Waziri wa Maji, Juma Aweso amtumbua kazi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma

Post ni kwa akili ya watu wa Dodoma tu. CHIDACHI mda mrefu sana hawana maji, makulu napo vivyo hivo kila siku ukipeleka malalamiko wanapiga danadana
 
Duwasa ni JIPU lililotunga usaa muda sana.
Fekenyua kwenye manunuzi utashangaa.
Kazi ni kwako.
 
Hivi Mkurugenzi kama huyu anapotumbuliwa huwa anapelekwa wapi? Anapewa desk tu huku akila mshahara wake uleule?

Hivi Waziri ana mamlaka ya kumtumbua Mkurugenzi wa Taasisi au anashauri tu kwa mamlaka iliyoteua ifanye kazi yake?
Mkurugenzi huyo aliyetumbuliwa anaweza kupangiwa majukumu mengine na muajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara iwapo alikuwa na mkataba wa kudumu i.e Permanent and Pensionable
Au Kama alikuwa na mkataba wa miaka 4 wanaweza kuvunja mkataba wake au kumfanya desk officer akivuta mshahara wake huku akisubiri mkataba uishe.

Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Maji Tanzania bara, wanateuliwa na Waziri wa Maji, kwa maana hiyo aliyekuteua ana mamlaka ya kutengua uteuzi wako iwapo utendaji kazi wako hautamridhisha pamoja na sababu nyingine za kiutumishi wa Umma.
 
Safi nilikua nashangaa,kwanini maji ya Victoria hayajafika singida na dodoma,,,kwanini mabinti zetu waendelea kuungua meno kwa kunywa maji yenye chumvi kwasababu ya uzembe wa watu wachache tu...
Kumbe singida na dodoma zina mabinti tu
Sikuwa nafahamu hii
 
Tatizo la maji ni kubwa sana ndani ya nchi hii, kama Mwanza maji yako ziwa Victoria lakini maji watu wanapata kwa mgao kwa wiki mara moja, Dar nako Bahari iko karibu lakini maji ya shida, sijui tatizo ni nini?
 
Hivi kutumbuatumbua ndio jawabu kweli la shida zetu
Ukweli ni kwamba kwa baadhi ya Miradi serikali inajificha nyuma ya kivuli cha kutumbua ili kuzuga, wakati tatizo ni la serikali yenyewe.

Kuna miradi inachukua miaka zaidi ya 10 kukamilika kwa sababu fedha zilizotengwa ni tofauti na zinazokuwa realized durung the project implementation kama ilivyo kwenye action plan!!!!
 
Back
Top Bottom