Wazo la Steps nalinunua

Wazo la Steps nalinunua

La Princesa

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
1,056
Reaction score
1,189
Mwishoni mwa mwaka huu kumetokea mambo kadhaa yaliyoleta msisimko mkubwa katika soko la filamu za kitanzania....

Issue iko hivi,Steps Entertainment ambaye anaaminika kuwa ndiye distributor mkubwa wa filamu za kitanzania yeye binafsi ameamua kushusha bei ya filamu anazozisambaza yeye kutoka shilingi 2500 mpaka 1000

Binafsi namsupport sana kwa wazo hilo kwa sababu zifuatazo

1) Itapunguza wizi wa filamu,watu wengi walikuwa hawana uwezo wa kununua filam kwa bei ya 2500so Atleast 1000,wengi watamudu

2) Ushindani kwa distributors wengine utaongezeka

3) Itakuwa changamoto kwa wasanii wa filamu kuweza kufikiri nje ya boksi ili kuhakikisha kuwa wanafaidika na kazi zao

So binafsi nimeona ni wazo zuri sana....mwenzangu unaonaje?

NAWASILISHA
 
sijakuelewa ''unalinunua'' wazo au unamsupport???
 
naona sababu ulizotoa ndo zile zile walizotoa hao steps kuhusu wasanii kufikiria nje ya boksi ni ongezeko la makahaba wa bongo muvi na wasanii wenye majina makubwa ambao hawana chochote walichoacha
 
Hata wakiuza 250 kwangu mimi ni sawa tu maana hawanipunguzii wala kuongeza chochote.
 
Mabongo muvi lazima washike adabu mwaka huu.
 
Collection za wanaojua kuigiza zinauzwa buku 2, halafu hawa wanaojifunza kuigiza eti muvi moja wanauza 2500.Afadhali Steps wameliona hili na kushusha bei vinginevyo tulikuwa tunaibiwa kwani quality ya hizi bongo muvi hata wangeshusha mpaka 500 ni poa tu.
 
Sawa ewe mswahili uliyeshindwa kuandika sentensi nzima kwa Kiswahili.
Mimi kiswahili ndio nyumbani hapo nimekuwekea alama za '' '' kuonesha utofauti.
 
Mwishoni mwa mwaka huu kumetokea mambo kadhaa yaliyoleta msisimko mkubwa katika soko la filamu za kitanzania....

Issue iko hivi,Steps Entertainment ambaye anaaminika kuwa ndiye distributor mkubwa wa filamu za kitanzania yeye binafsi ameamua kushusha bei ya filamu anazozisambaza yeye kutoka shilingi 2500 mpaka 1000

Binafsi namsupport sana kwa wazo hilo kwa sababu zifuatazo

1) Itapunguza wizi wa filamu,watu wengi walikuwa hawana uwezo wa kununua filam kwa bei ya 2500so Atleast 1000,wengi watamudu

2) Ushindani kwa distributors wengine utaongezeka

3) Itakuwa changamoto kwa wasanii wa filamu kuweza kufikiri nje ya boksi ili kuhakikisha kuwa wanafaidika na kazi zao

So binafsi nimeona ni wazo zuri sana....mwenzangu unaonaje?

NAWASILISHA

Ndio tabu ya kusikiliza Clouds kisha ku-paste hapa nzima nzima, uwe unachuja au ku-edit basi!!
 
Mimi kiswahili ndio nyumbani hapo nimekuwekea alama za '' '' kuonesha utofauti.

Haijapoteza lengo la kujifaragua ni mjuvi wa lugha hii adhimu,ilhali u debe tupu.
 
Back
Top Bottom