Robots na mifumo yenye Artificial Intelligence ndio dunia ya kesho

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Zamani kipindi tunatizama movies kama Terminator na muendelezo wake, RoboCop, Irobot ya Will Smith iliyotoka 2004, na Animations mbalimbali kama Wall-E tuliweza kuona namna maisha ya Binadamu yalivyobadilika na kwa asilimia kubwa Kazi zikafanywa na Robots. Wengi wetu utotoni tuliona kama ni Fiction tu, na hazitakuja kutokea lakini ukweli ni kwamba sasa hivi ndio tunaanza kuishi ulimwengu huo, hususani kwa wale walioko Dunia ya kwanza.

Sasa hivi Gari nyingi ni Automatic, na mfumo wa gari za umeme ndio unaingia, na mfumo huu ukiwa dhabiti ni kwamba badae gari nyingi zitakuwa ni za ki-electronic, na zitakuwa na motherboard kama ilivyo simu na zitakuwa asilimia kubwa zinajiendesha zenyewe, yani full auto-drive. Sasa hivi gari nyingi matoleo mapya zinafungwa mfumo wa A.I, ambao unaweza kuwa unazungumza na gari lako na kuliamrisha baadhi ya vitu. Hivyo basi miaka ijayo gari nyingi hazitakuwa na Usukani, ni kuweka tu Destination unayotaka kwenda, kitu kinajipa chenyewe, hapo Madereva wataanza kukosa kazi.

Kwa upande wa Jeshini, sasa hivi kuna Teknolojia zinafanyiwa utafiti, ni kwamba zitakuwa ni Robots zilizofungwa dhana na vifaa vya kivita ambapo zenyewe ndizo zitakuwa zinaingia vitani, zitakuwa na uwezi wa kumgundua adui, na kumimina Risasi au mabomu. Tumeanza kuona Drone za kivita ambazo ni auto-pilot zikitumwa kumimina makombora maeneo mbalimbali, na sasa robots za ardhini nazo ziko kwenye majaribio. Kwa wenzetu maaskari wa uraiani, miaka kadhaa mbele hakutakuwa na Askari Binadamu wa kutuliza gasia au kumkamata muharifu, kazi zote za ulinzi na usalama zitafanywa na mifumo kama robots, CCTV camera, Thermodetector, na mifumo kibao. Hivyo Robot ndio anatumwa kukutia hatiani.
Hapo tayari askari na wanajeshi kazi zitakuwa zimepotea.

Hospitalini pia watu wa kada ya afya wataanza kupoteza ajira, sasa hivi kuna A.I ambazo ukizielezea matatizo yako ya kiafya zinaweza kukupatia ugonjwa, na kukushauri vipimo vya kufanya na kukupatia matibabu ya dawa na ushauri wa kiafya, A.I ya ChatGPT tayari inauwezo huo wa kuipa scenario na ikakupatia majibu ya mgonjwa wako. Bado pia vitakuja vifaa huko mbeleni ambavyo vitakuwa Multi-functional ambapo vitakuwa na uwezo wa kukupima na kujua matatizo yako ya kiafya papo hapo, na kukutibu. Hakutakuwa na mzunguko wa matibabu kwa sababu kazi zote za matibabu zitafanywa na mfumo mmoja. Hizi CT scan, Utrasound, na X-ray scan zitakuwa na uwezo mkubwa wa kung'amua ugonjwa na hautahitaji tena daktari atafasiri majibu ya vipimo. Mpaka hapo Madaktari na manesi, na wahudumu wengine wa afya wataanza kupoteza ajira.

Watu wa marketing, nyie shughuli yenu ndio basi tena, maana sasa hivi Instagram na Facebook zinafanya kazi hiyo, bado Search Engines kama Google, Bing na nyinginezo zinatumia mifumo ya A.I kwa ajili ya kutafuta wateja kwa kufanya suggestions za maudhui na bidhaa. Ukipenda Porno, utakuwa unaletewa bidhaa za porno, na kadhalika. Watu hapo washakosa kazi za masoko.

Watangazaji nao wako mbioni kukosa kazi, Spotify tayari inafunga mfumo wa A.I ambao utakao kuwa unakuelezea kuhusu mziki utakaoupiga katika mfumo wa historia ya msanii, kazi alizofanya, tuzo alizonazo, na mambo kadha wa kadha... Itakuwa kama watu wa radio wanavyozungumza. A.I ikiendelea kuboreshwa utashangaa kuona hata TV pia zinatangazwa na Robots. Vile vile mziki, siku hizi A.I zinapiga beats, zinaimba hata ukitaka zitumie sauti ya Snoop Dogg, zinaimba pia kama Harmonize. Movies zipo ambazo ni A.I generated.

Wale wazee wa kataa Ndoa, sasa hivi mmeletewa midoli maalumu ya kujamiiana nayo, wengi wetu tunamfahamu robot anayeitwa Sophia, ambaye anafikiri kama binadamu. Sasa miaka kadhaa mbeleni basi watakuwepo robots wa kike kwa ajili ya kazi hiyo, na hawatakuwa wanakuomba nauli au tuma na ya kutolea. Hivyo hivyo kwa wanawake, watakuwepo robots wa kiume ambao kazi yao itakuwa ni kuwaridhisha wanawake kadri wanavyohitaji, na hawatakuwa na kibamia.

Kwa kifupi karibia kila sector itavamiwa na mifumo ya kujiendesha yenyewe ambayo itakuwa na akili bandia "Artificial Intelligence" na inamsadia Binadamu katika kila nyanja na sekta. Na kazi ya binadamu itakuwa ni kukaa tu bila shughuli yoyote, akisubiri kuletewa chakula, kupewa burudani, na kufarijiwa.

Kwa wale wenye ndoto za Elimu, basi hii sekta ya Robotics, machinery, Artificial Intelligence and Computer Engineering, Software Engineering mi naona ndio Future ya baadae.

Wale wasomi wengine mjiandae kazi zenu kuwa replaced na Robots na A.I.

Robots will leave no stone unturned
 
Shukrani ni somo zuri hili!

Sasa elimu ya Filisofia tulio nayo je AI itaweza? Ila future ni elimu AI na Robots haswa kwa watoto wetu!
 
Shukrani ni somo zuri hili!

Sasa elimu ya Filisofia tulio nayo je AI itaweza? Ila future ni AI na Robots haswa kwa watoto wetu!
Kinachofanyika ni kwamba wanapandikiza maarifa yote ya binadamu kwa robots, hata hizo filosofia ni kitendo cha kuziamishia kwenye mfumo tu... Alafu pia A.I itakuwa na uwezo wa kujifunza mambo isiyoyajua, kwa sababu itapewa uwezo wa kufikiri. Hivyo mambo mengi itayajua
 
Back
Top Bottom