Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Na. M. M. Mwanakijiji

Sasa imekuwa ni kama kawaida tu. Kwamba, tunatumia maneno bila kujua hasa tunachomaanisha na hatujali sana madhara ya kutumia maneno hayo bila kumaanisha tunachotaka kumaanisha. Mfano mzuri ni haya maneno mawili ambayo sasa yameanza kukubaliwa kama kawaida - "Watu Wasiojulikana". Nina uhakika wanaotumia maneno haya wanataka kutuambia tu kuwa wahusika wanaozungumziwa ni watu ambao hakuna aliyewatambua au wao wenyewe hawakujitambulisha.

Nafahamu kuwa watu wanaposema "kujulikana" kimsingi wanataka kutuambia kumaanisha "kutambulika". Na kweli mara nyingi katika lugha ya Kiswahili tunaposema "kujulikana" tunataka kusema "kutambulika" au "kufahamika". Na kuna wakati bila ya shaka maneno hayo yanaweza kutumiwa kwa kubadilishana (interchangeable).

Hata hivyo, linapokuja suala hili la matukio ya watu kujikuta wanakamatwa na watu ambao baadaye ama wanakuja kutambulika kuwa ni maafisa fulani wa polisi basi neno "kujulikana" linakosa maana kidogo. Unapozungumzia "watu wasiojulikana" kuna maana kubwa sana. Kwa sababu kuna ngazi mbalimbali za "kumjua mtu" lakini hakuna mtu anayeweza kutokea mahali popote bila uwezekano wa "kujulikana" kabisa.

Mtu anapoingia nyumbani kwangu na mimi simtambui bado nina mambo kadhaa naweza kusema nayajua kuhusu mtu huyo. Kwa mfano naweza kusema "alikuwa ni mwanamme, mrefu, mwembaba kiasi na sauti yake yenye mikwaruzo". Katika ngazi hiyo kuna vitu basi "navijua" kuhusu mtu huyo hata kama "simtambui" ama kwa sura, jina au ajira yake.

Kwa wanaoangalia TV, filamu na hata utendaji wa polisi wa kawaida, mtu anaweza asijulikane lakini polisi wanaweza kumuita mchoraji wa picha za wahalifu na kwa kutumia maelezo ya mashahidi watu wanaweza kuja na mambo mbalimbali waliyoyajua kumhusu mtu kiasi cha kuwezesha kumtambua mtu huyo.

Na hii ndio sababu ya kufanya kitu kinachoitwa "gwaride la utambulisho" yaani "identification parade". Inawezakana usiwe unamjua kila kitu mtu lakini ukaweza kumtambua kutokana na machache unayoyajua kumbusu mtu huyo. Hapa chini nitatoa mifano michache ya michoro ya polisi (police sketches) kulinganisha na picha halisi (actual photos) za watuhumiwa. Kwamba, hata kama mashuhuda hawakuweza kuwatambua watu hao lakini walijua mambo mbalimbali kiasi cha kuwezesha polisi kuwanasa watu hao.

View attachment 1111018
Kulia picha ya mchoro wa mtuhumiwa kufuatia maelezo ya mashuhuda na kushoto picha yake baada ya kutiwa mbaroni.

View attachment 1111020
Huyu mdada naye alikuwa na uhakika asingeweza kupatikana lakini kwa kutumia polisi na kumbukumbu ya mashuhuda utadhani ilikuwa ni "c & p".

Hii ina maana gani?
Kwa ufupi, maana yake ni kuwa matukio ya "watu wasiojulikana" hayafanywi na watu wasiojulikana. Watu wote wanaoitwa "wasiojulikana" wanajulikana angalau na watu wachache.
1. Wale waliowatuma - kama wametumwa na watu wengine.
2. Wale waliowaona kwenye tukio - hata kama hawajui yote lakini kuna mambo mashuhuda wanayajua kuhusu watu hao.
3. Kwa kujumlisha vyanzo mbalimbali inawezekana kupata kwa kiasi kikubwa taarifa zao na hivyo kuweza "kuwatambua".

Kwa msingi huo, wale wote wanaoamini wanafuatwa au wamewahi kukamatwa au kutendewa na "watu wasiojulikana" waanze kujiuliza kama kweli watu hao hawajulikani. Ni vizuri watu kama CDM au vyombo vingine kuanza kutumia "sketch artists" yaani wachoraji na kuanza kutengeneza picha za wahusika ili watu waanze kuwajua taratibu. Endapo picha za michoro za watu hao zikitengenezwa vizuri na kusambazwa watu wengine wataanza kutengeneza tahahadhari na hata kuweza kuwatambua kuwa ni kina nani.

Umuhimu ni kuwa wakati mwingine hawa watu wanaodhaniwa ni watumishi wa serikali, au vyombo vya dola wanawezekana kuwa ni wahalifu uchwara ambao wanatumia mianya mbalimbali kwa vile wanajua kuna watu wanaamini katika "watu wasiojulikana". Katika kuwafichua watu hawa wananchi, wanasiasa na watu wote wenye kulitakia mema taifa letu watakuwa wanalisaidia taifa na vyombo vya dola ambavyo kama wengi tunavyojua vina changamoto kubwa sana ya kupambana na wahalifu wa aina hizi.

Polisi wanapata shida sana kupambana na uhalifu na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya wahalifu. Hii ndio sababu mara nyingi tunasikia "uchunguzi haujakamilika". Sasa ni wakati wa kuwasaidia polisi kuwambua wale ambao walidhaniwa kuwa "hawajulikani".

Hii ni kwa sababu, kimsingi - hakuna 'watu wasiojulikana' kwani hata wanaodhaniwa "hawajulikani" tayari wanajulikana na watu wachache na wananchi wakikusanya nguvu zao kwa pamoja katika kuwajua basi watu hao wataweza kutambulika na tutaanza kutumia maneno kama "watu wasiotambulika" au "watu wasiojitambulisha" badala ya "watu wasiojulikana'.

Tunapotaka kusema kabisa kuwa "watu wasiojulikana" ni pale ambapo tukio limefanywa na hakuna mtu hata mmoja aliyeshuhudia na hivyo hakuna taarifa zozote za kujua kitu chochote kuhusu watu hao. Hapo LABDA tunaweza kutumia neno hili. Nje ya hapo...

Hakuna mtu asiyejulikana - labda awe mzimu!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
We mzee unapoteza muda tu. Ulishawahi sikia au ona reaction ya mkuu wa kaya ambaye katiba imempa jukumu LA kutulinda,

Sema au kemea raisi Magufuli aache kufadhili vikundi vya kigaidi dhidi ya RAIA, wasio na hatia vinginevyo watu wakianza kulipiza visasi hakuna atakayesalimika,

Wakiwashindwa wahusika halisi Kuna siku watu watavamia familia zao na kulipiza visasi,

Nami nasema halii hii ikiendelea wananchi watamwaga mboga. Watu watakamata wanafamilia wa raisi. Mawaziri, wakuu was vyombo vya ulinzi, watawachinja hadharani, siku inakuja
 
M.M,
Pole swaumu mkuu.
Asante kwa mchango wako huu, wakati ni muafaka.
Hakuna siasa hapa lakini kesi zote, na "mawazo fyatu" utayaona. Sihitaji ufafanuzi hapa.

This is a serious case of "known unknowns"

Kwa hali hii, kuongeza mchango wa Wanasaikolojia Watanzania itakuwa barabaara. Nafikiri wamo humu.

MM, kuna maneno mengi tu..."wapinzani" hawa nasikia wanawasha "madude" eti wanaweza hata kupinga kushangiliwa kwa mtu!
"Fisadi" ...enzi hizo ukiona shangingi unaweza kusema 'gari za wabunge, za mkopo tu" leo unasikia "fisadi huyo" au za EPA hizo, taharuki zinazoweza kutokana na maneno hayo, known unknowns?..basi nisiharibu hapa
WANAJULIKANA/WATAJULIKANA hata pale tusipo wajua.

Aluta continua
 
huwezi kumjua mtu asiyejulikana kama unashindwa tu kutambua hapa wanaotumia ID fakes maana yangu ni kubwa mno yaan tuko nao hapa hapa wasiojulikana wanaotambulika
 
Mmoja wao yuko hivi,

Anavaa miwani, uso una ndita sana, kipara kichwani, juu katikati ya kichwa kama kuna bonde (rift valley), ndevu nyeupe!

Wa pili,

Anavaa miwani, anapenda kulialia, hana ndevu, ana ngongingo (wowowo) japo mwanaume! Anavaa jeans imekatika magotini kama wahuni wa Tandale au Mburahati

Unachora lakini?????
 
Unaona
sasa, upo uwezekano wa kuwagundua, hivyo basi kama jinsi limekatika magotini basi ni wa Tandale au mburahati,
Mbona kwngine hutaji, walipotoka, mabatini? Magomeni au goni?
Utajua tu
 
Tokea umepata ufahamu na kujitambua,umeshawahi kuona sketch ikipitishwa kwenye vyombo vya habari kuwa mtu huyu anatafutwa hapa nchini?Mimi sijawahi ona hapa bongo,huko mbele sawa ila si bongo!
unaweza kupitisha sketch ukakuta ni ya kamanda Mambo Leo au Bashite. Nani ataitangaza??
 
Acha zako mzee kemea uovu, usimpake Nguruwe lipstick halafu ukaanza kuaminisha watu kuwa sasa kageuka kuwa binti mrembo!.

Tunapotumia maneno "Wasiojulikana" tunamaanisha wale ambao tunajua wana mafunzo ya kufanya operesheni bila kujulikana na raia wa kawaida.

Hatumaanishi kuwa eti hawajulikani!. Wao wenyewe wanajijua sasa iweje wasijulikane?
Hasomeki siku hizi, mfuasi mtiifu wa Dkt.Slaa
 
Mkuu MMM nasita kuamini mchambuzi mahiri kama wewe umegeuka kuwa ‘apologist’ wa jeshi la polisi.
Hili neno wasiojulikana ni tafsri isiyo rasmi ya maneno ya kiingereza ‘unknown subject’(UNSUB) au ‘perpetrator(PERP) ambayo ni ‘jargon’ ya polisi wa Marekani katika hatua za mwanzo za upelelezi wa jinai, yaani jinai imetendwa, na wahusika au mhusika bado hawajajulikana achilia mbali kutiwa nguvuni.
Kitakachofuata hapo ni upelelezi wa kina na ambao hautasitishwa mpaka wahalifu hao(UNSUBS or PERPS /wasiojulikana) wajulikane na kutiwa mikononi mwa dola na kisha sheria ifuate mkondo wake. Hiyo michoro na hata ‘profiling’(umekwepa kuitaja hii)
ni mbinu mojawapo tu za upelelezi.
Suala hapa ni kwamba jeshi letu la polisi limepeleleza hizo jinai zinazopelekea kuwa na “ watu wasiojulikana” kwenye jamii yetu kwa weledi na nguvu zake zote au imewapendeza tu kutupatia msamiati mpya wa watu kukogana kwenye majukwaa ya mitandaoni, magazetini na kwenye vijiwe?
Maana watanzania tu wapenzi sana wa misamiati mipya bila kuifanyia kazi.
Hilo la wahalifu uchwara kujificha kwenye kivuli cha wasiojulikana, tafadhali mkuu. Hawa wakwetu wamehusishwa zaidi na uhalifu wa kisiasa(jaribio la kuua na utekaji). Tena kwa walengwa fulani. Sioni kwa mfano wahalifu uchwara wakiwa na motive yoyote ya kumteka Mdude Nyagali!
Hitimisho langu ni kwamba jeshi letu likifanya au kama linaendelea kufanya wajibu wake kama ipasavyo, kwa weledi na ujasiri(ambao naamini wanao) “wasiojulikana” watajulikana na kuwajibishwa mbele ya sheria.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Sasa imekuwa ni kama kawaida tu. Kwamba, tunatumia maneno bila kujua hasa tunachomaanisha na hatujali sana madhara ya kutumia maneno hayo bila kumaanisha tunachotaka kumaanisha. Mfano mzuri ni haya maneno mawili ambayo sasa yameanza kukubaliwa kama kawaida - "Watu Wasiojulikana". Nina uhakika wanaotumia maneno haya wanataka kutuambia tu kuwa wahusika wanaozungumziwa ni watu ambao hakuna aliyewatambua au wao wenyewe hawakujitambulisha.

Nafahamu kuwa watu wanaposema "kujulikana" kimsingi wanataka kutuambia kumaanisha "kutambulika". Na kweli mara nyingi katika lugha ya Kiswahili tunaposema "kujulikana" tunataka kusema "kutambulika" au "kufahamika". Na kuna wakati bila ya shaka maneno hayo yanaweza kutumiwa kwa kubadilishana (interchangeable).

Hata hivyo, linapokuja suala hili la matukio ya watu kujikuta wanakamatwa na watu ambao baadaye ama wanakuja kutambulika kuwa ni maafisa fulani wa polisi basi neno "kujulikana" linakosa maana kidogo. Unapozungumzia "watu wasiojulikana" kuna maana kubwa sana. Kwa sababu kuna ngazi mbalimbali za "kumjua mtu" lakini hakuna mtu anayeweza kutokea mahali popote bila uwezekano wa "kujulikana" kabisa.

Mtu anapoingia nyumbani kwangu na mimi simtambui bado nina mambo kadhaa naweza kusema nayajua kuhusu mtu huyo. Kwa mfano naweza kusema "alikuwa ni mwanamme, mrefu, mwembaba kiasi na sauti yake yenye mikwaruzo". Katika ngazi hiyo kuna vitu basi "navijua" kuhusu mtu huyo hata kama "simtambui" ama kwa sura, jina au ajira yake.

Kwa wanaoangalia TV, filamu na hata utendaji wa polisi wa kawaida, mtu anaweza asijulikane lakini polisi wanaweza kumuita mchoraji wa picha za wahalifu na kwa kutumia maelezo ya mashahidi watu wanaweza kuja na mambo mbalimbali waliyoyajua kumhusu mtu kiasi cha kuwezesha kumtambua mtu huyo.

Na hii ndio sababu ya kufanya kitu kinachoitwa "gwaride la utambulisho" yaani "identification parade". Inawezakana usiwe unamjua kila kitu mtu lakini ukaweza kumtambua kutokana na machache unayoyajua kumbusu mtu huyo. Hapa chini nitatoa mifano michache ya michoro ya polisi (police sketches) kulinganisha na picha halisi (actual photos) za watuhumiwa. Kwamba, hata kama mashuhuda hawakuweza kuwatambua watu hao lakini walijua mambo mbalimbali kiasi cha kuwezesha polisi kuwanasa watu hao.

View attachment 1111018
Kulia picha ya mchoro wa mtuhumiwa kufuatia maelezo ya mashuhuda na kushoto picha yake baada ya kutiwa mbaroni.

View attachment 1111020
Huyu mdada naye alikuwa na uhakika asingeweza kupatikana lakini kwa kutumia polisi na kumbukumbu ya mashuhuda utadhani ilikuwa ni "c & p".

Hii ina maana gani?
Kwa ufupi, maana yake ni kuwa matukio ya "watu wasiojulikana" hayafanywi na watu wasiojulikana. Watu wote wanaoitwa "wasiojulikana" wanajulikana angalau na watu wachache.
1. Wale waliowatuma - kama wametumwa na watu wengine.
2. Wale waliowaona kwenye tukio - hata kama hawajui yote lakini kuna mambo mashuhuda wanayajua kuhusu watu hao.
3. Kwa kujumlisha vyanzo mbalimbali inawezekana kupata kwa kiasi kikubwa taarifa zao na hivyo kuweza "kuwatambua".

Kwa msingi huo, wale wote wanaoamini wanafuatwa au wamewahi kukamatwa au kutendewa na "watu wasiojulikana" waanze kujiuliza kama kweli watu hao hawajulikani. Ni vizuri watu kama CDM au vyombo vingine kuanza kutumia "sketch artists" yaani wachoraji na kuanza kutengeneza picha za wahusika ili watu waanze kuwajua taratibu. Endapo picha za michoro za watu hao zikitengenezwa vizuri na kusambazwa watu wengine wataanza kutengeneza tahahadhari na hata kuweza kuwatambua kuwa ni kina nani.

Umuhimu ni kuwa wakati mwingine hawa watu wanaodhaniwa ni watumishi wa serikali, au vyombo vya dola wanawezekana kuwa ni wahalifu uchwara ambao wanatumia mianya mbalimbali kwa vile wanajua kuna watu wanaamini katika "watu wasiojulikana". Katika kuwafichua watu hawa wananchi, wanasiasa na watu wote wenye kulitakia mema taifa letu watakuwa wanalisaidia taifa na vyombo vya dola ambavyo kama wengi tunavyojua vina changamoto kubwa sana ya kupambana na wahalifu wa aina hizi.

Polisi wanapata shida sana kupambana na uhalifu na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya wahalifu. Hii ndio sababu mara nyingi tunasikia "uchunguzi haujakamilika". Sasa ni wakati wa kuwasaidia polisi kuwambua wale ambao walidhaniwa kuwa "hawajulikani".

Hii ni kwa sababu, kimsingi - hakuna 'watu wasiojulikana' kwani hata wanaodhaniwa "hawajulikani" tayari wanajulikana na watu wachache na wananchi wakikusanya nguvu zao kwa pamoja katika kuwajua basi watu hao wataweza kutambulika na tutaanza kutumia maneno kama "watu wasiotambulika" au "watu wasiojitambulisha" badala ya "watu wasiojulikana'.

Tunapotaka kusema kabisa kuwa "watu wasiojulikana" ni pale ambapo tukio limefanywa na hakuna mtu hata mmoja aliyeshuhudia na hivyo hakuna taarifa zozote za kujua kitu chochote kuhusu watu hao. Hapo LABDA tunaweza kutumia neno hili. Nje ya hapo...

Hakuna mtu asiyejulikana - labda awe mzimu!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Maktaba hii🙌🏾
 
Maktaba hii🙌🏾
Asante kufukua hii, sijui ilinipitia wapi,!
Na. M. M. Mwanakijiji
Hakuna mtu asiyejulikana - labda awe mzimu!
Mzee Mwenzangu, Mkuu Mzee Mwanakijiji
Kuna wasiojulikana wa aina mbili, kuna "Wasiojulikana" na 'wasiojulikana' nilipandisha uzi wa namna ya kuwajua na kuwatofautisha. Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Hata hawa wasiojulikana wa juzi kati waliosimamisha basi la Tashrif, wakajitambulisha, wakaingia kwenye basi na mitutu ya AK 47, wakamchukua waliomchukua Mzee Kibao, wakamfunga pingu, wakashuka nae, wakaondoka nae ile Ijumaa asubuhi. JJ Mnyika anatangaza kuchukuliwa kwa mtu wao.

Jumamosi asubuhi Jeshi la Polisi wakapata taarifa ya kuokotwa mwili wa mtu Ununio, wakauchukua mwili huo na kuutelekeza mortuary ya Hospital ya Mwananyamala, Jumamosi saa 9 mchana, msemaji Jeshi la Polisi anatangaza Jeshi la Polisi linamtafuta Mzee Kibao, Jumamosi usiku Boni Yai na ndugu wanautambua mwili kwa kovu la mguuni!.

Rais wa JMT ambaye ni CinC anatoa amri ya uchunguzi wa haraka, ameyasikia matokeo yoyote ya uchunguzi huo?.

Siku ya mazishi wana Tanga wakasoma Albadir, tukawashauri Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!

Inaelekea CinC alidanganywa kuwa yule jamaa ni ring leader wa uhaini, just to justify what they did na masikini CinC wetu wa sasa, kwa IQ yake, akaamini!, akatangaza!, sisi wa jicho la tatu, tukamweleza kuwa watu wake anao waaminia wanamdanganya Uhaini My God!. Kuna Uwezekano Anadanganywa na Kadanganyika? I Don't Believe This!. Sitatizwi na Uongo Wao, Natatizwa na The Motives Behind Such Lies! tukamuomba mama Ombi kwa Rais Samia, tunakushukuru kwa mahubiri mazuri kuhusu haki, tunakuomba utende unachohubiri yasibaki kuwa maneno tuu lakini vitendo ni tofauti na tukawashauri watu wake Utamaduni Viongozi Kuwajibika umeishia wapi?, Mbona Mwinyi, mauaji Mwanza aliwajibika?. Tusiruhusu madoa haya ya damu kuichafua nchi yetu -Wajibikeni!
Wa mwisho kuwajibika na karma ya machozi, jasho na damu hizi ni mwenye dhamana.

Bado unadhani ni "wasiojulikana" au hawa ni 'wasiojulikana' ?.
P
 
Back
Top Bottom