Waziri wa Afya awataka Wakuu wa Wilaya kuchunguza hospitali zinazotoza hela ya kadi ya Kliniki

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,108
2,000
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Dk. Dorothy Gwajima amewaagiza wakuu wa wilaya zote nchini kufuatilia mienendo ya watumishi wa afya katika hospitali, vituo vya afya na zahanati wanaokiuka sheria za nchi na utaratibu wa utumishi wa umma kwa kuwatoza wakina mama wajawazito kwa kuwauzia kadi za kliniki kati ya shilingi 2000 hadi shilingi 5000 ili watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria.

Amebainisha hayo wakati akizindua mpango maalumu wa utekelezaji wa watoto wachanga Nest 360 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Temeke Jijini Dar es salaam ambayo imeboresha huduma kwa kuhudumia watoto kutoka watoto 20 Mwaka 2019 hadi kufikia watoto 70 mwaka 2021 kwa siku hali iliyopunguza msongamano katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha Dkt Gwajima Ametoa siku saba kwa hospitali zote nchini kuonyesha taarifa ya utekelezaji wa mpango maalumu watoto wachanga Nest 360 kwa lengo la kupunguza vifo vya watoto wachanga wanaopoteza maisha kwa sababu zisizo zuilika ili kuwa na taifa lenye afya njema.

Chanzo: ITV
 

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
8,044
2,000
Hakuna haja ya kuchunguza,
Mbona iko wazi kabisaa,
Ni mtego mdogo tu mutawakamata wengi sana sema tatizo wengi ni ndugu kwa ndugu kwa hiyo hii ni kama kuwaalert Ili wakae chonjo😂
 

pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
8,044
2,000
Saa hii tunavoongea ni saa tano na nusu usiku hakuna umeme misheni kota kariakoo yaani ni joto la kufa mtu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom