Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Inawezekana only POLISI wetu wakitanuliwa katika utendaji kazi wao..waajiri wachoraji wa kazi hizo,wa waandae askari wa upelelezi ki ukweli ukweli, Askari wa upelelezi ili tuone kazi yake inatakiwa Asijue chochote kuhusu TUKIO zaidi ya kujua tu mtu flani aliuliwa sehemu flani,kuanzia hapo yeye afanye upelelezi hadi agundue...Atumie elimu yake kumpata mhalifu.

Mbona wapelelezi ncu za wenzetu wakija nchini kutafuta kitu in a month wanatoa report ya hadi mhalifu katokea wapi na kaenda wapi?? kwanini askari wetu wasiweze? Kuna shida huko mavyuoni mwao wanapopaita UPELELEZINI..watu wasiojulikana kweli wapo ila watajulikana tu pale TEAM YA WAPELELEZI walioiva wakiingia kazini na si hawa askari wetu.
 
Acha siasa za kishamba, utawezaje kusimama na kukariri sura ya mtu mwenye AK 47 huku anatishia kuua au anafyatua risasi?
 
Mkuu! Kinadharia uko sahihi 100%. Tatizo ni pale mamlaka husika zinapokaa kimya wakati taarifa zinapotolewa. Watu wanajulikana ila neno la "wasiojulikana" awali lilikuwa linatumiwa kuwaficha wamaofanya matukio, ila sasa linatumiwa kama sitiari kwa vile jamii imechoshwa na mwenendo mzima unavyochukuliwa/unavyoshughulikwa.
 
Mzee Mwanakijiji lazima kwanza tujiulize hili neno wasiojulikana limeanzia wapi na wakati gani.

Mwananchi au raia hana mamlaka ya kufanya uchunguzi na kumtambua mhalifu au uhalifu na kutangaza hadharani, Mamlaka zenye dhamana kwa maana ya vyombo vya usalama ndio vyenye mamlaka ya kutokea ufafanuzi mambo yote ya kiusalama katika nchi yeyote ile. "Watu wasiojulikana" neno hili limetoka kwenye vinywa vya wenye dhamana kila linapotokea tukio la mtu kutekwa hivyo nasisi wananchi tumeendelea kuwaita watu hawa "wasiojulikana" maana wahusika mpaka sasa wanashindwa kutuambia ni nani muhusika wa matukio haya yanayoendelea zaidi ya wao kutuambia watu wasiojulikana wamefanya - - - - - -

Wasiojulikana wataendelea kuwa wasiojulikana mpaka pale Serikali yenye dhamana ya kulinda Raia wake itakapotoa ufafanuzi wa kina na wenye kuingia akilini utakaotuambia ni fulani na fulani ndio wahusika na wakafikishwa kwenye vyombo husika.
 
Ushauri wa watu kama CDM, CCM, CUF, ACT - Wazalendo n.k. kujipa mamlaka ya kuchora watu na kutuaminisha kuwa ni waarifu sikubaliani nao ila nisamehe bure kama nitakuwa sijakuelewa vizuri!

Amewataja cdm wala hajawataja ccm kwani ndio wahanga wakubwa wa watu wasiojulikana. Hata huyo mwanakijiji anazunguka tu kufurahisha genge, lakini ukweli hao watu wasiojulikana ni matokeo ya siasa za jiwe. Na siku anatoka madarakani kundi hilo halitakuwepo fullstop.
 
Siasa ambazo naziunga mkono 100% Ili watu waamke next time hao wajinga upinzani wajifunze maana haya yasingetokea kama tungekua na upinzani makini tangu mwanzo badala ya wachumia tumbo
 
Huo msamiati wa WASIOJULIKANA umeanzishwa na WANAOJULIKANA ili wajifiche chini ya huo mwamvuli kukwepa maovu yao ya dhulma na uonevu dhidi ya haki
 
Na. M. M. Mwanakijiji. Ni vizuri watu kama CDM au vyombo vingine kuanza kutumia "sketch artists" yaani wachoraji na kuanza kutengeneza picha za wahusika ili watu waanze kuwajua taratibu.[/b] Endapo picha za michoro za watu hao zikitengenezwa vizuri na kusambazwa watu wengine wataanza kutengeneza tahahadhari na hata kuweza kuwatambua kuwa ni kina nani.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Hapa nakubaliana na wewe, sio lazima tuwategemee polisi kwa kila kitu.
 
Hizo akili zilikuwepo enzi za CHADEMA ya akina Dr.
Hiki cha waandikisha magari ya chama kwa jina la Mwenyekiti, wako busy kuwaza 2020 watapataje tena dili la kuiuzia CCM kiti cha mgombea URAIS.
Yani mnaoona slaa alikuwa kichwa sana nawashangaa sana
Mtu makini hawezi kurudi kushirikiana na wanyang'anyi wa haki,yule alikuwa njaa tu ndio maana alidemand alipwe mshahara sawa na wa ubunge
 
Siasa ambazo naziunga mkono 100% Ili watu waamke next time hao wajinga upinzani wajifunze maana haya yasingetokea kama tungekua na upinzani makini tangu mwanzo badala ya wachumia tumbo

Anzisha chama chako chenye upinzani makini tuje tujiunge.
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽

Teh Mzee Mwanakijiji kweli hili wazo fyatu

"Watu wasiojulikana" haimaanishi kweli hawajulikani bali ni nickname ya wahusika wenyewe kwenye vyombo vyetu

Acha kujitoa ufahamu .
Mwanakijiji uneshachoka akili sikuhizi huna jipya na mada zako za Lumumba zinaegemea Kwenye kujipendekeza
Ikitokea Mtu asiejulikana akawa ameingia kupiga tukio huku amevaa Mask itawezekanaje kumchora (sketch)?

Wacha hili wazo lako libaki tu fyatu kama ulivoliita.
 
Anzisha chama chako chenye upinzani makini tuje tujiunge.
Mpinzani wa kweli na mwenye msimamo alikua Mtikila peke yake tatizo hakupata ushirikiano na wanamageuzi wenzake. Tundu Lissu kabla hajawa mbunge na kuambukizwa virusi vya wakongwe wa siasa yule Lissu mwanaharakati siyo Lissu wa leo Kinyonga. Lissu mtetezi wa wana blyankuru waliofukiwa na serikali badhirifu ya kina mwinyi na mkapa. Mzee James Mapalala muanzilishi na mtetezi wa vyama vingi Tanganyika.

Hawa tulio nao wanaonekana wanamageuzi kwa vijana waliozaliwa 1990 wakati wa vyama vingi ni vizuri kuwaonea huruma sababu hawajui kuwa wanaowashabikia ndiyo wavurugaji wa siasa za vyama vingi wakiwasaidia ccm
 
mzee mwanakijiji unadhani wasiojulikana ni kweli kwamba hawajulikani??

aliye mtishia bape bastora anasema hajulikani lakn je ni kweli hajulikani? anajulikana na kila mtu alifanywa nini??

waliopiga bastora tajiri wa mwanza naye akawarudishia na kuwaumiza je hawajulikani si wanajulikana? akaishia kufunguliwa kesi muathirika . kumbuka ni usalama ambao kisheria hawatuhusiwi kumkamata mtu lakn waliishia kurushiana risasi na kusema ni mhujumu uchumi baada ya kumshindwa kumteka?

sisi tunawajua ni watu wa kitengo endelea ww unaejifanya huwajui?

au hujasikia Nyarandu kakatwa na maafisa wa takukuru ni mi Ak47 huku hawaruhusiwi na hakuna anayekemea??

mzee mwanakijiji nakukumbusha ni vigumu sana kumtetea ibilisi hana fadhira muda wowote anakuumbua
 
Mpinzani wa kweli na mwenye msimamo alikua Mtikila peke yake tatizo hakupata ushirikiano na wanamageuzi wenzake. Tundu Lissu kabla hajawa mbunge na kuambukizwa virusi vya wakongwe wa siasa yule Lissu mwanaharakati siyo Lissu wa leo Kinyonga. Lissu mtetezi wa wana blyankuru waliofukiwa na serikali badhirifu ya kina mwinyi na mkapa. Mzee James Mapalala muanzilishi na mtetezi wa vyama vingi Tanganyika.

Hawa tulio nao wanaonekana wanamageuzi kwa vijana waliozaliwa 1990 wakati wa vyama vingi ni vizuri kuwaonea huruma sababu hawajui kuwa wanaowashabikia ndiyo wavurugaji wa siasa za vyama vingi wakiwasaidia ccm

Anzisha chama chako haya maoni yako yafanye kazi.
 
Back
Top Bottom