Waziri Profesa Sospeter Muhongo: Punguzeni siasa wananchi wa Arusha nchi bado maskini

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.

Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.

Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.

“Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.

“Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.

“China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5,” alisema Profesa.

“Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu,” alisema.

“Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana,” alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini,” alisema Profesa Muhongo.

“Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300,” alisema.
 
Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
500
Naamini yeye ni smart person,hatokuwa mnafiki kama wenzake na pamoja hana muda mrefu ofisini lakini tofauti yake na wenzake nimeiona.Hope atasaidia kuwa sehemu ya kukua kwa uchumi...!
 
Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,033
2,000
Angeanza kuwaambia akina Wassira, Nape, Mzinzi 1st class a.k.a mkaba koo kwa bendera yetu tukufu.
 
mnduoeye

Senior Member
Jun 30, 2012
166
0
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.

Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.

Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.

"Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.

"Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.

"Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu," alisema Profesa Muhongo.

Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.

"China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5," alisema Profesa.

"Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu," alisema.

"Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana," alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini," alisema Profesa Muhongo.

"Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300," alisema.
Huyo ndio waziri katika serikali dhaifu anawauliza wananchi wake kwa nini uchumi wa Kenya uko juu kuliko wa Tanzania.Serikali ilioko madarakani ndiyo iliyoua iliokuwa Tanzania Germstone ambayo ndio iliyokuwa na wajibu wa kusimamia madini kama Tanzanite,Greem garnet, rubby,nk Ndiyo iliyotakiwa iwe inanunua madini hayo kutoka wachimbaji wadogowadogo.Lakini serikali hii hii ikafilisi shirika lile wachimbaji wadogo wakakosa soko na kuanza kuuza Kenya na kuifanya nchi ya Kenya kuwa muuzaji mkuu wa Tanzanite nje wakati Tanzanite inapatikan a Tanzania pekee.Leo ndio Waziri anawahoji wananchi wake kwa nini Keanya ni tajiri kuliko Tanzania na kuwaasa waache siasa.Anjaribu kuwadanganya wa Arusha mchana kweupe.
 
mnduoeye

Senior Member
Jun 30, 2012
166
0
Naamini yeye ni smart person,hatokuwa mnafiki kama wenzake na pamoja hana muda mrefu ofisini lakini tofauti yake na wenzake nimeiona.Hope atasaidia kuwa sehemu ya kukua kwa uchumi...!
Hana tofauti kubwa sana na wenzake kwani hawawajibiki pamoja.Wizara yake kwa ujumla wake haewezi kubadili lolote kama hakuna collectve resonsibillity.Anglia yanayoanikwa kila siku ufisadi katika wizara yake .Yeye anawaza hili lakini watendaji ndani ya wizara yake wanawaza tofauti kabisa.Namsikitikia sana pamoja na jitihada zake likini komba ni wengi wanangangania kibuyu kidogo cha mnazi.
 
manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,067
2,000
Atleast huyu Muheshimiwa anajitahidi sana ila labda ni sababu ya ugeni kwenye kapu la samaki waliooza?

Time will tell.
 
Mgaya D.W

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
965
500
Hana tofauti kubwa sana na wenzake kwani hawawajibiki pamoja.Wizara yake kwa ujumla wake haewezi kubadili lolote kama hakuna collectve resonsibillity.Anglia yanayoanikwa kila siku ufisadi katika wizara yake .Yeye anawaza hili lakini watendaji ndani ya wizara yake wanawaza tofauti kabisa.Namsikitikia sana pamoja na jitihada zake likini komba ni wengi wanangangania kibuyu kidogo cha mnazi.

Nakubaliana sana nawe mkuu,lakini walu anaonesha dhamira ya kweli ktk kushughulikia masuala muhimu.Kwa nature ya wizara ya Nishati na madini nimekuwa nikifikiria mara nyingi unajua mkuu kitendo cha wizara hii kuwa na mawaziri watatu waliotoka kwa kashfa si rekodi nzuri kiutendaje na ili kuleta maendeleo.

Lakini walau kumpa moyo,mimi ni mwananchi wa kawaida ial walau ktk kipindi hiki cha miezi kadhaa aliyoingia walau kuna tofauti japo si kubwa lakini ipo.Miaka ya nyuma kipindi hiki tulikuwa ktk hali ngumu kinishati nadhani unakumbuka vema.So naweza kusema kwa juhudi inaonekana.Japo najua anahujumiwa sana na watendaji na hata baadhi ya wakurugenzi wa board ya Tanesco lakini amekuwa na msimamo ktk analoliamini.
 
Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,736
0
Ne siamina kama watanzania hawafanyi kazi,wanafanya kazi sana na mwishowe wao akina muhongo ndo wanawaangusha watanzania,namaanisha kuwa viongozi ndo wanawanyong'onyesha watz,
 
MNYISANZU

JF-Expert Member
Oct 21, 2011
7,047
2,000
Kumbe na huyu waziri ni bogus! Kwa hiyo kufanya siasa ni kuipenda CHADEMA?! Mbona hawaambii wakazi wa Tanga, Pwani na Lindi kwamba wapunguze siasa na wafanye kazi?! Ana kinywa kichafu sana.
 
HUGO CHAVES

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
2,045
1,500
waziri muhongo anapita wakazi wa arusha ni wachapakazi sana na hili analijua kati ya watu waliothirika na mgao wa umeme ni wakazi wa arusha asilimia kubwa ya wakazi wamejiajiri angewaomba radhi kwa yaliopita .pili wakazi wa arusha ni waelewa wa mambo yanavyokwenda hii ni kutokana na vuguvugu lililokuwa linaendelea pale nairobi ,shughuli nyingi za kibiashara hutegemea mahusiano y apande mbili kenya na tanzania tatizo linatokea nairobi taarifa zinafika mapema arusha kuliko dar .upevu huu ni kikwazo kwa watawala kufanya mambo yao .wananchi watahoji na kutaka kujua ukweli .
 
Nyasirori

JF-Expert Member
May 3, 2009
333
500
Lakini Arusha si ni wao wana CCM wanaopeleka siasa. Hawaamini kwamba hawakubaliki na hivyo kila mara wanataka ushindani na Chadema.
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,497
2,000
Asitufundishe maisha huyu mzee.
Tunajua tunachofanya.
Yeye afanye yake atuache na maswala yetu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
SoNotorious

JF-Expert Member
Sep 11, 2011
2,422
1,195
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.

Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.

Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.

"Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.

"Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.

"Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu," alisema Profesa Muhongo.

Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.

"China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5," alisema Profesa.

"Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu," alisema.

"Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana," alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

"Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini," alisema Profesa Muhongo.

"Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300," alisema.

how can you develop without politics in the development equation, a very bogus professor, we have been out of politics for over fifty years and nothing has changed, politics is nothing but development watch dog. arusha people should be more political active and more radical otherwise maendeleo mtakuwa mnayasikia kama ndugu zenu wa kusini walioamua kufa green.
 
Job K

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
9,322
2,000
Anamaanisha nini huyu mgonjwa? Yaani hii nchi tuna shida sana misomi yetu ni mipumbavu tu sijui kwa nini? huyu naye anatuambia umaskini wetu unatokana na Ars kupenda siasa? Upumbavu mtupu! wakishabikia ccm hawasemi!! Huyu naye ni walewale.
 
Japtz

Member
Nov 16, 2012
23
0
Huyo ndio waziri katika serikali dhaifu anawauliza wananchi wake kwa nini uchumi wa Kenya uko juu kuliko wa Tanzania.Serikali ilioko madarakani ndiyo iliyoua iliokuwa Tanzania Germstone ambayo ndio iliyokuwa na wajibu wa kusimamia madini kama Tanzanite,Greem garnet, rubby,nk Ndiyo iliyotakiwa iwe inanunua madini hayo kutoka wachimbaji wadogowadogo.Lakini serikali hii hii ikafilisi shirika lile wachimbaji wadogo wakakosa soko na kuanza kuuza Kenya na kuifanya nchi ya Kenya kuwa muuzaji mkuu wa Tanzanite nje wakati Tanzanite inapatikan a Tanzania pekee.Leo ndio Waziri anawahoji wananchi wake kwa nini Keanya ni tajiri kuliko Tanzania na kuwaasa waache siasa.Anjaribu kuwadanganya wa Arusha mchana kweupe.

kweli kabisa mkuu.moja ya sababu kubwa sana iliyotufanya tanzania tusiwe na maendeleo miaka 50 baada ya uhuru ni hii ya kuwa na viongozi ambao ama hawajui mambo yanayotufanya tusipate maendeleo au wanatuhadaa wananchi kwa uongo dhahiri shahiri.na kama tutaendelea na mfumo huu wa kuwa na viongozi namna hii,basi tutegemee miaka 50 mingine pasipo kutoka ktk umaskini wetu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom