Wazo la kudai Katiba Mpya lilikuwa ni la Dkt. Sengodo Mvungi. Inabidi apatikane mtu mwingine mwenye nia ya dhati kuongoza mapambano, si Mbowe

Tuanze na wewe hapa

1) Tueleze kwny Katiba ya sasa ni jambo gani haliwezi kuboreshwa kwa kuingiza mambo mapya kwa njia ya ammendments hadi tulazimike kuwa na katiba mpya?

2) Kazi ya Bunge la Katiba kwny rasimu ya Warioba ni ipi?

3) Msimamo wa wenu ni upi mchakato kuanza upya au kuendelea ulipoishia kwny rasimu au kwny kura ya maoni?
Nimependa hilo swali namba 2!
 
Wenye kuhitaji Katiba Mpya ni wachache sana sema tu wana kelele nyingi sana kwny mitandao

Ukizima data halafu ukapita pita mitaani na kwny Vijiwe huwezi kusikia hizo kelele za Katiba mpya...
Mkuu, hivi unataka watu waandamane au wafanye nini ndiyo ujue kuwa wanahitaji katiba mpya. Kigezo cha kujua hitaji la Watanzania ni nini hasa? Maana hata kwenye maji, Umeme na madarasa hatujawahi kusikia watanzania wote wakilalamika.

Na hiyo haitakuja tokea kama unategemea hilo. Hata kwenye nchi zilizowahi kuwa na Mapinduzi siyo wananchi wote wanahusika..... That's how the world is!!

Huko nyuma ziliundwa Tume kuangalia mahitaji ya Wananchi na tume zote ziliwahoji wananchi na mwisho wa siku zilipendekeza katiba mpya. Hizo ni Tume za Jaji Nyalali aliteteuliwa na Mwinyi na Tume ya Jaji Kisanga aliyeteuliwa na Mkapa.

Tume ya Warioba ilipoundwa ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba wanayoitaka, Kama Watanzania hawataki katiba mpya hayo maoni Warioba na tume yake wameyatoa wapi?

Swala la katiba mpya ni common sense tu. Watanzania tangu wapate uhuru hawajawahi kutengeneza katiba yao. Katiba inayotumika iliyotengenezwa na wachache bado in sheria nyingi za mkoloni. Ndiyo maana wakati wa JPM tuliona jinsi gani Mkuu wa Wilaya alivyo na mamlaka ... anaweza kukuweka ndani kwa masaa 48 bila hata kosa.

Anyway, tuassume kuwa hayo unayoyasema ni kweli kuwa Watanzania hawataki katiba mpya. Je ni nani ambaye kamwambia Maza kuwa Watanzania wanataka Tume huru ya Uchaguzi. Hayo mapungufu unayohoji na unafikiri yanawza kuboreshwa pia siyo watanzania wote wanayaona.

Kumbe na utafiti umeonyesha hiyo TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya
 
Wenye kuhitaji Katiba Mpya ni wachache sana sema tu wana kelele nyingi sana kwny mitandao

Ukizima data halafu ukapita pita mitaani na kwny Vijiwe huwezi kusikia hizo kelele za Katiba mpya...
Swala la nchi kua na katiba bora wala haliitaji sana kelele au maneno mengi maana mwenendo wa nchi unajieleza.Sasa inashangaza wewe unataka kila mwananchi azungumze katiba mpya uko mtaani kitu ambacho hakimake sense.

Jambo lolote lile lazima liwe na wawakilishi wachache wanaowakilisha mahitaji ya wengi ilimradi hilo jambo liwe na manufaa.Ata wakati wa wakina Nyerere wanafanya jitihada za kupata uhuru usifikiri ni wananchi wote nchi nzima walikua wanaongelea kupata uhuru uko mitaani.

Kinachokosekana sasa hivi ni uzalendo ndo maana hatuwazi mustakabali wa nchi zaidi yakufikiria matumbo yetu ndo maana hii hoja ya katiba mpya watu wanajificha kwenye kichaka cha wananchi.
 
Lini Mbowe amesema kuwa amejipa uongozi wa hayo mapambano dhidi ya katiba mpya?

Mfano wewe johnthebaptist ukiwa ubanda pale mitaa yako ya Ipogoro unakunywa ulanzi na wenzako na ikatokea ukaanza kuainisha umuhimu wa katiba mpya, inamaana utakuwa umefanya hiyo kwa nia ya kujipachika nafasi ya uongozi juu mapambano ya kudai katiba mpya?
Bwashee natoa tu angalizo kwamba tukimwachia Mbowe hatutafika popote!
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete alisema ni Dr Sengodo Mvungi ndiye aliyemshawishi hadi akaanzisha mchakato wa Katiba mpya kwa kuunda Tume ya Warioba.

Kikwete alisema Dr Mvungi alikuwa anapiga kambi hotelini kule Bagamoyo akifanya michakato ya namna ya kuipata katiba mpya itakayowainua Watanzania.

Naye, mzee Warioba alisema Dr Mvungi alikuwa ndio Injini ya Tume ya Katiba kwani alijitoa kwa 100% kuifanya kazi hiyo.

Sasa, tujiulize Mbowe au Zitto Kabwe wana uthubutu huo wa kuachilia fursa zote ili kuongoza Mapambano ya kudai Katiba mpya?

Maendeleo hayana vyama!
Ni ujinga wa hali ya juu kusema hayo na ni dharau kwa Watanzania pia. Watanzania walipendekeza wawe na katiba mpya kwenye Tume za Nyalali na Kisanga ... well before ya Dr. Mvungi na Kikwete wake kama ni kweli.

Kama wewe hutaki katiba mpya talk for yourself. Lakini usiwasemee Watanzania wote. Yaani Kikwete akubali kufanya maamuzi kama hayo kwa sababu ya mtu moja. Seriusly...!? Dr. Mvungi hakuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho .... Tusidanganyane.
 
Ni ujinga wa hali ya juu kusema hayo na ni dharau kwa Watanzania pia. Watanzania walipendekeza wawe na katiba mpya kwenye Tume za Nyalali na Kisanga ... well before ya Dr. Mvungi na Kikwete wake kama ni kweli.

Kama wewe hutaki katiba mpya talk for yourself. Lakini usiwasemee Watanzania wote. Yaani Kikwete akubali kufanya maamuzi kama hayo kwa sababu ya mtu moja. Seriusly...!? Dr. Mvungi hakuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho .... Tusidanganyane.
Mbona alivyokufa na katiba yenyewe imekufa?!!

Utasubiri sana.
 
Mbona alivyokufa na katiba yenyewe imekufa?!!

Utasubiri sana.
You must be kidding me ..... sasa akina Mbowe wanadai nini kama imekufa!!?

Mkuu, mimi sina cha kusubiri lakini nitaendelea kusupport madai ya katiba mpya. Kama kusubiri tulisha subiri sana ... lanini kama nyie mnaona siyo issue na Watanzania hawataki, kwa nini mnapoteza muda kuja na thread au kuwajibu wanaotaka kaiba mpya. Mwambieni Maza akae kimya tu badala ya kuhangaika kujibu na kuunda za uliji za kina Mkandala....!!
 
Back
Top Bottom