Waziri wa Magufuli, Ndugu Mwakyembe awatukana Waswahili

Waswahili wengi wao ni waislamu na wengi wao wanaishi pwani na wengi wao sio wasomi wa sekula.Msomi akisema"unakuwa kama mswahili" ana maanisha wewe hujaenda shule.l
 
Nia ya Mwakyembe alitaka kumaanisha kubenea hajasoma ni mswahili tu kama wakina Msukuma[/QUOTE
Ok,ila mimi naona ni heri mtu akwambie hujasoma kuliko akwambie huna elimu,manake kusoma ni darasani lakini elimu hukaa kichwani kutokana na kujifunza either kupitia darasani au hata kupitia uzoefu wako katika mambo mbali mbali,kwa hiyo unaweza hata kuwa na PHD lakini hujaelimika (na hapa ni haki kwa walimwengu kukucheka), lakini mwingine akawa hajasoma lakini kichwani kukawa na elimu kubwa kuliko hata aliesoma kwa kiwango cha PHD (huyu huwezi kumcheka kwa kuwa inawezekana jambo la kutokusoma lilikuwa nje ya uwezo wake).

Hapa nataka kumaanisha kwamba kama kamwambia hana elimu ni DONGO ZITO kuliko kumwambia hajasoma, kwa hiyo basi tushukuru amemwambia hajasoma kuliko angemwambia hana elimu.
 
  • Mbona sisi Watanzania wote ni Waswahili! Shida iko wapi?
  • Nijuavyo mimi Mswahili ni mtu anayetumia Lugha ya Kiswahili
Mswahili lugha yake ya kuzaliwa ni Kiswahili, lugha nyingine atazijua kwa kujifunza, aghalabu hutokea maeneo ya Mwambao.
 
Kuna jinsi na jinsi ya kumuita MTU MSWAHILI
Kuna maana ya KUMPAISHA MTU kuwa ni MTU kutoka PWANI mzungumza lugha ya kiswahili mbele ya watu wa BARA waongea KILUGHA na kiswahili kibovubovu MF; nalikwendagah.
Maana nyingine ni kumdharau MTU anayejifanya ni mtoto wa mjini mwenyewe maneno mengi ya ujanjaujanja yasio na maana hapa ni wajuzi ndo hutambua msemaji ana maana gani?
Dharau au utani
Hilo la kumwagiwa tindikali ni MASIMANGO yenye uchonganishi na yy angekuwa gazeti tosha KUFUNGIWA.
 
Huyu ni waziri mwandamizi kwenye wizara nyeti sana ya Habari.

kafanya mahojiano na Radio ya Ujerumani kuhusiana na suala la kufungiwa kwa gazeti linalomilikiwa na Said Kubenea.

Mwisho wa mahojiano yake waziri aliamua kuwatusi waSwahili.

Waziri huyu aliteuliwa na Rais Magufuli na alikula kiapo cha utumishi wa Umma kuwa atatumikia wananchi wa Tanzania pasipo upendeleo,madharau na kwa haki. Hii dhamana aliyopewa ni kubwa mno na sielewi kwa nini amekuwa ujasiri wa kutukana jamii moja ya watanzania kwenye suala la kikazi.

Sisi waswahili tupo na ni raia kama raia wengine. Tuna mapungufu yetu kama wengine na pia tuna mazuri yetu. Lakini tunatoa tahadhari kuwa watu waliopewa dhamana ya uongozi nchi hii wawe makini kwenye matamshi yao kwa sababu kuna uwezekano kesho

Ndugu Mwakyembe, alikuwa na haki ya kujitetea kuhusu hatua ya kulifungia gazeti lakini kwenye utetezi wake kaamua kuvuka mipaka.

Saed Kubenea ni Mswahili na ana asili ya kisiwa cha Mafia. Lakini hakukupewepo ulazima wa Ndugu Mwakyembe kutujumisha sisi waswahili kwenye kutoa matusi mazito dhidi yetu kwenye utetezi wake.

Tutuma barua rasmi ya kulalamika kwa Rais na vyombo vyote vya dola kuhusu matamshi ya ndugu mwakyembe.
Hacha unafiki wewe mleta hoja ebu toa nukuu ya matusi aliyotoa kwa waswahili. Au lete audio lasivyo utakuwa umetumwa na kuleta ushilawadu hapa.
 
Huyu ni waziri mwandamizi kwenye wizara nyeti sana ya Habari.

kafanya mahojiano na Radio ya Ujerumani kuhusiana na suala la kufungiwa kwa gazeti linalomilikiwa na Said Kubenea.

Mwisho wa mahojiano yake waziri aliamua kuwatusi waSwahili.

Waziri huyu aliteuliwa na Rais Magufuli na alikula kiapo cha utumishi wa Umma kuwa atatumikia wananchi wa Tanzania pasipo upendeleo,madharau na kwa haki. Hii dhamana aliyopewa ni kubwa mno na sielewi kwa nini amekuwa ujasiri wa kutukana jamii moja ya watanzania kwenye suala la kikazi.

Sisi waswahili tupo na ni raia kama raia wengine. Tuna mapungufu yetu kama wengine na pia tuna mazuri yetu. Lakini tunatoa tahadhari kuwa watu waliopewa dhamana ya uongozi nchi hii wawe makini kwenye matamshi yao kwa sababu kuna uwezekano kesho

Ndugu Mwakyembe, alikuwa na haki ya kujitetea kuhusu hatua ya kulifungia gazeti lakini kwenye utetezi wake kaamua kuvuka mipaka.

Saed Kubenea ni Mswahili na ana asili ya kisiwa cha Mafia. Lakini hakukupewepo ulazima wa Ndugu Mwakyembe kutujumisha sisi waswahili kwenye kutoa matusi mazito dhidi yetu kwenye utetezi wake.

Tutuma barua rasmi ya kulalamika kwa Rais na vyombo vyote vya dola kuhusu matamshi ya ndugu mwakyembe.
Sijajua kama kuna kabila la waswahili Tanzania,ila nachojua wako Kenya,na sioni sababu ya kuita majina ya kikabila kwenye siasa zetu.
 
Matusi gani mbona unashindwa kujieleza waswahili ni kabaila gani Tanzania
 
..mbona vijembe vyenye ukakasi wa kikabila ni jambo la kawaida siku hizi?

..labda hujavizoea tu?

..au uko nje ya nchi?

SWAHILIYA
 
Mkapa hakutukana watanzania usipotoshe alisema baadhi ya vyama vya upinzani

..sasa "baadhi ya vyama vya upinzani" siyo waTz?

..kauli ya Mkapa haikupaswa kutolewa na mtu wa hadhi na heshma yake hata kwa mTz mmoja, sembuse " baadhi ya vyama vya upinzani."
 
..sasa "baadhi ya vyama vya upinzani" siyo waTz?

..kauli ya Mkapa haikupaswa kutolewa na mtu wa hadhi na heshma yake hata kwa mTz mmoja, sembuse " baadhi ya vyama vya upinzani."
Drop uwe muelewa sio kujibu jibu tu nafikiri umejibiwa vizur hapo
 
Fafanua basi tusi gan katumia?? Kasema Fulani ni mswahili kutoka mafia ni tusi???
 
Back
Top Bottom