Waziri Ummy Mwalimu: Matumizi holela ya P2 yanaweza kusababisha ugumba na saratani

Savage Dad

JF-Expert Member
Jul 10, 2018
1,388
2,613
Kupitia ukaunti yake rasmi, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amenena haya kuhusu watu wanaofanya mzaha wa matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba aina ya P2.

Ummy Mwalimu.PNG

Inaweza kuonekana ni utani lakini huu ndio ukweli hasa kwa baadhi ya watoto wetu wa kike walio shuleni.

P2 ni dawa ya kuzuia mimba zisizotarajiwa mathalani kutokana na kubakwa, kondom kupasuka na kwa waliokosea hesabu za siku zao za hedhi na hivyo kujikuta wamefanya yao na ili kuepuka kutoa mimba (abortion) au kuzaa watoto wasiowatarajia wanaweza kutumia dawa hii. Hivyo kama Serikali tusingependa kuziwekea vikwazo dawa hizi. Tunatamani upatikanaji wake usiwe na changamoto yaani ziwe zinapatikana haraka na kwa kila mwenye uhitaji aliepata DHARURA.

Hata hivyo tunatambua kwamba kuna misuse ya hizi dawa hasa kwa watoto wa Shule ambao kwa sasa inaonekana wanaogopa zaidi mimba kuliko UKIMWI! Matumizi holela ya P2 yanaweza kuzalisha matatizo mengine makubwa ya kiafya kwa wasichana/wanawake. Wataalam wetu wamenihakikishia kuwa MATUMIZI HOLELA NA YA MARA KWA MARA YA P2 yanaweza kusababisha UGUMBA na SARATANI.

Tunaendelea kuliangalia suala hili kwa mapana yake. Wakati tunaendelea kulijadili ndani ya Serikali na wadau, hatua ya haraka tutakazo kuchukua ni kuongeza KASI YA UTOAJI ELIMU ya juu ya madhara ya matumizi holela ya dawa hizi (P2). Nimeshawaelekeza timu yangu kulitekeleza hili haraka.

Nasi Wazazi/Walezi tusione aibu kuwaeleza mabint zetu madhara ya ngono za mapema na kuepuka ngono zisizo salama. Kama binti/msichana unaona hupo tayari kuzaa basi unashauriwa kutumia njia za uzazi wa mpango na siyo P2
 
Tuendelee kuunga mkono juhudi za serekali.
Kabisa haya ndio mambo tulokuwa tunayataka.

Utandawazi kama ulaya.

Iko siku watasema watoto wasikatazwe kula vitu ila wapewe elimu.
 
Si mko tayari kusomesha Wazazi na wajawazito, iweje tena mhamasishe watumie P2! Acheni Mabeberu yatukimbize kadri yatakavyo.
 
Back
Top Bottom