Waziri Ummy Mwalimu, tunaomba MDH wasiondoke mkoa wa Geita

NAFIKIRE

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
634
415
Wasalaam ndugu wana Jukwaa,

Kwanza nianze bandiko langu kwa kumpongeza Mhe. Waziri wa afya kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya ndani ya hii Wizara kubwa na muhimu sana kwa Watanzania. Hongera sana mheshimiwa Waziri Ummy. Wewe ni jembe haswa kwa maoni yangu na ni askari wa mwavuli wa Mheshimiwa Rais.

Sasa nihamie kwenye kiini cha bandiko langu. Mheshimiwa Waziri Kuna taarifa za shirika lisilo la kiserikali MDH kuacha kufanya kazi zake mkoani Geita kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu. Kama nitakuwa sijakosea kwangu mimi kama mdau wa afya hii taarifa imeniumiza sana sijui kwa wenzangu.

Sijui ni vigezo gani vilivyotumika kuwaondoa MDH kama wadau wa afya mkoa Geita. Mheshimiwa Waziri, shirika la MDH kwa miaka ambayo limefanya kazi mkoa wa Geita limefanya kazi nzuri sana na ya kutukuka. Kama ni viashiria vya utendaji kazi vya sekta ya UKIMWI wamefanya vizuri sana na kwa taarifa zilizopo wanakuwa wa pili au wa kwanza kila wakati Kitaifa.

Kama hiyo haitoshi Waziri, MDH wametoa ajira nyingi mno kwa Watanzania watumishi wanaofanya kazi katika hospitali, vituo vya afya na zahati nyingi kama sio zote za mkoa wa Geita. Mheshimiwa Waziri, MDH wameshiriki katika kuboresha miundombinu na kujenga majengo kwenye vituo vingi sana kwenye mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Waziri, MDH wamewajengea uwezo watumishi wengi sana wa afya katika mkoa wa Geita. Kiujumla Mheshimiwa wamefanya mambo makubwa sana kwenye sekta ya afya kwa mkoa wa Geita. Chonde Chonde Mheshiwa Waziri hawa wadau wasiondolewe kwenye mkoa wetu.

Mheshimiwa Waziri nilikusikia ukisema moja ya wadau wa afya ambao ungependa kufanya nao kazi ni mdau anayetoa ajira kwa Watanzania. Mheshimiwa Waziri, MDH wamelifanya hili kwa mafanikio makubwa.

Mheshimiwa Waziri ombi langu kwako, na kwa maslahi mapana ya sekta ya afya mkoa wa Geita tunaomba sana MDH wasiondolewe katika mkoa wa Geita. Hatuna uhakika na mdau mwingine aliyechaguliwa Kama anaweza kufanya kazi nzuri na iliyotukuka Kama ya MDH ndani ya mkoa wa Geita.

Nimalizie bandiko langu kwa kukurudia tena kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Kazi iendelee.
 
Kwani Wanaondoka au Wamefukuzwa? Kuna kitu wameharibu? Kwa nini serikalikali isiajiri na kujenga hadi wasubiri MDH?
 
Kwani Wanaondoka au Wamefukuzwa? Kuna kitu wameharibu? Kwa nini serikalikali isiajiri na kujenga hadi wasubiri MDH?
Serikali haiwezi kufanya kila kitu yenyewe..ndio maana inashirikiana na wadau Kama MDH.na matokeo ya ushirikiano wa serikali na wadau wa afya umekuwa na faida kubwa sana kwa serikali na watanzania
 
Back
Top Bottom