nimependa hiyo"wanaokupenda wanazidi kukukataa"
Najivunia kuwa Mtanzania
Mtu mmoja alifariki na kwenda kuzimu. Akiwa huko aligundua kwamba kuna kuzimu tofauti kwa nchi tofauti na akaamua kuchagua mojawapo yenye maumivu kidogo kwa ajili kufaidi ufalme wa kuzimu. Akaenda kuzimu ya Ujerumani na kuuliza hapa wanafanya je?
Akajibiwa "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kijerumani na kukucharaza bakora kutwa nzima.Hakukubaliana na hali hiyo akaondoka.
Akaenda kuzimu ya Marekani,Urusi na nyingine nyingi.Akagundua kwamba zote zinafanana na kuzimu ya Ujerumani. Baada ya hapo akaenda kuzimu ya Tanzania, huko alikuta kuna misururu mirefu ya watu wanaosubiri kuingia ndani,akashangaa,akauliza wanafanya nini humo?.
Akajibiwa, "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kitanzania na kukucharaza bakora kutwa nzima. " Akauliza,Lakini hii inafanana kweli na kuzimu za nchi nyingine mbona kuna misururu mirefu ya watu namna hii?
"Akajibiwa ,kwa sababu hakuna umeme hivyo kiti cha umeme hakifanyi kazi na misumali iliyonunuliwa haijaletwa, kwa hiyo kitanda ni kizuri kulalia.Na shetani wa kitanzania ni mtumishi wa umma,ambaye anakuja asubuhi,anasaini kwenye kitabu cha mahudhurio kazini na kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zake binafsi.
Ni Yule anayewaibia Watanzania hela kwa ufisadi na kugoma kujiuzulu, kwa kulindwa na wakubwa na kuwaacha watanzania walio wengi wakikosa huduma muhimu za Jamii na huku walioko madarakani wanateteana kwenye
madeal kibao ya kupiga fedha za walalahoi na wezi wadogo wanaoiba chakula kwa sababu ya njaa ya chakula cha siku na mazao waliyolima na wazazi wao hayana soko na yaliyonunuliwa wakulima wamekopwa na bado wanaibiwa kura zao wanapofanya maamuzi ya kubadilisha viongozi wasiofaa na wezi wa mali ya umma.Pia viongozi wanaopuuza maamuzi ya wananchi ya kubadili katiba wanayoitaka na kuweka matakwa yao ili kujilinda wao na mafisadi wenzao
.Eee mungu tusaidie tuepuke kikombe hiki
Siku njema!!