Waziri wa Maji, Juma Aweso amtumbua kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Dodoma (Duwasa), David Palangyo kumtaka asubiri kupangiwa kazi nyingine. Aweso amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa Palangyo.
Aweso.jpg


Amesema kuondolewa kwa kiongozi huyo iwe ishara kuwa hatakuwa tayari kufanya kazi na watu wazembe na ambao hawaendi na kasi ya Rais Magufuli.

“Najua kaka yangu umefanya kazi kubwa, hata hivyo lazima tuwe wa kweli kwamba Dodoma tunahitaji kasi zaidi kwa kuwa macho ya viongozi yanatazama hapa, sitakuwa mpole naomba utupishe utapangiwa majukumu mengine baadaye,” amesema Aweso.

Kiongozi huyo amesema hawezi kudanganywa kwa namna yoyote kwa kuwa anaifahamu Duwasa kuliko wanavyodhani na jicho lake liko hapo.

Amesema ni wakati wa watumishi wazembe kukaa mguu sawa na ikibidi waanze kupisha wenyewe na kusisitiza a kuwa atawapa ushirikiano mkubwa watumishi wote kuanzia ngazi ya chini ambao watakuwa wakiwajibika.

Waziri Aweso amewaonya watumishi wa Duwasa watakaoanza kukwamisha kazi ya mkurugenzi atakayeteuliwa, “hao ndio watakuwa wa kwanza kuondoka kabla ya huyo aliyepewa jukumu hilo.”
 
Safi nilikua nashangaa,kwanini maji ya Victoria hayajafika singida na dodoma,,,kwanini mabinti zetu waendelea kuungua meno kwa kunywa maji yenye chumvi kwasababu ya uzembe wa watu wachache tu...
 
Hebu aje na huku makongo aangalie nani anasimamia usambazaji maji, haiwezekani mwezi sasa hakuna maji.
 
Miradi mingi ya maji hasa ya vijiji ni hovyo kabisa,atumbue tu.Tunahitaji viongozi kama hao,sio akina Mbarawa.Alikuwa mzigo kwa Wizara ya maji.
Hivi unaamini kutumbua watu ndio jawabu? Haujiulizi kwa nini toka watu wamekuwa wakitumbuliwa hamna mabadiliko makubwa? Matatizo mara nyingi ni mfumo mzima wa utendaji na upungufu wa rasili mali.

Watatumbuliwa sana lakini hali itabaki hivyo hivyo kwa sababu hatutaki kuchunguza kwa uwazi chanzo cha matatizo yetu na kutafuta njia za kuyatatua.

Amandla...
 
Back
Top Bottom