Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe atangaza kanuni za mitandao, radio na TV

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza kanuni mmbalimbali za sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010.

Kanuni hizo ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Habari za Mtandaoni) ya mwaka 2018 ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Online Content) Regulations, 2018.

Kanuni nyingine ni zile za sheria ya Mawasilinao ya Kielektroniki na Posta (Maudhui ya Utangazji katika Redio na Runinga) ya mwaka 2018, ijulikanayo kama The Electronic and Postal Communications (Radio and Television Broadcasting Content) Regulations 2018.

Kanuni hizo ambazo zimetengenezwa chini ya kifungu cha 103 cha sheria ya EPOCA zimesainiwa na Waziri Mwakyembe ambaye ndiye mwenye dhamana ya maudhui ya Habari na Utangazaji.

-————

Zile online content regulations zilizotangazwa jana tarehe 27.03.2018 na Mwakyembe hizi hapa

Vitu vya kuzingatia:

1. Kanuni ya 12 ndiyo itakwenda kukwamisha na kuzuia na kukamata watu(wahamasishaji wa vitu, wachochezi, wapingaji vitu wote wapo humo)

2. Mamlaka husika inaweza kumlazimisha mtu kutoa mtandaoni contents ndani ya saa 12

3. Online contents (media related) zimewekewa leseni ya Tsh. 1,000,000 kwa miaka 3, ikiwa ni gharama kubwa kuliko redio na television ambazo leseni zake zimewekewa Tshs 200,000 kwa miaka 3

Sasa unajiuliza: Kwanini online content ziwe 1,000,000 wakati unachohitaji ni Modem na Laptop yako nadhani wale wazee wa online TV watapatikana sana maana watafungiwa sababu hawana leseni?

--
Fungua HAPA kusoma kanuni zaidi.

Pia soma...

- Tanzania: The Electronic And Postal Communications (Online Content) Regulations, 2017

- Kanuni za Maudhui Mtandaoni: Bloga lazima asajiliwe na achuje taarifa pia awe tayari kuwataja wanaompa taarifa akitakiwa

- Kanuni za kusimamia Maudhui ya Mtandaoni: Je zitasaidia kuwainua wasanii kwenye tasnia ya sanaa?
 
Au hizo kanuni ndo zile hautakiwi kutoa taarifa yoyote ile "fact" ili kujiepusha inabidi utumie terminologies za kufikirika?
 
Asante tumepokea!.
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ni ya mwaka 2010, lakini kanuni ndio leo!.
Tukisema sisi Watanzania tunamatatizo seriously, mtasema hatuitakii mema serikali yetu!.

Hata hivyo tushukuru kwa madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, Prof. Mwakyembe, asante kwa kanuni hizi, sasa tunasubiri kanuni za sharia zetu mbili za habari. The right to information, na media services bill!.

P.
 
Tunaomba tupate hasa za blogs ili tusiende nje ya compliance, jf pse fuatilieni tupate hapa, sie sio wa kupitwa na habari
 
Asante tumepokea!.
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ni ya mwaka 2010, lakini kanuni ndio leo!.
Tukisema sisi Watanzania tunamatatizo seriously, mtasema hatuitakii mema serikali yetu!.

Hata hivyo tushukuru kwa madogo ili tuweze kupatiwa makubwa, Prof. Mwakyembe, asante kwa kanuni hizi, sasa tunasubiri kanuni za sharia zetu mbili za habari. The right to information, na media services bill!.

P.
Kwa umbumbumbu wangu nadhani kutunga kanuni ni kazi ngumu kuliko sheria
 
Back
Top Bottom