Wazo la Project ya Kusaidia Watoto wa Shule Mabegi

stephenga

Senior Member
Joined
Sep 15, 2022
Posts
139
Reaction score
309
Nina wazo la kuanzisha project ndogo ya kusaidia watoto wa shule za msingi wanaotoka mazingira magumu kupata begi la shule lenye vifaa muhimu vya kujifunzia ndani yake—kama madaftari, vitabu, kalamu, mkebe n.k.

Kwa sasa nataka kuanza kama initiative yangu binafsi, mimi na washikaji wachache. Sina mpango wa kuanza na NGO au kampuni; nataka kutumia WhatsApp kuwaalika marafiki wanaoweza kusaidia, tuanze kidogo na kuona itakavyokwenda.

Kusema kweli, nafanya hivi kama passion tu ya kusaidia watoto, kwa sababu ni kitu ninachopenda kufanya. Lakini who knows, inaweza kukua na kufika mbali zaidi.

Ninachojiuliza ni:

Je, ni sawa kuanza kama individual bila usajili, halafu baadaye project ikikua au donor akihitaji organization rasmi ndiyo nisajili?

Pia, kama nataka kushirikiana na shule, Serikali za Mitaa/Mtaa au Halmashauri ili kuwafikia watoto wanaohitaji msaada, je, mtu binafsi anaweza kupata ushirikiano kama huo? Mfano kupata taarifa/utambulisho wa wanafunzi wanaohitaji msaada, bila kuwa NGO iliyosajiliwa?

Kwa watu ambao mmewahi kuanzisha projects za kijamii hapa Tanzania, mnanishaurije?

Nataka tu kuanza. Sitaki kusubiri mpaka niwe na organization kubwa ndipo nianze kusaidia. 🙏
 
Good idea. Nitashiriki kikamilifu
 
Back
Top Bottom