mbu wa dengue
JF-Expert Member
- Jun 2, 2014
- 7,658
- 9,761
Hii comment ndio imemaliza maelekezo yote.Biashara ya boda boda ni nzuri Sana, ila inachangamoto zake km zilivyo biashara zingine tu. Chamoto kubwa kabisa ni uaminifu kwa hao vijana wanao tufanyia kazi. Ili kukabiliana na changamoto hizo yafuatayo uyazingatie.
1. Anza pikipiki mpya but zile za Bei nafuu
2. Fanya utafiti wa tabia za hao vijana unaotaka kuwapatia.
3. Zingatia umri wa hao vijana above 18 age na ikwezekana awe ameoa.
3. Malipo yawe kwa kila wiki
4. Fanya kwa mkataba(miezi 11)
5. Kila siku akuletee 10000 chukua malipo kwa wiki
6. Funga GPS kwenye hizo boda hiyo itakurahisishia kuzifuatilia popote utakapokuwepo.
7. Hakikisha pikipiki umeikatia vibali vyote mhimu km vile bima, Sumatra n.k
8. Hakikisha kijana unaemkabidhi hicho chombo lazima awe na leseni ya drive. pia km anafamilia yake karibu ni vyema kuishirikisha familia yake na ikiwezekana wamzamini.
Nafikiri kwa kuanzia hayo yanatosha mengine, utapa izoefu huko mbele ya Safari
Hata Mimi mwaka huu mkataba wangu wa kazi uliisha nikanunua pikipiki 2 mwezi wa kwanza nikawapa vijana wastaarabu ninaowafaham nashukur mungu hawanisumbui kabisa.
Na hizo pikipiki ndio zinanisaidia kunipa hela za kulisha familia.
Ingekuwa Nina pesa nyingi ningenunua hata 10 niwe na uhakika wa hela za kuendesha familia halaf baada ya hapo ndio ningewaza biashara nyingine.
Uzur wa hii biashara naipenda kwa sababu hainiharibii muda wangu na pia hakuna haja ya kumlipa mshahara dereva bali anajilipa mwenyewe.