Waziri Ummy: Tumewanusuru Wakazi million 3.7 wa Manispaa mbili za DSM na Magonjwa ya Mabusha na Matende, tumesitisha Zoezi la Dawa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,995
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amempongeza mganga wa mkoa wa DSM kwa kufanikisha kuwanusuru wakazi milioni 3.7 na maradhi ya Mabusha na Matende

Ummy amesema zoezi la kuwamezesha Wananchi Dawa limesitishwa lakini limekuwa na mafanikio makubwa sana

Manispaa 2 na Kata 10 za mkoa wa DSM zimekunywa Dawa za Mabusha na Matende

Source Upendo TV
 
Kwani mkoa mzima wa Dar una wanaume wangapi hadi manispaa mbili tu zifikishe hiyo idadi ya wakazi 3.7m na ukizingatia hakukuwa na uhamasishaji wowote mkubwa kwa watu kunywa dawa? Au ni kwa miaka mingapi? Takwimu zimepikwa?
 
Wanawake hawahusiki na matende?
 
Takwimu uchwara, manispaa mbili Ina watu wangapi Hio? 3.7... kwa io bila dawa wakazi wote wangekua na mabusha na matende sio
 
Back
Top Bottom