Waziri wa Habari, Nape Moses Nnauye awasilisha Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi 2024/2025, Mei 16, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,923
12,198
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 27, leo Mei 16, 2024 ambapo pamoja na Maswali na Majibu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye atasoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/25


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) akiwasili bungeni jijini Dodoma ambapo leo 16 Mei, 2024 atawasilisha Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa mwaka 2024/2025.
WhatsApp Image 2024-05-16 at 10.06.04_30766028.jpg

WhatsApp Image 2024-05-16 at 10.06.07_5c26f92d.jpg

Hali ya Upatikanaji wa Mawasiliano Nchini
Sekta ya Mawasiliano imeendelea kukua, takwimu zinaonesha kuwa laini za simu zilizosajiliwa zimeongezeka kutoka milioni 62.3 Aprili, 2023 hadi laini milioni 72.5 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 16.4.

Watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 33.1 Aprili, 2023 hadi milioni 36.8 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 11.2. Watumiaji wa huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya mtandao wa simu wameongezeka kutoka milioni 44.3 Aprili, 2023 hadi Milioni 53.0 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 19.6. Aidha, Idadi ya Watoa Huduma wa Miundombinu ya Mawasiliano imefikia 25 ikilinganishwa na watoa huduma 23 Aprili, 2023.

Kuanzishwa kwa Jamii Namba
Mfumo wa Jamii Namba, ambao utatumika kufanya utambuzi wa kipekee wa kila mwananchi kuanzia anapozaliwa ambapo atakuwa na akaunti ya kidijitali itakayomwezesha kupata huduma zote za
kijamii.

Mfumo wa Jamii Malipo, ambao utawezesha wananchi kutumia Jamii Namba kupokea fedha na kurahisisha kufanya malipo kidijitali. Mfumo huu pia utasaidia ujumuishi katika huduma za kifedha (Financial Inclusion) na kuongeza Wigo wa mapato ya Serikali.

Mfumo wa Jamii Data Shirikishi, ambao unamwezesha mwananchi kumiliki taarifa zake katika kupokea huduma mbalimbali nchini.

Hali ya Sekta ya Habari Nchini
Serikali imeendelea kuimarisha Sekta ya habari nchini ambapo vituo vya kurusha matangazo ya runinga
vimeongezeka kutoka vituo 65 mwaka 2023 hadi vituo 68 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 4.6 na Cable Television zimeongezeka kutoka 57 Aprili, 2023 hadi 60 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 5.3.

Vituo vya kurusha matangazo ya redio vimeongezeka kutoka vituo 215 mwaka 2023 hadi vituo 231 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 7.4 na magazeti yameongezeka kutoka 321 Aprili, 2023 hadi 351 Aprili, 2024 sawa na ongezeko la asilimia 9.3.
 

Attachments

  • FINAL_20HOTUBA_20WIZARA_20YA_20MAWASILIANO_202024-25.pdf
    13.9 MB · Views: 4
Back
Top Bottom