Wazo la kudai Katiba Mpya lilikuwa ni la Dkt. Sengodo Mvungi. Inabidi apatikane mtu mwingine mwenye nia ya dhati kuongoza mapambano, si Mbowe

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete alisema ni Dr Sengodo Mvungi ndiye aliyemshawishi hadi akaanzisha mchakato wa Katiba mpya kwa kuunda Tume ya Warioba.

Kikwete alisema Dr Mvungi alikuwa anapiga kambi hotelini kule Bagamoyo akifanya michakato ya namna ya kuipata katiba mpya itakayowainua Watanzania.

Naye, mzee Warioba alisema Dr Mvungi alikuwa ndio Injini ya Tume ya Katiba kwani alijitoa kwa 100% kuifanya kazi hiyo.

Sasa, tujiulize Mbowe au Zitto Kabwe wana uthubutu huo wa kuachilia fursa zote ili kuongoza Mapambano ya kudai Katiba mpya?

Maendeleo hayana vyama!
 
Weka chanzo cha taarifa ndugu

Hearsay hazisaidii

Hata hivyo katiba si ya mtu ni mustakabali wa wananchi wote ikiwemo mimi na wwe
 
Yule unayetamani awepo jela Hana dhamira ya dhati au ndio unajaribu kumvunja moyo.
 
Niliwahi hoji hili hapa ya kuwa katiba mpya muasisi wake alikuwa nani?

Na kwanini idaiwe na chadema? Matokeo yake mod walinifutia ule uzii,
 
Labda katika kufanya siasa zao za ufatilia umeshindwa kuelewa aina ya siasa za Kikwete.

Hata ungekuwa wewe Kikwete angekubali. Lakini mfumo ungekumeza, namba ya wajinga Tanzania ni kubwa maana humu ndani tu kuna watu ukiwauliza KATIBA hii kuna shida watasema hakuna. Au unaweza kukutana na swali kama hili humu " Katiba inakuletea ugali nyumbani "

Tunajua hupendi mbinu zinazotumika kueleza umuhimu wa KATIBA MPYA sawa hutukatazi lakini hujawai kuiongelea KATIBA MPYA huo ni unafiki.

Tukutane miaka ya mbele. Awamu ya Tano ulikuwa mtori ngoja nyama zipo chini.

Sent from my SM-G928I using JamiiForums mobile app
 
Mi n
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete alisema ni Dr Sengodo Mvungi ndiye aliyemshawishi hadi akaanzisha mchakato wa Katiba mpya kwa kuunda Tume ya Warioba...

Mi nafikiri wewe ndo unafaa kama Mvungi na uanzie magereza kama Mbowe
 
Wenye kuhitaji Katiba Mpya ni wachache sana sema tu wana kelele nyingi sana kwny mitandao

Ukizima data halafu ukapita pita mitaani na kwny Vijiwe huwezi kusikia hizo kelele za Katiba mpya

Watetezi wa Katiba mpya wengi wao hawaijui katiba ya sasa na hata ukiwauliza mapungufu ya Katiba ya sasa wengi hawawezi kueleza kwa ufasaha.

Mapungufu gani makubwa ambayo yapo kwny Katiba ya sasa ambayo hayawezi kuboreshwa kuakisi hayo matazamio ya wengi au ndio tuimbe tu katiba mpya hata kama watabadili Cover la katiba ya 1977 na kuiweka mpya tutajiona washindi

Strategy ya kudai katiba mpya ni chovu sana na inasubiri ama huruma ya watawala au mbinyo wa mabeberu sio shinikizo la ndani ya nchi
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete alisema ni Dr Sengodo Mvungi ndiye aliyemshawishi hadi akaanzisha mchakato wa Katiba mpya kwa kuunda Tume ya Warioba...
Kwa hiyo Mbowe asiwepo kabisa kwenye madai ya katiba mpya kwa sababu yalianzishwa na Mvungi?

Sababu za kumtoa Mbowe ni nini hasa?
 
Wenye kuhitaji Katiba Mpya ni wachache sana sema tu wana kelele nyingi sana kwny mitandao

Ukizima data halafu ukapita pita mitaani na kwny Vijiwe huwezi kusikia hizo kelele za Katiba mpya...
Sasa,hivi kweli unataka uzime data na upitapo mitaani usikie madai ya katiba kwa sauti kuu...katibaaa...katiiiibaaa...katibaaaa tunatakaaaa!? Ingekuwa mambo yanaenda hivyo hata kuhusu mfumuko wa bei ingekuwa hivyo.

Hata kama ni "wachache" kama unavyodai,kwa nini wasisikilizwe?
 
Huenda hujaelewa

Straregy ya wadai katiba mpya ni mbovu na haiwezi kuishinikiza Serikali kwa kuwa wameshindwa kuuza mitaani Agenda ya Katiba mpya

Ntakupa mf.mmoja wakati wa utawala wa Jakaya wadau walifanikiwa sana kuuza agenda ya ufisadi mitaani na ikazungumzika kweli kweli kwa kuwa ilipata watu sahihi na fasaha wa kuizungumza hiyo agenda

Kwa sasa hakuna mtu fasaha na sahihi wa kuuuza hoja ya katiba mpya mitaani…imebakia hoja ya wanaojiona wasomi pekee
Sasa,hivi kweli unataka uzime data na upitapo mitaani usikie madai ya katiba kwa sauti kuu...katibaaa...katiiiibaaa...katibaaaa tunatakaaaa!? Ingekuwa mambo yanaenda hivyo hata kuhusu mfumuko wa bei ingekuwa hivyo.Hata kama ni "wachache" kama unavyodai,kwa nini wasisikilizwe?
 
Huenda hujaelewa

Straregy ya wadai katiba mpya ni mbovu na haiwezi kuishinikiza Serikali kwa kuwa wameshindwa kuuza mitaani Agenda ya Katiba mpya..
Huyo mtu sahihi wa kuuza agenda kwa wananchi anapatikanaje?Maana walivyoanza tu wakakamatwa na "kupewa" kesi ya ugaidi wahangaike nayo.

Vilevile shughuli za mikutano ya vyama(Usipokuwa CCM)vimekatazwa na wahusika kusumbuliwa kila watakapo kufikisha agenda kwa wananchi.

Ulitaka hizo kelele au majadiliano uyapataje kwa wananchi ambao bado wanahitaji ufafanuzi na hamasa?

Tofauti kabisa na wakati wa agenda ya ufisadi ambapo vyama vilipata fursa ya kuilezea katika mikoa yote bara na pwani.
 
Tuanze na wewe hapa

1) Tueleze kwny Katiba ya sasa ni jambo gani haliwezi kuboreshwa kwa kuingiza mambo mapya kwa njia ya ammendments hadi tulazimike kuwa na katiba mpya?

2) Kazi ya Bunge la Katiba kwny rasimu ya Warioba ni ipi?

3) Msimamo wa wenu ni upi mchakato kuanza upya au kuendelea ulipoishia kwny rasimu au kwny kura ya maoni?

Huyo mtu sahihi wa kuuza agenda kwa wananchi anapatikanaje?Maana walivyoanza tu wakakamatwa na "kupewa" kesi ya ugaidi wahangaike nayo.Vilevile shughuli za mikutano ya vyama(Usipokuwa CCM)vimekatazwa na wahusika kusumbuliwa kila watakapo kufikisha agenda kwa wananchi.Ulitaka hizo kelele au majadiliano uyapataje kwa wananchi ambao bado wanahitaji ufafanuzi na hamasa?Tofauti kabisa na wakati wa agenda ya ufisadi ambapo vyama vilipata fursa ya kuilezea katika mikoa yote bara na pwani.
 
Rais wa awamu ya 4 mzee Kikwete alisema ni Dr Sengodo Mvungi ndiye aliyemshawishi hadi akaanzisha mchakato wa Katiba mpya kwa kuunda Tume ya Warioba...!
Hivi niulize.. Kwann serikali ya chama tawala ikisikia neno katiba mpya yaan wanapagawa mazima hawatak hata kusikia?

Kuna kibaya gan Kweny mpya?

Ambayo itatupa dira nzur ya muelekeo wa Taifa na kiutawala!!
 
Back
Top Bottom