Waziri wa afya kikaangoni!

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Kuna kikao cha siri kimefanyika usiku huu na wabunge wa CCM wameazimia kumng'oa Waziri wa Afya. Si ajabu kesho tukiona wakimshinikiza kwa nguvu zote aachie ngazi.

Wasiwasi wangu ni kuwa watatoa povu jingi kuonyesha kuwa wana machungu lakini mwisho wa siku yatajirudia yaleyale ya kina Ngeleja.

Nafuatilia kwa karibu hapa Dodoma, nitakujulisheni kinachojiri na pengine kabla ya kucha.
 
Ha!
Hii itakuwa elimu mpya kwa kizazi hiki!...Bora hata enzi hizo bunge hilo lilipomng'oa EL lilikuwa serious kidogo....sasa hivi limekuwa na wachumia tumbo mno!
 
Kuna kikao cha siri kimefanyika usiku huu na wabunge wa CCM wameazimia kumng'oa Waziri wa Afya. Si ajabu kesho tukiona wakimshinikiza kwa nguvu zote aachie ngazi.

Wasiwasi wangu ni kuwa watatoa povu jingi kuonyesha kuwa wana machungu lakini mwisho wa siku yatajirudia yaleyale ya kina Ngeleja.

Nafuatilia kwa karibu hapa Dodoma, nitakujulisheni kinachojiri na pengine kabla ya kucha.

thax, tunasubiri kwa hamu!
 
labda c wabunge wa magamba! Ctegemei jipya toka kwao:...
 
Yani siku hizi hawawezi kuingia bungeni bila ya kuwa na kikao cha pamoja! Mwanzo wa dalili mbaya!
 
nasikia kichefuchefu nikisikia na kuwaona wabunge wa CCM, uozo mtupu wakiongozwa na Pinda
 
Kwani hao wabunge wa CCM ndio walimteua kuwa waziri?
 
Kwani hao wabunge wa CCM ndio walimteua kuwa waziri?

Kama sababu za kiutendaji zipo za kumuondoa madarakani basi ataondoka,yuko wapi Jairo leo?? hakuteuliwa na wabunge yule... Ilianza tu kwa hoja ya Beatrice Shelukindo,lolote laweza kutokea....tusubiri!
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Mbona wamekuwa vigeugeu juzi walikuwa wamemkaba shingo Dr. Kigwangwala leo waziri?
Kuna umuhimu wa Lowasa kuchukua nchi 2015
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Unajua mimi niliona kitendo cha wabunge wa CCM kumcheka Mnyika baada ya hoja yake kupigwa chini ilikuwa kama faraja lakini moyoni walitambua umuhimu wa jambo hilo.

Baada ya kuona hivyo wanataka kujitia wanafanya maamuzi ambayo yatakijeng chama. Nawashauri kama wanaweza wasafishe wizara ya afya kwa kuwatimua wote watendaji kuanzia waziri Mponda.
 
Usitegemee hawa jamaa hata wangekaa namna gani au mara ngapi wanaweza kumbana mwenzao, ni kulindana tuuuuuuu na kutoa povu kisha yanaishia hapo hapo. Atapinga mpaka basi na kuishia KUUNGA mkono hoja!!!!!
 
kimsingi ni lazima mtu awajibike,wananchi wameteseka na kufa kwa sababu ya uzembe wake.
 
Kuwajibika bado ni kugumu wa Waafrika hasa watanzania upo tayari baba yako, mama yako na ukoo mzima utukanwe lakini kuachia ngazi ni mwiko!!!!
 
Back
Top Bottom