Ushauri- Raisi Samia usiogope tangaza kura ya maoni tupate katiba mpya, kisha uchaguzi wa 2025 ukishinda utaleta mapinduzi ya kiuchumi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,936
20,373
Miezi nane ijayo Raisi Samia atakuwa madarakani kwa mwaka wa pili tangu amrithi hayati John Magufuli na hadi sasa atakuwa amejifunza mengi na sasa unaonyesha kusimama ingawa bado, kuna figisu za hapa na pale. Kuongoza nchi ni kazi ngumu ambayo pia yahitaji maamuzi magumu pale unopoona pahitaji mabadiliko.

Raisi Samia amefanya mabadiliko katika vyombo vya ulinzi na usalama tumepata mkuu mpya wa majeshi, IGP mpya na DCI mpya pia. Hiyo ni kawaida kwa viongozi kuchagua wale watu ambao watawasikiliza na kuwaelewa wataka nini, ndiyo mamlaka yampa raisi uwezo huo.

Raisi Samia ana bahati moja kwamba amerithi uzuri yale yote mazuri ambayo mtangulizi wake alikuwa akiyatekeleza hususan ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere na reli mpya ya SGR.

Bwawa la Mwalimu Nyerere litatoa umeme wa uhakika, ambao utaruhusu viwanda mbalimbali vodogo na vikubwa kujengwa na pia umeme huo utakuwa nafuu kuliko sasa. Reli ya SGR italeta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuhamisha na kusambaza shughuli za kiuchumi nchini kwa maana ya kurahisisha usafirishaji wa bidhaa, abiria , utengenezaji wa ajira mpya katika vituo vya reli hiyo na vitongoji vyake na pia kuhamasisha maendeleo ya makazi mapya ambayo yatatokana na kuwepo kwa reli hiyo.

Hakuna nchi duniani ambayo imepata maendeleo kwa kubebana na kupendeleana au kuchekeana, zote hizo zimepitia hatua ngumu na mapinduzi makubwa katika kila sekta.

Nchi yetu ni jidubwana lilolala usingizi wa pono (sleeping giant) ambalo lasubiri tu kuamushwa na nguvu za wengi na wengi hao ni wananchi wakulima na wafanyakazi. NI katika kipindi hichi cha sintofahamu iliopo duniani na vita ya Ukraine ndipo viongozi wa nchi kama ya kwetu twahitaji kutumia fursa hiyo kufanya kitu chaitwa "great reset".

Yaani ni kitendo cha kutafakari ni kuangali nchi yaenda wapi kiuchumi, kuangalia nchi zinokuzunguka, kila njia ikuingiziayo mapato, miradi ya kimakakati na mwelekeo wa baadae kufikia ile azimio na dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025. Tukumbuke tuna miaka mitatu tu imebakia kufikia dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025.

Nchi yetu bado ni maskini kinadharia lakini yenye utajiri mkubwa wa rasilimali kuanzia misitu hadi madini adimu duniani ya Tanzanite, twahitaji kufanya maamuzi magumu. Nchi yetu ina bandari, ina maziwa makuu Victoria, Nyasa na Tanganyika na pia nchi hii kistratejia ipo mahala pazuri kupaa kiuchumi pale tukiwa na miongozo imara itokanayo na raisi makini na katiba imara.

Kelele za katiba mpya zimekuwa nyingi mno hadi kufikia wakati zilikuwa zikimkera lakini ana nafasi, ya kuhakikisha tunazuia kelele hizo. Wapinzani wako wanadhani katiba mpya ndo suluhisho la wao kuweza kushinda uchaguzi na kushika Ikulu.

Wananchi wa Tunisia leo wanapiga kura ya maoni kuruhusu mabadiliko ya katiba ili kupata katiba sahihi kwa ajili ya Tunisia. Lakini huku nje twaambiwa kuwa raisi Kais Saied ataka kubakia madarakani na kupata nguvu zaidi katika kutoa maamuzi, kuagiza bunge litekeleze maamuzi mazito na pia kusimamia zaidi shughuli za mahakama.

Raisi Saied si mjinga, kwani yeye mwenyewe ni mwanasheria ambae amebobea kwenye sheria za katiba na mwaka 2014 aliketi na jopo la wataalam wa masuala ya katiba kutengeneza katiba mpya baada ya mapinduzi ya mwaka 2011.

Lakini sasa raisi Saied ataka kufanya marekebisho mengine lakini baada ya kutumia wiki nne tu kutengeneza rasimu ya katiba hiyo badala ya miaka miwili kama ilvyokuwa kwa katiba ilotungwa baada ya mchakato wa mwaka 2014.

Rasimu ya sasa ilitengenezwa mwezi Juni mwaka huu kamati ambayo aliiteua yeye na ambayo ilijumuisha pia wanasheria, kamati za maridhiano ya kitaifa, uchumi, jamii na kamati zingine za ushauri.

Utaratibu huu alofanya raisi Saied hautofautiani sana na utaratibu ambao Tanzania iliupitia wa kutengeneza rasimu ya katiba chini ya jaji mstaafu Joseph Sinde Warioba ambae baada ya kuja na mapendekezo rasimu ile ipo mahala imetulia.

Tofauti na utaraibu ulofanywa na Tanzania ambapo wasiasa wa upinzani akiwemo marehemu Dr Sengodo Mvungi, raisi wa Tunisia hakuweka mwanasiasa wa upinzani hata mmoja kutoka vyama vya upinzani nchini humo akiwemo mpinzani wake mkuu Ennahda ambe ni wa chama cha FCP na pia jumuiya ya wafanyakazi nchini humo ya UGTT haikuwemo na hivyo kukosa kuwakilisha maoni ya wafanyakazi.

Baadae mwishoni mwa Juni rasimu ilotengenezwa ilipotoka ilionekana ipo tofauti na mwenyekiti wa kamati bwana Belaid akatoa taarifa kuwa haitambui rasimu hiyo mpya isipokuwa ile ambayo alishiriki na kusimamia kuitengeneza.

Bwana Belaid akaenda mbali na kusema kuwa rasimu waliopeleka kwa raisi Saied si ile ambayo imetolewa na rasimu ya sasa (ambayo ndiyo yapigiwa kura ya maoni leo) ina kipengele ambacho champa madaraka "makubwa sana" raisi Saied.

Katika rasimu katiba inopigiwa leo ina mabadiliko ambayo kwanza ni kuondoa uchaguzi unoshirikisha wagombea mbalimbali wa kutoka vyama mbalimbali jambo ambalo lilifikwa baada ya mapinduzi na kuleta mfumo mmoja wa uchaguzi wa raisi (mfumo wa chama kimoja) na kisha kumpa raisi madaraka ya kumteua waziri mkuu na mawaziri na kisha kumpa madaraka raisi huyohuyo kulivunja bunge mara moja.

Pia raisi atakuwa na madaraka ya kuteua majaji na kisha katiba itazuia majaji hao kufanya mgomo wowote katika ile inoonekana kuziba mwanya huo ambapo majaji 57 walifukuzwa kazi na raisi Saied mwezi Juni na wenzao kugoma kwenda kazini.

Rasimu mpya inopigiwa kura ya maoni leo pia inaondoa kipengele cha kumuondoa raisi kwa sababu yoyote ile kupitia bunge jambo ambalo lilikuwemo katika katiba ya 2014.

Pia katiba mpya ilotengenezwa baada ya 2014 ilikataza kuwepo na mabadiliko ya ukomo wa raisi ili kuongeza muda wa raisi kuwepo madarakani na kipengele hicho bado kipo katika katiba mopya ya sasa inopigiwa kura leo.

Katiba hiyo mpya inipogiwa kura ya maoni leo yamo masuala kama kuruhusu dini ya kiislamu kuwa ndi msingi wa katiba hiyo tofauti ya ile ilopendekezwa, ambayo inasema suala la dini litakuwa ni uislamu ya jumuiya au Islamic Umaah na kwamba serikali itatekeleza baadhi tu ya vipengele vya sheria ya kiislamu katika masuala kama fedha, dini, uhuru na kulinda wananchi wake.

Tangu aingie madarakani raisi Saied amelivunja bunge, kumfukuza waziri mkuu, kuvunja bodi ya kupambana na rushwa na tume ya uchaguzi.

Akijitetea raisi Saied amesema amechukua hatua zote kwa kuzingatia sheria zote na ni hatua za lazima katika kuiokoa nchi kutoka katika hatari ya kiusalama inoinyemelea nchi hiyo.

Wananchi wengi khasa vijana ndo wanomuunga mkono raisi Saied na hata wale walomsaidia kufika hapo alipo akiwa ni mtu wa nje ya mfumo wa kifisadi (outsider) anaonekana amedhamiria kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kiutendaji nchini humo khasa kumaliza vitendo vya rushwa na madhila mengine yanoikabili nchi hiyo.

Mimi sipendekezi raisi Samia afuate yale yanofanywa na raisi Saied isipokuwa kuna yale ya kujifunza kuwa kama nchi ina yumba kiuchumi basi zipo sababu zinopelekea hali hiyo. Nchi yetu ina tatizo la mfumuko wa bei, maisha yamekuwa magumu na pia serikali imezidisha kodi kwa wananchi wa kipato cha chini huku wafanyabiashara wakifaidika na kupanda kwa bei.

Moja ya matatizo makubwa yanoikabili nchi leo ni mapato hafifu ya kodi na kukosekana kwa udhibiti wa mianya inosaidia ukwepaji wa kodi. Tatizo jingine ni kwa idara kama TAKUKURU kushindwa kufanya kazi yake ipasanyo na pia kukosekana kwa uwazi (transparency) kwa vyombo vya serikali na khasa idara ya twakwimu ya taifa ambayo utoaji wake wa taarifa za hali ya uchumi huridhishi.

Huu ni wakati muafaka kwa raisi Samia kuchukua maamuzi magumu ya kuipitia tena rasimu ya katiba ilowasilishgwa na jaji mstaafu Joseph Warioba, kuangalia kama kunahitajika marekebisho ya hapa na pale na kisha kuamua kuwepo na kura ya maoni kuwaomba wananchi wabarikie katika hiyo.

Raisi Samia anatambua kuwa njia pekee ya kurudisha juu uchumi ulokuwa na kutangazwa na Benki ya Dunia na IMF wakati wa serikali ya awamu ya tano kwamba Tanzania ilifikia "uchumi wa kati" ni kuwepo kwa katiba mpya.

Katiba mpya ikiridhiwa na wananchi itatoa fursa kwa taifa kurudisha ari ya kujituma kwa wanachi , kufanya kazxi, kuleta mapinduzi ya kilimo, mapinduzi ya teknolojia na viwanda ambayo yataongeza tija kwa taifa pamoja na pato la taifa.

Raisi Samia asingojee uchaguzi mkuu wa 2025 bali aweza kuwezesha kura ya maoni kwa sasa na kisha uchaguzi ukawepo bila shida yoyote ile.

Utakuwa raisi wa kwanza Tanzania kuweka historia ya kuwepo kwa kura ya maoni kuleta katiba mpya na kisha uchaguzi wa 2025 ushinde kihalali na mwisho Tanzania ibadilike iwe kama Dubai.

Utakumbukwa kwa hilo.
 
Back
Top Bottom