji, njoo mtujuze changamoto mnazokumbana nazo

Hakuna biashara inayokosa changamoto, serikali yenyewe inakusanya kodi tu kwa wafanyabiashara lkn changamoto zipo. Wewe kama umeona kuna fursa hiyo piga kazi, usisikilize mawazo ya watu walioshindwa, watu tunaishi, tumejenga tunasomesha kwa pikipiki. Ila nivema ziwe za mikataba ya mwaka 1 na jitaidi uziongeze zifikie 10 na kuendelea utaona mambo yanaenda
 
Hakuna biashara inayokosa changamoto, serikali yenyewe inakusanya kodi tu kwa wafanyabiashara lkn changamoto zipo. Wewe kama umeona kuna fursa hiyo piga kazi, usisikilize mawazo ya watu walioshindwa, watu tunaishi, tumejenga tunasomesha kwa pikipiki. Ila nivema ziwe za mikataba ya mwaka 1 na jitaidi uziongeze zifikie 10 na kuendelea utaona mambo yanaenda
Biashara kweli haina changamoto cha msingi ni kutafuta namna ya kuweza kupunguza changamoto hizo.

Naamini nitafanikiwa kupunguza kwa asilimia kadhaa na sio zote
 
Umeongea ukweli kaka.
Kiukweli Bodaboda sio biashara ya kudumu na kuitegemea kwa miaka yote bali unaweza kuifanya Kama daraja wakati unafikiria vitu vingine vya kufanya.
Kwa mfano biashara ya bodaboda huwa naipenda inapotokea nimepata hela za ghafla na sijajipanga kibiashara akilini mwangu huwa nawahi kununua bodaboda ili nipate pesa za kujikimu na kuulinda mtaji wangu.
Kwa mfano Kama nimepata milioni 10 Sasa hivi nitanunua bodaboda 2 fasta kwa mil 4 ili nipate hela za kula na milioni 6 zinatulia benki wakati huo natafuta biashara nyingine ya kufanya.
 
Mkuu mimi nafanya kazi ya Bajaj toka nimalize chuo kikuu mwaka 2016, mpaka sasa mafanikio ni makubwa sana. Kama ilivo kawaida changamoto ni nyingi mno lakini jitahidi uzikabili wala usikate tamaa! Bajaj nunua TVS King+ ni nzuri sana...zingatia Service kila week, mwaga oil kama ilivoelekezwa! hiyo ni ajira ya kudumu na wala hutatamani tena zile zingine kutoka Tamisemi. Mwisho kabisa itakuwa vyema ukiendesha mwenyewe na sio kumpa mtu mana wataila kabla hata haijarudisha pesa
Safi kabisa umemaliza
 
Umeongea ukweli kaka.
Kila biashara ina changamoto zake lkn kabla fanya Research hasara haikosekani na faida haikosekani muhimu upate madereva wazuri na ukiweza usitoe mkataba ukitoa mkataba kila kitu juu yake haitengenezi anaua injini mwisho wa siku anaua chombo na mkatab hamalizi mm nakwambia ivo nilipita apa apa sasa ivi nna pikipiki zaidi ya 10 na bajaj kadhaa nna uzoefu mzuri tu.
 
Wakuu naomba mnijuze bei ya Boxer (pkpk) kwa Dar mana Mbeya wanauza 2,550,000 tena hiyo nibei yahizi Boxer zakawaida nasio zile Boxer Dume zile bei yake imepaa zaid
 
Lakini kumbuka hiyo staili ya mkataba sio lazima.
Ni wamiliki wa pikipiki ndio walibuni hvyo baada ya kuona madereva ni wasumbufu kuleta hesabu.
Kwa hyo ukiona staili ya mkataba huipendi unaweza kutumia ile staili nyingine ya bila mkataba ambayo unapokea 7000 kwa siku bila kikomo yaani pikipiki inabaki kuwa yako miaka yote.
Ila unasahau kuwa service na matengezo mengine ni juu yako .....ukute Huna knowledge yeyote ..huko gereji utapigwa hela mpaka
 
Lengo la biashara ya bodaboda libaki tu kuwa ni kuwainua vijana wanaoendesha sio faida kwa BOSS, kwa style ya mkataba unapata kama 1M faida kwa mwaka (say 10k kila siku) baada ya hapo boda sio yako tena.... bila mkataba utapokea kama elfu 7 kila siku bila kikomo ila service ni juu yako na utajuta kwa maana dereva ni kama atataka kukukomoa.
Nimecheka sana aisee,hapo kwenye service
 
Back
Top Bottom