Zanzibar: Serikali yazuia Mazao ya Ndizi kutoka nje, ndizi za Veronica Mwanjala kuharibiwa ili kuzuia Magonjwa

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,663
Hii ni mojawapo mfanyabiashara wa bara anyang'anywa tenga 30 za ndizi na faini ya shilingi 50,000 kwa kosa la kuingiza ndizi Zanzibar

USSR

====

Alichoandika Askofu Mwamakula katika Ukurasa wake wa Facebook

MJANE WA DAR ES SALAAM ANYANG'ANYWA TENGA 30 ZA NDIZI ZANZIBAR KWA AMRI YA WAZIRI WA KILIMO WA ZANZIBAR!

Ofisi ya Haki ya Askofu Mwamakula imepokea taarifa kuhusu Veronica Mwanjala ambaye ni mama mjane na mjasiliamali kutoka Dar es Salaam kunyang'anywa ndizi zake kwa amri ya Waziri wa Kilimo wa Zanzibar.

Veronica Mwanjala ni mama wa watoto 2 na mjane kwa miaka 9 sasa. Tarehe 30 Januari 2023 alisafiri na meli ya usiku kutokea Dar es Salaam kwenda Zanzibar kupeleka biashara ya ndizi za kuiva. Asubuhi tarehe 31 Januari 2023, alipofika bandarini, mzigo wake ukalipiwa lakini baadaye mzigo wake ukazuiwa getini. Sababu zilizotolewa ni kuwa ndizi za kuiva au ndizi za aina yoyote haziruhusiwi kuingia Zanzibar kwa sababu soko la ndani linajitosheleza.

Kwa amri ya Waziri wa Kilimo ambaye alifika eneo la tukio maofisa wa Wizara ya Kilimo wa Zanzibar kwa kushirikiana na maofisa wengine kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar walichukua na kutaifisha ndizi zake tenga 30 na kupeleka kwa wafungwa. Pia, walimlipisha faini ya shilingi 50,000 kwa kile walichokiita kuwa ni kosa la kuingiza ndizi Zanzibar.

Hivyo, mama huyo amepoteza ndizi zake tenga 30, amepoteza nauli yake ya kwenda Zanzibar na kurudi Dar es Salaam, amepoteza pesa ya kulipia mzigo, amepoteza pesa shilingi 50,000 aliyolazimishwa kulipa kama faini, amepoteza mtaji wake. Akirudi Dar es Salaam atakumbana pia na shida ya kudaiwa pesa kutoka kwa watu waliomkopesha mtaji.

Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuona jinsi ya kushauriana jinsi ya kutatua tatizo hilo na kumsaidia mama huyo arudishiwa ndizi zake na pesa ya faini alizolipa. La sivyo, kama ndizi zimetumika, basi mama hiyo arudishiwe pesa ya tenga 30 ya ndizi kwa bei ya kule alikokuwa akipeleka ndizi hizo kama ni hotelini au sokoni.

Video ya hapa chini inaonesha maofisa wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakichukua ndizi. Video nyingine inayomuonesha Waziri wa Kilimo wa Zanzibar akiingia katika eneo la tukio kutoa amri ya kutaifisha ndizi tumeihifadhi, ila tunaweza kuiweka hadharani kama suala hili halitashughulikiwa kwa wakati.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

====

Waziri aeleza sababu mwanamke aliyezuiwa kuingiza ndizi Zanzibar​


Zanzibar. Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Mifugo na Biashara wa Zanzibar, Shamata Shaame Khamis ametoa ufafanuzi kuhusu tukio la kutaifisha tenga 30 za ndizi za Veronica Mwanjala aliyekuwa akizisafirisha kutoka Tanzania Bara kwenda Zanzibar kwa ajili ya biashara.

Katika mitandao ya kijamii imeonekana taarifa inayoeleza tukio hilo ikimtaja mwanamke huyo ambaye anadaiwa mjane na kueleza jinsi waziri huyo alivyoagiza maofisa kutoka wizara yake wataifishe ndizi hizo na kumtoza faini ya Sh50,000 kwa madai Zanzibar haihitaji ndizi kutoka Tanzania Bara kwasababu inajitosheleza soko lake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea jana Jumatano Februari Mosi, 2023 kisiwani humo. Hata hivyo, akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Februari 2, 2023, Waziri Shaame licha ya kukiri tukio hilo kutokea, amesema siyo kweli mzigo huo umekamatwa kwasababu Zanzibar inajitosheleza, isipokuwa ni kutokana na taratibu ambazo imejiwekea Zanzibar zinazokataza kuingiza ndizi kutoka nje kutokana na magonjwa yaliyoikumba migomba ya Tanzania Bara.

“Ni kweli tukio lipo lakini siyo kwa mazingira ambavyo linatangazwa kuwa Zanzibar inajitosheleza kwa ndizi ama kisa ni kutoka Tanzania Bara, uhitaji upo ila kwa mujibu wa sheria zilizopo haturuhusu kuingiza ndizi kwasababu ya kuzuia ugonjwa ulioshambulia migomba,” amesema.

Pia amesema mwanamke huyo aliingiza mzigo huo kimagendo maana hakuwa na kibali chochote huku akichanganya ndizo hizo na nyanya ili mzigo uonekane ni nyanya pekee.
“Hata hizo sanduku (matenga) sio 30 bali yalikuwa 15, na ndizi zilikuwa zimefichwa kwenye tungule (nyanya) ili kuonyesha kwamba mzigo huo ni wa nyanya kwahiyo inaonekana kabisa alikuwa akifanya jambo hilo akijua kuwa ni haramu,” amesema

Kuhusu faini, waziri amekiri mwanamke huyo kutozwa faini hiyo ya Sh50,000 lakini kuhusu kutaifisha mzigo akasema walitoa pendekezo kwa mwanamke huyo ama kuzirejesha alipozitoa au kuziharibu mbele yake akishuhudia jambo ambalo amedai hakuonyesha ushirikiano.

“Hivyo bado mzigo huo tunao, hakuonyesha ushirikiano, lakini kama akitaka kuuchukua tunamruhusu auchukue na asipouchukua tutaangalia ni njia ipi ya kufanya lengo kubwa ni kuzuia maganda yake ili yasilete magonjwa ya ndizi.
 

Waziri wa Kilimo Zanzibar ameamrisha kutaifisha tenga 30 za ndizi za Veronica Mwanjala, mjane wa watoto 2 kutoka Dar es Salaam na kumlipisha faini ya Sh. 50,000 akisema soko la ndani la Zanzibar halihitaji ndizi za Bara. Video inaonesha maofisa wa wizara wakipekua ndizi hizo.
 
Back
Top Bottom