waziri wa jinsia uko wapi?

waziri wa jinsia uko wapi?

hii nchi ishaingiliwa na pepo inahitaji maombi sana hao mawaziri wetu wanawaza posho tu na mishahara lakini kuhudumia wananchi hawataki mweee.
 
Joyce Kiria kumbe upo humu... aisee siku ukipata fursa ya kuhojiana an huyu mtoto nsombs uweke uzi hapa kabla ili tufuatilie kipindi...
 
Last edited by a moderator:
Serikali iko wapi na wamama??? mbona mnawatelekeza wapiga kura wenu, ambao wengi ni wanawake???
 
Jamani GTs hang on little bit. Waziri jinsia wanawake na watoto bado anachunguza kama aliyefanya huo UNYAMA ni Mwana CCM, basi usitegemee kwamba litatoka tamko lolote.

Lakini kama itabainika aliyefanya huo unyama ni MPINZANI believe me atafunga safari hadi TARIME na kutoa MACHOZI YA MAMBA.

Kama Sophia Simba ameshindwa kutoa tamko kwa binti wa miaka 16 aliyebakwa na Prof Kapuya. Japo tamko la kutaka suala la huyo binti lifikishwe mahakamani ile sheria ichukue mkondo wako. Je wewe mama Joyce Kiria bado unaamini kwamba Sophia Simba ni WAZIRI WA JINSIA WANAWAKE NA WATOTO WA TANZANIA? kama bado unaamini hivyo THEN YOU'LL BELIEVE ANYTHING IN THIS WORLD. Sophia Simba ni WAZIRI WA JINSIA WANAWAKE NA WATOTO WA CCM!, KALAGABHAHO.
 
Haiwezekani Wanawake wafanyiwe unyama huu wakati tuna Wizara tena inayosimamiwa na Wanawake wenzetu! Haiwezekani Wanawake tunafanyiwa unyama mkubwa kama huu na wengine kuuwawa kikatili na Wanawake viongozi/wabunge wamepiga kimya!

Haiwezekani hata kidogo! Kwa matukio kama haya nilitegemea Wabunge Wanawake wawe wamoja na ikiwezakana watoke nje ya bunge ili sheria kali zitungwe na pia Kampeni kubwa sana ifanyike nchi nzima ya kutokomeza unyama huu dhidi ya Wanawake...

Kama Waziri yupo kimya, Wabunge Wanawake Je?

Umoja wenu TWPG unafanya kazi gani ya maana kuliko maisha na Usalama wa Wanawake wemzenu? Haya matukio yakiwatokea ninyi je, mtaendelea kuwa kimya?


Unyama huu umefanyika mwezi wa nane huko kijiji cha Nyantira Tarime Mara.

Ajabu ni kwamba baadhi yetu tumekuwa tukiwasifu ndugu zetu wa Mara hasa wanaume kwamba ni kawaida sana mambo haya wao kufanya, badala ya kukemea tunawasifu. Najua hata hapa kwenye uzi huu tutawasifu kwa ukatili huu wa kutisha.

Wakati mwingine wanawake tunaona hatupo salama kama ambavyo wengi mnadai Tanzania tuna Amani! Kwa habari zaidi bonyeza www.wanawakelivetv.com

naomba radhi kwa picha za kutisha....

Vipi kuhusiana na wanawake waliopita Weruweru? Leo hawana tena msaada? Kwa ubaguzi uliotoa kwa wanawake wenzako hauna tena credibility ya kukemea uovu kwa kuwa na wewe pia ni mmoja wa kundi hilo ovu. Jitokeze hadharani kuwaomba msamaha wanawake wenzio ulowabagua kwa kujiita eti mlopita Weruweru ndio wanawake bora kwa hapa Tanzania.

Halafu mbona kama unajipa promo hapa JF na hiyo website yako? Vipi kama ungeweka story kamili na sio kutoa link ili watu watembelee site yako? Hiyo ni dalili ya kutokujitambua na kutokujiamini. Nakushangaa kwa ubaguzi ulowafanyia wanawake wenzio halafu leo unataka wakuunge mkono na pia unaomba support yao kwa kuwa tu umepatwa na shida wewe ya kutekeleza maslahi yako kwenye hili. Nani hajui kama unatumiwa kwenye hili? That's why watu wengi wanaamini kuwa wanawake wanatumika kirahisi sana. Jisafishe kwanza kwa dhambi ya ubaguzi halafu ndio uweze kukemea maovu na ukatili wanaofanyiwa wanawake wenzako. Umenielewa mke na mama bora unavyojiita wewe kwa kuwa umepita Weruweru?
 
Serikali iko wapi na wamama??? mbona mnawatelekeza wapiga kura wenu, ambao wengi ni wanawake???
Hilo muhimu sana,kina mama tanzania wamekua wasaliti kwenye kura hasa baada ya kupewa vimkopo njaa!bi dada ni bora ufanye makusudi ya kuwaelimisha akina mama madhara ya ccm ktk ustawi wa mtanzania
 
Mi cku zote naamini wanawake hawapendani naamini kabaka akiona na mzee pita pinda machoz akiona wa kwanza kulia atakua mzee machoz, dis is too much bora mzee jk smile awe mwepec wa kudondosha sain na kunyongwa mara moja watu wenye ukatli kama wa kijinca
 
Haya hayawezi kuisha hadi wanawake wapunguze au waache kujipendekeza kwa watawala...

Wanawake wana nguvu sana. Bahati mbaya nguvu hiyo imezama kwenye kuvaa khanga, Tshirt na scarf za kijani huku wakiendekeza kukata viuno kwa nyimbo za kipuuzi za akina Komba na TOT yao....

Sishabikii ila kwa kiwango kikubwa, wanawake wenye madaraka ndiyo wanaoendeleza huu ukatili kwa kujiona kama nao wamekuwa wanaume!!
 
huyu joyce ndiyo yule mmewake anamwagia watu tindikali ukiolewa na mwizi lazima usaidie kuiba na ukiolewa na mwagia watu tindikali lazima na wewe uwe unamwagia watu tindikali ndivyo alivyo joice kwa sasa.

Kama huu ndio mwisho wako wa kufikiri basi sio muda mrefu utakuwa unatumia M-a-s-a-b-u-r-i kama kichwa.... Pole kwa hilo. Kumbuka umezaliwa na Mwanamke. Fikiria ukatili huu afanyiwe mama yako wa kukuzaa; je uwezo wako wakufikiri utaishia hapo? Self attack will not help you in any way. Tafakari kwa utashi uliotunukiwa.
 
Yule waziri kazi yake ni kuzunguka na mipasho tu hana lolote analofanya. Hao ndio mawaziri wa kubebwa. Spika wa bunge nao hakuna lolote kapachikwa tu pale na mafisadi atafanya nini?
 
huyu joyce ndiyo yule mmewake anamwagia watu tindikali ukiolewa na mwizi lazima usaidie kuiba na ukiolewa na mwagia watu tindikali lazima na wewe uwe unamwagia watu tindikali ndivyo alivyo joice kwa sasa.

Tchhhhhhhhh!!! Unawaza Kwa kutumia nini wewe? Mada Ni ya huzuni tena inayogusa hisia za watu we unaleta akili za MATEJA kwenye arguments?
Angekuwa Ni dada yako ama mama yako kafanyiwa ukatili huu unge-comment huu up ujuzo?

Next time use your brain and not the other body organs.
 
Chonde chonde ndugu zangu wa Mara tuache ukatili huu Kwa mama na dada zetu. Inaleta Aibu sana. Dada Joyce nafahamu unaguswa sana na hili jambo. Hima hima shirikianeni kuangamiza ukatili huu. Siyo Mara tu Hata mikoa mingine.
Sisi wanaume (baadhi yetu) tuko pamoja katika hili.
Sasa na tuseme ukatili BASI.
 
Back
Top Bottom