Waziri wa elimu Huku mashuleni watalaamu wa unasihi tupo ila tumeambiwa hatuhitajiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa elimu Huku mashuleni watalaamu wa unasihi tupo ila tumeambiwa hatuhitajiki

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nkisumuno, Aug 2, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimekusikia bungeni waziri ukisema mtajitahidi kufanya kila linalowezekana kupata wataalamu wa Counselling
  Kwa taarifa yako baadhi ya walimu wamesomea unasihi yaani counselling mimi nikiwa mmoja wao nina shahada lakini hata hivyo tulipoleta vyeti tukaambiwa shahada yenu haitambuliki. Hivyo tunahesabiwa kama hatukusoma.

  Baada ya kuona hivyo baadhi ya walimu wameacha kazi na kwenda kufanya kazi kwenye mashirika mbalimbali. Counselling ni muhimu sana katika jamii hasa mashuleni, hospitalini, katika majeshi, katika jamii nk. Leo hii vijana wanaiga mambo kwa vile tu wamekosa kujiamini, hivyo wanajiingiza katika ulevi, umalaya nk kumbe counsellors wanaouwezo wa kuwasaidia na kupata jamii iliyo bora.

  Matatizo mengi ya jamii hutokana na matatizo ya kisaikolojia. Hivyo waziri agiza shahada zetu zitambuliwe ili tufanyie kazi taaluma hii muhimu maana kwa sasa tumekaa kimya wala hatutumii taaluma hizo.
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii taaluma ni ya muhimu sana katika kutatua matatizo mbalimbali katika jamii yetu yenye mikanganyiko ya mambo mengi Hata Wabunge na hasa Viongozi wao wanahitaji sana hii huduma. Naomba ukaombe nafasi huko kwanza, wakishaona umuhimu wake watapitisha huduma hii itolewe sehemu zote hizo ulizoshauri na nyinginezo nyingi.
   
 3. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Kwani kumfanyia Counselling Mwanafunzi ni lazima kwanza Cheti chako kitambuliwe? Naomba kueleweshwa hapa. Nina maana mfano wewe ni Mwalimu mwenye diploma ya Ualimu umeajiriwa baada ya hapo ukaenda pale IUCo kusomea Shahada ya Counselling ukimaliza si unakuwa na ujuzi na unaweza kuutumia kuwasaidia wanafunzi hata kama Cheti hakijatambuliwa? Naomba kueleweshwa hapa
   
 4. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inawezekana kufanya hivyo tatizo ni kwamba utafanyaje kazi ambayo haithaminiwi, unaweza kufanya sawa lakini si kama vile ambavyo ungefanya huku ukithaminiwa kwa maana ya kiofisi, kwa sasa nafanya kwa kujisikia si kama inavyopaswa. Na ikumbukwe kuwa watu wote wanahitaji counselling, kwani watu wote wanamsongo wa mawazo hivyo wanapaswa wapate elimu namna ya kukabiliana nao au namna ya kuishi na msongo wa mawazo kwa usalama ( How to cope with stress, since stress is there)
   
 5. Voice of Wisdom

  Voice of Wisdom JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 541
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  najaribu kufikiria ni kwa kinsi gani imewezekana kwa chuo kufundisha kozi ambayo haitambuliki! Inanipa mashaka sana kwamba ni ama kuna sababu za kisiasa nyuma ya hilo swala au wakati wanaanzisha hiyo kozi walikuwa hawajajipanga, by the way unachotakiwa kufanya ni ku-"demostrate" kile ulichokipata hata katika mazingira magumu.
  Isitoshe una nafasi kubwa sana ya kufanya kimatendo ukizingatia wewe ni mwalimu,fanya kwa bidii na kwa moyo bila kujali kadhia watu waone matokea(wanafunzi wenye tabia njema) hatimaye watakudhamini. Tumia hyo fursa ya kuwa mwalimu kuwafanyia "counsel" wanafunzi weka bidii katika kuwabadilisha walioshindikana, isikupe shida kama hakuna ushirikiano, iko siku watatambua umuhimu wa elimu yako.
   
 6. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,204
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 180
  Nimeyapenda sana maelezo yako Mkuu nkisumuno. Nakutakia kila la heri katika Utumishi wako, elimu yako itakuja kuthaminiwa siku moja.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashukuru sana mkuu!
   
 8. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ushauri nimeuchukua nitaufanyia kazi inapowezekana
   
Loading...