Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Feb 26, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yaani umbelembele wa Waziri Membe unaelekea pabaya baada ya kudhihirika kuwa mikakati yake ya kujitapa na kuwa kuna njama za kuizalilisha ziara ya Bin Kimuni. Huu ni ubovu wa serikali ya CCM ,serikali ambayo inaonyesha kila hali kuwa imejaa viongozi waongo na mmoja wapo ni huyu ,muuwaji ambae tayari alikwisha aamrisha polisi wajipange ili kukabiliana na WaPemba bahati nzuri Msemaji wa UN amemuwahi na kuivunja siri ya dhamira yao ya kutaka kufanya mauaji, hivi serikali hii haioni haitazami nchi zingine ambazo viongozi wanaposhiriki hutokea maandamano ya mabango na kuwasilisha barua kwa anaefanya ziara, ila jamaa wa UN ndio amepasua kuwa mambo ya Pemba kudhalilishwa yanafanyiwa utafiti wa kimataifa na juhudi za kuyapatia ufumbuzi matatizo yao hazikulala zinafanyiwa kazi. Ole wenu uchaguzi wa 2010 serikali ya CCM ifanye manyago Pemba hapo ndipo Un itakapomfunga Paka kengele.

  Endelea uone Mbabe Membe alivyoshushuliwa ,very simple ila ni pigo kwa serikali ya CCM.

  Date::2/25/2009
  Mwakilishi UN awatuliza Wapemba kuhusu ziara ya Ban Ki-moon
  Elias Msuya na Levina Jackob
  MWAKILISHI mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Oscar Fernandez Taranco, amesema kwamba, hakutakuwa na tishio lolote la kuvurugwa kwa ziara ya siku mbili ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayoanza leo.
  Taranco ametoa taarifa hiyo siku moja tu baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kudai kuwa kuna makundi yaliyojipanga kuvuruga ziara hiyo, akilitaja kundi la watu wanaojiita, "Wazee wa Pemba" na la wapinzani wa katibu huyo, ambaye ni raia wa Korea Kusini kuwa ndiyo yenye mpango huo.

  Wazee wa Pemba wanataka Umoja wa Mataifa uwasaidie ili kisiwa hicho kijitenge na Zanzibar ili kiwe na uhuru kamili, wakidai kuwa, kisiwa hicho kimekuwa kikibaguliwa katika mipango ya maendeleo na Membe alidai wazee hao walitaka kuandamana ili kuivuruga ziara hiyo.

  Alisema kuwa, Wapemba hao pamoja na kundi jingine kutoka nje ya nchi walipanga kufanya maandamano ya kumkashifu Ban Ki-moon na kusoma risala ya matatizo yao endapo wangefanikiwa kuusimamisha msafara wake.
  Lakini Taranco aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa, ameshaongea na kundi hilo baada ya kupokea barua ya malalamiko yao waliyoyawasilisha ofisi za Umoja wa Mataifa nchini.

  "Ni kweli tunalijua tatizo hilo na kwa bahati nzuri hao viongozi wa Wapemba nimekutana nao leo asubuhi na wamenieleza matatizo yao tukaongea na tumekubaliana kuyamaliza," alisema Taranco, ambaye hata hivyo hakufafanua kuwa UN itamaliza lini madai ya Wapemba hao.
  "Malalamiko ya Wapemba tumeshayajadili sana na nilishayawakilisha Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na juhudi zinafanyika ili kuyamaliza. Hivyo nawahakikishia Watanzania kuwa, hakutakuwa na tishio lolote katika ziara ya katibu mkuu huyo."


  Toka Kikwete afanye ziara Pemba hadi leo hawajawashiwa tena umeme ,Kikwete alikwenda na majenereta yake kisha akaondoka nayo ,ila ndio hivyo hata wapeleke umeme wa uranium CCM haitakiwi hata kuonekana Pemba na kura za WaPemba haziendi CCM hata mwisho wa dunia ,WaPemba wameikataa CCM na utawala wake ,hivyo hasira za CCM zitapasuka lakini kwa Pemba wasahau watabaki huko huko upande wa pili.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Mimi nilishangaa ni kwa nini waziri aliamua kwenda public na hizo allegations. Hata kama zingekuwa kweli, serikali ina njia nyingi ya kuzima dukuduku hizo za Wapemba bila kwenda public. Hayo matatizo wangeyashugulikia kimya kimya kama alivyofanya mwakilishi wa UN
  na hata ingeshindikana basi Wapemba wangeambiwa kuwa polisi haitawapa kibali cha kufanya maandamano. Inanikumbusha yule kijana aliyekuwa anapiga makelele kuashiria mbweha, mbweha, kumbe hamna kitu.
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hana jipya huyo. Hata wakati wa Sullivan pale Arusha alichemsha sana tu,,,, kiasi JK aliamua kumwamrisha kijeshi kuwa kuna utaratibu kasahau. Ni mtu wa kukurupuka sana huyu Bwana mzee.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mhh, lakini mbona nilishasikia kuwa anaandaliwa kuchukua mikoba pale Magogoni?:confused:
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sie huyu peke yake lakini ni CCM wote na utawala wao na mkuu wao hawana jipya ,kila kukicha maendeleo yanakwenda kusiko julikana ,la ajabu na ambalo linawawacha wananchi hoi ni pale wanapojisifu kuwa maendeleleo yamepanda kwa asilimia nyingi tu ,na pato la mwananchi limeongezeka sana ,sasa sijui pato la wananchi wanalolipata wao ndio kusudio. chukulia unaposema pato la korosho limeongezeka sana....utaona korosho inamsaidia mkulima kupata fedha nyingi ,hivyo linaposemwa pato la mwananchi limeongezeka jua kuwa Utawala wa CCM unafaidika na fedha ya mlala hoi ,ndio maana yake.
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Before kuwa waziri alishika nyadhifa zipi?
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Alikuwa afisa ubalozini Canada na kabla alikuwa UWT.
   
 8. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yeah ndivyo inavyodhaniwa na wengi. Ila elewa kuwa ili kuonyesha tofauti mjinga mmoja na mwingine ni lazima umteue mjinga kuliko. Yaani aliye mbumbu kuliko wewe,,, hapo watu watasema afadhali ya aliyepita.
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwa Membe kuonya kungali mapema ni sawa kabisa, Wapemba hawaaminiki kabisa!
   
 10. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Duu! ebwana ehh!! hii imetulia kweli Mangi, ndivyo ilivyo.
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wewe shukuru CCM ipo madarakani maana siku ikianguka basi ndio mwisho wako wa kushiriki hapa JF ,bisha :D
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  kwi!kwi!kwi! Msinivunje mbavu.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  :D :D
  Ndio maana hampewi nchi, tena shukuru sana CCM kwa kukupatia hata nafasi ya kupayuka payuka....!
   
 14. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #14
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwi, kwi, kwi, Kumbe ukiwa kilaza inabidi utafute vilaza wenzio ili wewe uonekana "Kipanga", kwi, kwi. Hii nimeipenda sana.
   
 15. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #15
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kwi, kwi, kwi.
  Leo raha kweli.
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Feb 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mkiambiwa waongo mna kuja juu ,hii hati ya uhuru wa kusema haikuletwa na CCM ,yaani mnazidi kudanganya tu ,yaani sioni ajabu ikiwa mawaziri ni waongo nyinyi wapiga debe mtakuwa hali gani.Kikwete yupo nje sijui kaulizwa suali simple akajibu eti umasikini wa Tanzania unamla kichwa ,maana sasa hivi sio hapati usingizi bali kichwa kimeanza kuliwa kwa umasikini hajui vipi ataikwamua Tanzania kutoka kwenye janga la umasikini.Huoni kama anawadanganya watu .

  Uhuru wa kusema ni haki ya kiraia ,utawala wenu mbovu wa kidikiteta ndio ulikuwa unabinya na kuigandamiza jamii ya Kitanzania isiwe na sauti ,mlisahau kuwa itafika siku uvumilivu utawaishia wananchi na ndio hapa tulipo na bado lazima maji mtaita mma. Nimefarijika hukuleta ubishi :D
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Feb 26, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Oooooh wabara wabaya wabara wabaya........haya Unguja V/s Pemba.....
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wewe si ulikutana na prez JK dukani kwako...No..no..! Kwenye duka la bosi wako.. Jinsi ulivyotetemeka kumwona kiboko ya wazee wa Pemba ukajitia Mjamaika.. Hata haya huna! Kama una ubavu kwa nini usimwambie live hapo dukani? Unasubiri hadi uje JF? Tena endelea kuishukuru CCM usie na adabu weye! Ingekuwa hicho chama cha jamaa wa kisiwa cha pili intaneti ungekuwa unaisoma kwenye magazeti na kuisikia redioni...:D
   
 19. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii thread ina kichwa cha habari "Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, MUONGO". Mimi kule kwa thread ya "JK amteua Jaji Kiongozi mpya" nilitumia neno Muongo, Mkuu SMU aliniomba niliombe radhi, SMU upo?, manake limetumika tena.

  Tukija kwa mada viongozi wetu hukulupuka mno. Watatue matatizo ya Wapemba hayatakuwepo hayo wanayotueleza eti kuwa kuna watu wamepanga kuvuruga ziara ya Ban. Wanaogopa nini ujio wa Ban kuvurugwa kwa mfano Mabango, manake wale wazee sidhani kama walikuwa watumie nguvu yotote, badala ya kuogopa yanayofukuta kule Pemba. Hawa tatizo wanafagia na uchafu kuutumbukiza chini ya zulia.
   
 20. O

  Ogah JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....aisee wee jamaa kwa kukariri ligi........!.....sasa unamtaka SMU ili uendeleze ligi au....?
   
Loading...