Waziri wa teknolojia anatakiwa leo kuongelea mambo ya Artificial Intelligence (AI) na sio kufungia Mitandao

lukubuzo Samsis

JF-Expert Member
Nov 3, 2014
2,909
3,340
Waziri wa teknolojia anatakiwa leo kuongelea mambo ya Artificial Intelligence (AI). Dunia ipo huko sasa hivi.

Waziri wa teknolojia anatakiwa kuzungumza namna tunatakiwa kuanza kutumia e-commerce payment system.

e-commerce payment system ni kama huduma zinazotolewa na Paypal. Sasa hizi huduma za PayPal ziende vijijini.

Waziri wa teknolojia anatakiwa kuwekeza nguvu katika e-commerce payment system (or an electronic payment system).

Waziri wa teknolojia anatakiwa kuumizwa na kwanini watu wengi katika nchi aliyopo hawatumii electronic payment system.

Waziri wa teknolojia anakaa chini anawaza jinsi ya kushughulikia VPN? VPN inamkosea nini? Kwanza anazuia vipi?

Waziri wa teknolojia unakaa chini unaagiza watoa huduma kuzuia kutoa huduma kwa ClubHouse? Kuipata hadi utumie VPN.

Waziri wa teknolojia unaumizwa na watu kufanya mijadala ClubHouse? Siku ukiwa Rais kwa bahati mbaya? Utaua watu wengi.

Waziri wa teknolojia anasherekea watumiaji wa internet kuwa wachache. Tena anasema wapiga kura hawapo mtandaoni. Akili ndogo.

Waziri wa teknolojia atafute namna wananchi wapige kura online hata akiwa nje ya nchi siyo kushangilia kuikosa kura hiyo.

Sifa ya kuwa waziri (tena wizara zenye kuhitaji wataalan) isiwe uwezo wa kupanua mdomo kuimba taarab kwa sauti.

08/10/2023, Noida, India; International Conference on Smart Technology, Artificial Intelligence and Computer Engineering (ICSTAICE)

Hii ndiyo mikutano waziri wa Teknolojia anatakiwa kuhudhuria na kutoa hotuba. Aondoke na mawazo alete nyumbani.

Waziri wa teknolojia anatakiwa kuwa kiumbe hai mwenye ubongo unaofanya kazi. Kiumbe aliyefaulu vizuri shule na ana akili timamu.

MMM, Mtikila.
20231007_233144.jpg
 
🤣🤣Huyu fomu foo felia
Mwalimu wa cheti toka butimba na technology wapi na wapi
Hesabu tu alipata zero🤣🤣
Kuwa serious basi
Waiter lete glass Nina celebration 🤣🏌️
 
Tunafanya mistake sana kama nchi katika kitu ambacho sio cha kuchukulia poa ni technolojia..
Apo alipaswa awe mtu kweli very bright ata kama ajasemea hayo mambo ila awe na abc za dunia inavyoenda maana tech inabadilika kila leo..
 
Tusidanganyane, hii India:

Kituo kinapanga kudhibiti utumaji wa teknolojia zinazoibuka na kinaweza kupiga marufuku kabisa baadhi ya teknolojia hizi mpya za umri ambapo kinaona hatari kwa mtumiaji, au hatari ya usalama wa kitaifa, The Indian Express imebaini.

"Lakini, chochote ambacho serikali itaamua, sababu zake za kuzuia teknolojia yoyote zitarekodiwa kwa maandishi," afisa mkuu wa serikali alisema...

Chanzo: In digital Bill, Govt may ban some new tech citing user harm, security
 
Back
Top Bottom