Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Wazo Fyatu: Hakuna Watu Wasiojulikana...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,240
Reaction score
44,487
Na. M. M. Mwanakijiji

Sasa imekuwa ni kama kawaida tu. Kwamba, tunatumia maneno bila kujua hasa tunachomaanisha na hatujali sana madhara ya kutumia maneno hayo bila kumaanisha tunachotaka kumaanisha. Mfano mzuri ni haya maneno mawili ambayo sasa yameanza kukubaliwa kama kawaida - "Watu Wasiojulikana". Nina uhakika wanaotumia maneno haya wanataka kutuambia tu kuwa wahusika wanaozungumziwa ni watu ambao hakuna aliyewatambua au wao wenyewe hawakujitambulisha.

Nafahamu kuwa watu wanaposema "kujulikana" kimsingi wanataka kutuambia kumaanisha "kutambulika". Na kweli mara nyingi katika lugha ya Kiswahili tunaposema "kujulikana" tunataka kusema "kutambulika" au "kufahamika". Na kuna wakati bila ya shaka maneno hayo yanaweza kutumiwa kwa kubadilishana (interchangeable).

Hata hivyo, linapokuja suala hili la matukio ya watu kujikuta wanakamatwa na watu ambao baadaye ama wanakuja kutambulika kuwa ni maafisa fulani wa polisi basi neno "kujulikana" linakosa maana kidogo. Unapozungumzia "watu wasiojulikana" kuna maana kubwa sana. Kwa sababu kuna ngazi mbalimbali za "kumjua mtu" lakini hakuna mtu anayeweza kutokea mahali popote bila uwezekano wa "kujulikana" kabisa.

Mtu anapoingia nyumbani kwangu na mimi simtambui bado nina mambo kadhaa naweza kusema nayajua kuhusu mtu huyo. Kwa mfano naweza kusema "alikuwa ni mwanamme, mrefu, mwembaba kiasi na sauti yake yenye mikwaruzo". Katika ngazi hiyo kuna vitu basi "navijua" kuhusu mtu huyo hata kama "simtambui" ama kwa sura, jina au ajira yake.

Kwa wanaoangalia TV, filamu na hata utendaji wa polisi wa kawaida, mtu anaweza asijulikane lakini polisi wanaweza kumuita mchoraji wa picha za wahalifu na kwa kutumia maelezo ya mashahidi watu wanaweza kuja na mambo mbalimbali waliyoyajua kumhusu mtu kiasi cha kuwezesha kumtambua mtu huyo.

Na hii ndio sababu ya kufanya kitu kinachoitwa "gwaride la utambulisho" yaani "identification parade". Inawezakana usiwe unamjua kila kitu mtu lakini ukaweza kumtambua kutokana na machache unayoyajua kumbusu mtu huyo. Hapa chini nitatoa mifano michache ya michoro ya polisi (police sketches) kulinganisha na picha halisi (actual photos) za watuhumiwa. Kwamba, hata kama mashuhuda hawakuweza kuwatambua watu hao lakini walijua mambo mbalimbali kiasi cha kuwezesha polisi kuwanasa watu hao.

1111018

Kulia picha ya mchoro wa mtuhumiwa kufuatia maelezo ya mashuhuda na kushoto picha yake baada ya kutiwa mbaroni.

1111020

Huyu mdada naye alikuwa na uhakika asingeweza kupatikana lakini kwa kutumia polisi na kumbukumbu ya mashuhuda utadhani ilikuwa ni "c & p".

Hii ina maana gani?
Kwa ufupi, maana yake ni kuwa matukio ya "watu wasiojulikana" hayafanywi na watu wasiojulikana. Watu wote wanaoitwa "wasiojulikana" wanajulikana angalau na watu wachache.
1. Wale waliowatuma - kama wametumwa na watu wengine.
2. Wale waliowaona kwenye tukio - hata kama hawajui yote lakini kuna mambo mashuhuda wanayajua kuhusu watu hao.
3. Kwa kujumlisha vyanzo mbalimbali inawezekana kupata kwa kiasi kikubwa taarifa zao na hivyo kuweza "kuwatambua".

Kwa msingi huo, wale wote wanaoamini wanafuatwa au wamewahi kukamatwa au kutendewa na "watu wasiojulikana" waanze kujiuliza kama kweli watu hao hawajulikani. Ni vizuri watu kama CDM au vyombo vingine kuanza kutumia "sketch artists" yaani wachoraji na kuanza kutengeneza picha za wahusika ili watu waanze kuwajua taratibu. Endapo picha za michoro za watu hao zikitengenezwa vizuri na kusambazwa watu wengine wataanza kutengeneza tahahadhari na hata kuweza kuwatambua kuwa ni kina nani.

Umuhimu ni kuwa wakati mwingine hawa watu wanaodhaniwa ni watumishi wa serikali, au vyombo vya dola wanawezekana kuwa ni wahalifu uchwara ambao wanatumia mianya mbalimbali kwa vile wanajua kuna watu wanaamini katika "watu wasiojulikana". Katika kuwafichua watu hawa wananchi, wanasiasa na watu wote wenye kulitakia mema taifa letu watakuwa wanalisaidia taifa na vyombo vya dola ambavyo kama wengi tunavyojua vina changamoto kubwa sana ya kupambana na wahalifu wa aina hizi.

Polisi wanapata shida sana kupambana na uhalifu na kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya wahalifu. Hii ndio sababu mara nyingi tunasikia "uchunguzi haujakamilika". Sasa ni wakati wa kuwasaidia polisi kuwambua wale ambao walidhaniwa kuwa "hawajulikani".

Hii ni kwa sababu, kimsingi - hakuna 'watu wasiojulikana' kwani hata wanaodhaniwa "hawajulikani" tayari wanajulikana na watu wachache na wananchi wakikusanya nguvu zao kwa pamoja katika kuwajua basi watu hao wataweza kutambulika na tutaanza kutumia maneno kama "watu wasiotambulika" au "watu wasiojitambulisha" badala ya "watu wasiojulikana'.

Tunapotaka kusema kabisa kuwa "watu wasiojulikana" ni pale ambapo tukio limefanywa na hakuna mtu hata mmoja aliyeshuhudia na hivyo hakuna taarifa zozote za kujua kitu chochote kuhusu watu hao. Hapo LABDA tunaweza kutumia neno hili. Nje ya hapo...

Hakuna mtu asiyejulikana - labda awe mzimu!

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Acha zako mzee kemea uovu, usimpake Nguruwe lipstick halafu ukaanza kuaminisha watu kuwa sasa kageuka kuwa binti mrembo!.

Tunapotumia maneno "Wasiojulikana" tunamaanisha wale ambao tunajua wana mafunzo ya kufanya operesheni bila kujulikana na raia wa kawaida.

Hatumaanishi kuwa eti hawajulikani!. Wao wenyewe wanajijua sasa iweje wasijulikane?
 
Wape darasa hayo mafunzo polisi.mtu ana somea miezi 6 polisi kesho unataka hawe mpelelezi mkubwa.
hii idara ya jeshi la polisi bado inawakati mgumu kwenye kufundisha mi na zani kila mwaka wakawa wanarudi shule kila idara ili kuendana na mbinu za kisasa
 
Wasiojurikana jamii nzima inawajua ila inakuwa shida kuwataja kwasababu wana mamlaka na nguvu na dola!


Kwani wasiojurikana wa Nyalandu si wamejurikana? Je waaiojurikana wa Zachariah wa musoma waliopigwa lisasi si nao wanajurikana?
 
Na. M. M. Mwanakijiji
.......Ni vizuri watu kama CDM au vyombo vingine kuanza kutumia "sketch artists" yaani wachoraji na kuanza kutengeneza picha za wahusika ili watu waanze kuwajua taratibu. ...............
Ushauri wa watu kama CDM, CCM, CUF, ACT - Wazalendo n.k. kujipa mamlaka ya kuchora watu na kutuaminisha kuwa ni waarifu sikubaliani nao ila nisamehe bure kama nitakuwa sijakuelewa vizuri!
 
Kwaiyo umefyatuka sio!! Kwaiyo wasio julikana kweli hawa julikani !?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hizo akili zilikuwepo enzi za CHADEMA ya akina Dr.
Hiki cha waandikisha magari ya chama kwa jina la Mwenyekiti, wako busy kuwaza 2020 watapataje tena dili la kuiuzia CCM kiti cha mgombea URAIS.
 
Wasiojurikana jamii nzima inawajua ila inakuwa shida kuwataja kwasababu wana mamlaka na nguvu na dola!


Kwani wasiojurikana wa Nyalandu si wamejurikana? Je waaiojurikana wa Zachariah wa musoma waliopigwa lisasi si nao wanajurikana?
Hata wakitajwa hakuna cha kuwafanya!...... Udicteta ndo huo!
 
hao Teleza nao wamekuja kivyao,wameiga mwelekeo wa nchi yao
 
Ikitokea Mtu asiejulikana akawa ameingia kupiga tukio huku amevaa Mask itawezekanaje kumchora (sketch)?

Wacha hili wazo lako libaki tu fyatu kama ulivoliita.
Mask..inaficha sura si vingine...
 
Back
Top Bottom