Waziri wa Magufuli, Ndugu Mwakyembe awatukana Waswahili

Kumbe kufungia gazeti alimlenga kumuadhibu Kubenea. Huyu nae anaupungufu kama yule wa mjengoni. Matamshi tata ndio sera zao.
 
nikitathmini mambo anayofanya dk mwakyembe, naona hamna haja ya kusoma, yule dingi pamoja na ELIMU yake kubwa aliyonayo, MAMBO YA KIPUUZI hayajawahi kumuacha salama
 
Njaa na tamaa humvunjia mtu utu na heshima yake.

Mwaki anazidi kuporomoka kiakili kadri siku zinavyosonga mbele. Amekuwa mropokaji kuliko mjenga hoja zenye mantiki.
 
Kwa waliosoma lugha kuna "denotative meaning" na "connotative meaning",
ya kwanza ni maana halisi ya kilichokusudiwa na ya pili ni zaidi ya kile kinachokusudiwa

Connotative meaning ya "mswahili" ni uncivilized, barbaric, unprogressive, na mengineyo, japo sijasikiliza mahojiano naamini mh waziri alimaanisha maana hiyo. Ni lugha flan ya kejeli kuonyesha arrogance ya mtu hasa kukuprovia kwamba yeye ni tofauti na wewe hasa katika masuala ya elimu, kutembea, maneneo ya kuishi (tandika vs Oysterbay), ni kawaida kwa baadhi ya makabila/watu kujitanabaisha kuwa wao sio "waswahili" kwa mkutadha huo
 
Saed Kubenea ni Mswahili na ana asili ya kisiwa cha Mafia. Lakini hakukupewepo ulazima wa Ndugu Mwakyembe kutujumisha sisi waswahili kwenye kutoa matusi mazito dhidi yetu kwenye utetezi wake.
Kwani ukiambiwa wewe ni mswahili utakuwa umetukanwa?
 
Sijaona tusi hapo, mtu anaposema Kubenea ni mswahili wa ajabu anaelengwa sio mswahili na wala haimaanishi kuabuse uswahili, ni sawa na kusema Kubenea ni Mtanzania wa ajabu,isingemaanisha tusi kwa watanzania,ni tofauti na kusema watanzania ni watu wa ajabu,au waswahili ni watu wa ajabu.

Ni either umekusudia kulikuza jambo (exagerration) kwa kuongozwa na mihemko ya kisiasa au hujaelewa kiswahili.
Kweli mkuu huyu ana mihemko ya kisiasa ina maana yeye hajawahi kumwambia mtu we ni mswahili...watanzania wote navyojua ni waswahili na neno mswahili kwa namna ta kitanzania ni mtu mjuaje...huyu mleta mada atafute lingine.
 
hakuna watu wanaitwa waswahili nchi hii acha kurukia mambo
Yani huyu ameshindwa cha kuandika...kma nu mwanamke atakuwa mmmmm...na kma ni mwanaume...duuuh! Ni hatari mtaani...hlf mode kichwa cha habari cha uchochezi mtu kma huyu wanaachaje uzi wa uongo kma huu
 
Huyu ni waziri mwandamizi kwenye wizara nyeti sana ya Habari.

kafanya mahojiano na Radio ya Ujerumani kuhusiana na suala la kufungiwa kwa gazeti linalomilikiwa na Said Kubenea.

Mwisho wa mahojiano yake waziri aliamua kuwatusi waSwahili.

Waziri huyu aliteuliwa na Rais Magufuli na alikula kiapo cha utumishi wa Umma kuwa atatumikia wananchi wa Tanzania pasipo upendeleo,madharau na kwa haki. Hii dhamana aliyopewa ni kubwa mno na sielewi kwa nini amekuwa ujasiri wa kutukana jamii moja ya watanzania kwenye suala la kikazi.

Sisi waswahili tupo na ni raia kama raia wengine. Tuna mapungufu yetu kama wengine na pia tuna mazuri yetu. Lakini tunatoa tahadhari kuwa watu waliopewa dhamana ya uongozi nchi hii wawe makini kwenye matamshi yao kwa sababu kuna uwezekano kesho

Ndugu Mwakyembe, alikuwa na haki ya kujitetea kuhusu hatua ya kulifungia gazeti lakini kwenye utetezi wake kaamua kuvuka mipaka.


Saed Kubenea ni Mswahili na ana asili ya kisiwa cha Mafia. Lakini hakukupewepo ulazima wa Ndugu Mwakyembe kutujumisha sisi waswahili kwenye kutoa matusi mazito dhidi yetu kwenye utetezi wake.


Tutuma barua rasmi ya kulalamika kwa Rais na vyombo vyote vya dola kuhusu matamshi ya ndugu mwakyembe.

Hivi kuna kabila la WQaswaili hapa Tanzania???? Hivi Waswahili ni kundi lpi hasa??? Labda tuanzie hapo kwanza....
 
Mimi niliomba kuhusu Mwakyembe, tumsamehe bure kama mnavyojua ile sumu ina madhara makubwa sana, hebu fikiria mpaka nywele ziliondoka, je katika mazingira kama hayo UBONGO WAKE utakua na hali gani?

Anahitajika arudi India
 
Kumbe kuwa mswahili ni kubaya kutokana na maneno ya waziri kumbe sisi wote watanzania ni watu wabaya tusio na elimu hatakama tuna elimu hatusaidi kitu kweli haya ni maneno yaliyo tolewa na mtu menye Phd anamdharau hata kiongozi wake anayetumia kiswahili kila sehemu anadharau hata utu wake
 
Back
Top Bottom