The mountain lion
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 1,153
- 418
Haijapoteza lengo la kujifaragua ni mjuvi wa lugha hii adhimu,ilhali u debe tupu.
Ahsante.Naona umemwaga Kiswahili cha mwambao wa Pwani kabisa,wenyewe tunasema umeongea kuntu.
Haijapoteza lengo la kujifaragua ni mjuvi wa lugha hii adhimu,ilhali u debe tupu.
Ahsante.Naona umemwaga Kiswahili cha mwambao wa Pwani kabisa,wenyewe tunasema umeongea kuntu.
Ndio tabu ya kusikiliza Clouds kisha ku-paste hapa nzima nzima, uwe unachuja au ku-edit basi!!
La Princesa toa maelezo ya ziada.
100% hii Habari umeitoa kwenye kipindi cha Radio cha TAKE-ONE cha juzi!!una uhakika kuwa nimecopy na kupaste?Me cyo fan wa Clouds at all,me ni mdau tu....hali yenyewe inajionesha
Wasanii wetu bado wana tatizo,Wao wanalalamika sana kuwa kushuka kwa bei kutawathiri,me najiuliza wataathirika vipi wakati wao huwa wanauza master then mdosi anawalipa wanamalizana kabisaa....
2) Ambae hajapenda wazo la step anaweza kudeal na distributor mwingine ambae Bei zake zitakuwa tofauti na Steps
Nnachoamini ni kuwa steps hawamlazimishi mtu kufanya nao kazi,ukiridhia,fine,usiporidhia fine...so Sioni tatizo wao kushusha bei,nadhani ni business strategies tu
Mdau kiswahili secondary nilifaulu sana kuliko hata masomo mengine.Haijapoteza lengo la kujifaragua ni mjuvi wa lugha hii adhimu,ilhali u debe tupu.
mdau kiswahili secondary nilifaulu sana kuliko hata masomo mengine.
Dah........ mdau umenikomalia.:A S-eek::A S-eek:...na si kigezo cha kujiona unafahamu kila kitu katika lugha ya kiswahili..
Dah........ mdau umenikomalia.:A S-eek::A S-eek:
Ufaulu sio unajiona unafahamu kila kitu ila unafahamu vingi.
Mwishoni mwa mwaka huu kumetokea mambo kadhaa yaliyoleta msisimko mkubwa katika soko la filamu za kitanzania....
Issue iko hivi,Steps Entertainment ambaye anaaminika kuwa ndiye distributor mkubwa wa filamu za kitanzania yeye binafsi ameamua kushusha bei ya filamu anazozisambaza yeye kutoka shilingi 2500 mpaka 1000
Binafsi namsupport sana kwa wazo hilo kwa sababu zifuatazo
1) Itapunguza wizi wa filamu,watu wengi walikuwa hawana uwezo wa kununua filam kwa bei ya 2500so Atleast 1000,wengi watamudu
2) Ushindani kwa distributors wengine utaongezeka
3) Itakuwa changamoto kwa wasanii wa filamu kuweza kufikiri nje ya boksi ili kuhakikisha kuwa wanafaidika na kazi zao
So binafsi nimeona ni wazo zuri sana....mwenzangu unaonaje?
NAWASILISHA
Hahaaaaa,hata wakigawa bure sizitaki.
Mimi wateja wa Bongo movie bado sijaelewa huwa wanavutiwa na nini kwenye hizo movie.
Hahahaha:A S wink::A S wink:Yes.I dont want to learn to quit..it will become a habit
Siioni pointi yoyote juu ya sula la kupigania bei.
Hivi watanzania woote tunadhani kuwa tatizo la filamu zetu ni bei ? sidhani kama tatizo ni bei, nadhani tatizo ni kushuka kwa thamani ya filamu zetu...kwa sasa majumbani na vibandani zinazotamba ni series za kikorea, kifilipino na filamu za kihindi zinazotafsiriwa kwa kiswahili.
Kwa muda mrefu wadau mbali mbali wamekuwa wakitahadharisha juu ya mfumo unaotumika kuendesha hii tasnia bila mafanikio...ni dhahiri kuwa hao Steps wanatapatapa kwa matokeo waliyoyaasisi wenyewe, na kukimbilia kushusha bei wakidhani ndio suluhisho.
Steps amefanikiwa kuwageuza baadhi ya wasanii mafisadi, ambao wamekuwa hawajali wengine zaidi ya kuneemesha matumbo yao...mfumo wa kutengeneza filamu pati one na two, msanii kushurutishwa kutengeneza filamu nzima ndani ya mwezi mmoja, msambazaji kuingia mkataba na msanii moja kwa moja na kupelekea msanii kuignore zile hatua zote muhimu za kuandaa filamu, kwa nini ahangaike ili hali uwepo wake tu kwenye filamu ni kigezo tosha kwa kazi yake kusambazwa ?
Kwa kuwa tasnia nzima imekosa sauti moja na kugawanywa kama mbuzi, sishangai kuona wanakimbilia suala la bei kama suluhisho la kuanguka kwa soko la filamu.
Mimi wateja wa Bongo movie bado sijaelewa huwa wanavutiwa na nini kwenye hizo movie.
Inagharimu kiasi gani kutengeneza Movie nzuri kabisa? wasanii mahili, locations barabara, sound quality safi, lightening safi, wide coverage marketing n.k