Gonjwa la Corona: Waziri wa Afya mbona unazidi kutuchanganya? Wananchi wanataka elimu sio matamko

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Nimepigwa na butwaa kusikia Waziri wa Afya akisema kuwa matamko juu ya Covid 19 basi. Maana viongozi wakuu wameshatoa matamko sasa kila mtu achukue wajibu wa kujilinda.

Hivi hili gonjwa linahitaji matamko au elimu endelevu na kukumbusha wananchi kuwa makini mara kwa mara?

Wewe kama waziri mwenye dhamana na afya za Watanzania, unalichukulia vipi hili gonjwa?

Kwamba waziri mkuu na rais wakisema watu wavae barako na kunawa mikono ndio inatosha?

Wewe ni mwenye dhamana na afya za Watanzania, kuwa makini na jinsi unavyolichukulia poa hili gonjwa
 
Kama amesema hivyo, basi huyu Waziri hajitambui!

Tumeanza kusikia matangazo ya malaria tangu mwaka gani na mpaka leo yanaendelea?
 
543200.jpg
 
Back
Top Bottom