WAZIRI wa KILIMO Zanzibar hili Lako, enhee Wadudu wanfurutu ada matunda hayaliki

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Kama Wazenji hapa wapo au humu wamo napenda wanifikishie Raisi wa Zanzibar Dr. Husein Bin Ali Bin Husein el Mwinyi ya kuwa sasa ni aibu kwa matunda ya Zanzibar, ulitafunalo lina ndudu aka funza.

Hili sio la Raisi ni la Wizara ya Kilimo na waziri husika wa Zanzibar hapa Tanganyika sijawahi kula tunda lina n'dudu isipokuwa pale Tanga ilitokea mara moja mbili ikanibidi niwe nakula kwenye kiza tu.

Kilichopuuzwa ni kuwaachia wadudu hawa ambao inasemekana wamehamia na kuivamia Zanzibar kutokea bara kwa maana ya Tanzania bara japo sina uhakika maana matunda ya kariakoo na kwenye magengeni nakula sana sijawahi kuona.

Nahisi wizara na waziri husika wanataka kuhamishia masaibu yao upande wa bara na kuwatwisha mzigo wabara. Pest control ya Zanzibar haifanyi kazi vilivyo ,matunda sasa hayaliki nchana ni lazima uyale kizani.

Serikali iliangalie hili kwani ni jambo la aibu, unaona tabu hata kumkaribisha mgeni matunda haswa mahembe. Linalowezekana lifanywe.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Dah shida sana. Tunda laliwa kizani sio? Lakini si ndio tudanyavyo hivyo huwa tunazumaga taa halaf twala "Apple" baasi na ma'hembe nayo yaliwe vivo ivi
 
Zaidi ya vijishamba vichache vya karafuu, kuna nini cha maana kinalimwa Zanzibar hadi kuwe na wizara kamili ya kilimo?

Kazi za wizara hii ni zipi exactly? Ingeweza kuwa idara ndani ya ofisi ya makamu wa rais kuokoa fedha umma.
 
Back
Top Bottom