Huyo ndio waziri katika serikali dhaifu anawauliza wananchi wake kwa nini uchumi wa Kenya uko juu kuliko wa Tanzania.Serikali ilioko madarakani ndiyo iliyoua iliokuwa Tanzania Germstone ambayo ndio iliyokuwa na wajibu wa kusimamia madini kama Tanzanite,Greem garnet, rubby,nk Ndiyo iliyotakiwa iwe inanunua madini hayo kutoka wachimbaji wadogowadogo.Lakini serikali hii hii ikafilisi shirika lile wachimbaji wadogo wakakosa soko na kuanza kuuza Kenya na kuifanya nchi ya Kenya kuwa muuzaji mkuu wa Tanzanite nje wakati Tanzanite inapatikan a Tanzania pekee.Leo ndio Waziri anawahoji wananchi wake kwa nini Keanya ni tajiri kuliko Tanzania na kuwaasa waache siasa.Anjaribu kuwadanganya wa Arusha mchana kweupe.Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.
Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.
"Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.
"Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.
"Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu," alisema Profesa Muhongo.
Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.
"China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5," alisema Profesa.
"Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu," alisema.
"Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana," alisema Prof. Muhongo.
Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini," alisema Profesa Muhongo.
"Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300," alisema.
Kweli kuna umhimu wa mawaziri kutokua wanasiasa sasa, nchi hii itapiga hatua sana..... SENGEREMA.
Hana tofauti kubwa sana na wenzake kwani hawawajibiki pamoja.Wizara yake kwa ujumla wake haewezi kubadili lolote kama hakuna collectve resonsibillity.Anglia yanayoanikwa kila siku ufisadi katika wizara yake .Yeye anawaza hili lakini watendaji ndani ya wizara yake wanawaza tofauti kabisa.Namsikitikia sana pamoja na jitihada zake likini komba ni wengi wanangangania kibuyu kidogo cha mnazi.Naamini yeye ni smart person,hatokuwa mnafiki kama wenzake na pamoja hana muda mrefu ofisini lakini tofauti yake na wenzake nimeiona.Hope atasaidia kuwa sehemu ya kukua kwa uchumi...!
Hana tofauti kubwa sana na wenzake kwani hawawajibiki pamoja.Wizara yake kwa ujumla wake haewezi kubadili lolote kama hakuna collectve resonsibillity.Anglia yanayoanikwa kila siku ufisadi katika wizara yake .Yeye anawaza hili lakini watendaji ndani ya wizara yake wanawaza tofauti kabisa.Namsikitikia sana pamoja na jitihada zake likini komba ni wengi wanangangania kibuyu kidogo cha mnazi.
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.
Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.
"Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.
"Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.
"Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu," alisema Profesa Muhongo.
Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.
"China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5," alisema Profesa.
"Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu," alisema.
"Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana," alisema Prof. Muhongo.
Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini," alisema Profesa Muhongo.
"Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300," alisema.
Huyo ndio waziri katika serikali dhaifu anawauliza wananchi wake kwa nini uchumi wa Kenya uko juu kuliko wa Tanzania.Serikali ilioko madarakani ndiyo iliyoua iliokuwa Tanzania Germstone ambayo ndio iliyokuwa na wajibu wa kusimamia madini kama Tanzanite,Greem garnet, rubby,nk Ndiyo iliyotakiwa iwe inanunua madini hayo kutoka wachimbaji wadogowadogo.Lakini serikali hii hii ikafilisi shirika lile wachimbaji wadogo wakakosa soko na kuanza kuuza Kenya na kuifanya nchi ya Kenya kuwa muuzaji mkuu wa Tanzanite nje wakati Tanzanite inapatikan a Tanzania pekee.Leo ndio Waziri anawahoji wananchi wake kwa nini Keanya ni tajiri kuliko Tanzania na kuwaasa waache siasa.Anjaribu kuwadanganya wa Arusha mchana kweupe.