R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,573
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.
Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.
Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.
Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.
Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.
Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu, alisema Profesa Muhongo.
Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.
China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5, alisema Profesa.
Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu, alisema.
Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana, alisema Prof. Muhongo.
Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini, alisema Profesa Muhongo.
Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300, alisema.