Waziri Profesa Sospeter Muhongo: Punguzeni siasa wananchi wa Arusha nchi bado maskini

Kweli acheni siasa, ili CCM iendelee.
Unahitaji kuwa genius ili uwe kiongozi wa ssm na uongee Point.
 
Chama chake cha ccm kimeiongoza hii nchi tangu uhuru. Kwa zaidi ya miaka 50 sera ambazo zimekuwa zikitekelezwa ni za ccm.
Kwahiyo umasikini walionao watanzania ni matokeo ya sera mbovu za ccm zinazochochea na kuhamasisha ufisadi.
Nadhani wakati Muhongo anatoa rai hiyo hakutumia akili ya kitaalamu bali alikuwa na mihenmko ya siasa uchwara ambazo amekuwa na bidii ya kuzifanya kadri siku zinavyokwenda.
 
Alhamisi, Novemba 29, 2012 04:49 Na Eliya Mbonea, Arusha

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amewashawishi wananchi wa Arusha kupunguza siasa na badala yake wajishughulishe na masuala ya kiuchumi.

Profesa Muhongo, alitoa kauli hiyo kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ya vito na mengine mkoani hapa.

Alisema wakati juhudi za kuendelea kuinua uchumi wa Taifa zikiendelea, ipo haja ya kujiuliza kwanini uchumi wa Kenya unapaa na kuiacha Tanzania yenye rasilimali, eneo kubwa na nchi yenye rutuba.

“Nimekuja Arusha kujaribu kuwashawishi tupunguze siasa, badala yake tujishughulishe na mambo ya kiuchimi.

“Mwaka 2015, wakati tutakuwa tunaendelea na siasa, Kenya uchumi wao utakuwa karibu mara mbili ya uchumi wa Tanzania.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na nyinyi, lazima tubadilishe hali hii, tusiwe taifa dhaifu,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema hadi kufikia mwaka 2050, China ndio taifa linalotajwa litakuwa na uchumi mkubwa duniani kuishinda hata Marekani inayoongoza sasa.

“China kufikia mwaka 2050, uchumi wake utakuwa Dola za Marekani trilioni 70.7. Marekani yenyewe itakuwa kwenye dola trilioni 38.5,” alisema Profesa.

“Marekani itakuwa na nusu ya uchumi wa Mchina kwa hiyo tuseme Mwalimu Julius Nyerere alikuwa ni nabii, kwani alijua kuwa China itakuja kutawala huu ulimwengu,” alisema.

“Ni muhimu muwe mnazijua ili muelewe mnakwendaje na hii hali. Je! sisi watu wa Tanzania, watu wa Afrika Mashariki tunaitaka? Jibu ni hapana,” alisema Prof. Muhongo.

Akizungumzia mifano halisi ya nchi zilizopiga hatua kiuchumi, Profesa Muhongo alitolea mfano wa uchumi wa nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Nchi hizi, zina watu milioni 127, pato lake la mwaka ni dola za Marekani bilioni 73. Tukimgawia kila mtu atachukua dola za Marekani 500, huu ni ukanda maskini,” alisema Profesa Muhongo.

“Uchumi wa nchi tano ukilinganisha na nchi ndogo ya Oman ya watu Milioni 2.8, pato lake kwa mwaka ni Dola za Marekani Bilioni 72, ukigawa kwa watu wake kila mtu anapata Dola 23,300,” alisema.

Wajua Serikali ya CCM inajisahau sana katika kunadi sera zake huko mikoani ili ingiza sana SIASA badara ya kuwafundisha watu njia za kiuchumi na kujijenga kiuchumi na kuwapa mianya wananchi ni jinsi gani ya kujikwamui kiuchumi na kuendelea kiuchumi kutoka katika ulalahoi.

Sasa wanakuja wakisema kwa wana Arusha waache siasa hivi nani alikuwa pandikizi la siasa kama sio CCM baada ya watu kuzinduka na kujua CCM ilikuwa na sera ya kujineemesha kisiasa na kiuchumi kivyake vyake na watu wake wachache na sasa kumefikia kubaya wanakuja na style ya kutuambia wana arusha waaache siasa hivi hili linamwingia nani akilini. ?? Mji wa Arusha unaandaliwa kuwa JIJI na bado haujawa JIJI kamili kwani hadhi yake kiutaalamu ni bado kabisaaaa nandio sasa watu wanajipanga mji haukuwi watu wanaogopa hamia nje ya mji kwa sababu ya miundombinu hakuna eg maji,umeme,barabara vingine ni Masoko hospital vituo vya police kwa ajili ya usalama hivi vyote ni duni sana katika mji wa arusha. Ukiangali viwanja tu vinavyo tolewa ni kwa ajabu sana ukienda hapo sakini bado ni kijijini mji haujapimwa na halimashauri leo hii mwataka kuwa jiji halaka hivyo?

Hivi Prof ulikuja kuyaongea haya kisiasa au kiutendaji? Leo hiii mvua ikinyesha ya masa 12 tu mji mzima unajaaa maji watu wote wa ngalelo wanakuwa kwenye janga la mafuriko na matejoo, na kwingineko hata rami zinazo jengwa tu juzi mvua imenyesha zimeanza kukatika jamani hii ni siasa au uwajibikaji ???? kama serikali imeshindwa tu kusimamia ujenzi wa mji leo hii itaweza kuwaambia watu waachane na siasa wakati serikali ndio mstari wa mbele kuhubiri siasa na kuitekeleza siasa.

Watu wa arusha wanatumia siasa kudai haki zao ndio njia pekee wanaona ndio ya ukombozi wanataka kuona rasilimali zao ziana wafanyia kazi na sioa zinaliwa na wajanja wachache huko serikalini na tatizo kubwa ya hii njii ni kufanya kila kitu Centralized kila kitu ni Dar. kwenye katiba me ntadai njii hiii irudi kwa majimbo period.

Prof Muhongo me nkajua umekja kutuambia twajaribu kuwa punguzia bei ya umeme ili isiwe shida kila mtanzania aweze kulipakwa hali hii ya uchumi tulio nayo ni ngumu sana. we waja na habari za siasa. Kama kweli ulisikiliza ile hotuba ya mwl. J.K Nyerere kule mbeya Mei mosi 1995 kwa umakini serikali ilitahadharishwa kwa mambo mengi sana hata CCM nayo iliambiwa esp kuhusu Azimio la Arusha kuwa hakukuwa na tatizo ila wajajnja wachache wakapinga kwa manufaa yao. Mramba aliambiwa swala la kukusanaya kodi na mwl.Nyerere alidokezwa na hao wakubwa IMF,WB kuwa watu wako hawakusanyi kodi na kwa sasa ukiangalia Kodi ya mtanzania wa kawaida ndio inaendesha njiii hiiii, esp 80% ya wafanya kazi wana katwa PAYE na hawaoni faida ya PAYE ila serikali inajilimbikizia na kuzila kwa semina za kinafiki. Leo hii utamwambia mtu aache siasa wakati CCM tu inanuka rushwa imewakatisha watanzani tamaa ya maendeleo.

Mkitaka SIASA ipungue ARUSHA watendeeni HAKI wana wa ARUSHA na AMANI ndi kweli siasa itapungua.

My Take;
Prof Muhongo we nenda ka deal na issues za mikataba ya madini yetu yanavyo liwa ili upunguze watu wajanja wasiendelee kuila ndilo twa kusiiiiiihi, yaaaani temana na sisi watu wa Arusha



 
Huyu Professor ameanza kukosa mwelekeo. Mimi nilishawahi kusema kuishabikia au kuipenda CCM is a mental disease.

Ona sasa Prof mzima anavyotoa pumba utafikiri Maji Marefu (STD VII). Hiyo kauli yake angeitoa Bagamoyo, Mkurunga etc ingekuwa na mashiko. Prof Mzima anaona kuipenda CDM ndiyo SIASA lakini kuipenda CCM sio SIASA ni maendeleo, POOR PROF Muhongo.
 
Chama chake cha ccm kimeiongoza hii nchi tangu uhuru. Kwa zaidi ya miaka 50 sera ambazo zimekuwa zikitekelezwa ni za ccm.
Kwahiyo umasikini walionao watanzania ni matokeo ya sera mbovu za ccm zinazochochea na kuhamasisha ufisadi.
Nadhani wakati Muhongo anatoa rai hiyo hakutumia akili ya kitaalamu bali alikuwa na mihenmko ya siasa uchwara ambazo amekuwa na bidii ya kuzifanya kadri siku zinavyokwenda.


Si mihemko, na wala hata hueleweki unapozungumzia 'akili ya kitaaluma'. Acha ushamba na ushabiki. Huna unalolojua wala wewe hutaweza kuwa na taaluma yeyeto ya maana kumfikia unayembeza.
Wenye akili hatuangalii mtu anatoka chama gani ndipo tukubali anachosema; tunaangalia anachokisimamia na yeye ni mtu wa aina gani katika utendaji wake na kujali maslahi ya umma. Ndio maana unakuwa mpuuzi na kukubali kila anachosema kila mtu wa CHADEMA hata kama tunamfahamu kuwa ni mamruki na ndumila-kuwili.
YETOTE ANAYEZISITIZA WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII lazima tumwelewe na tukubaliane na hilo maana suala la kuajibika halina rangi ya bendera.

Suala kutawala hata miaka mia ni juu yako mwananchi CCM hawajawahi kukushikia bunduki uwachague; Work- hard mhamasishe watu wawakate katika sanduku la kura na si kuleta hapa mihemko yako ya kichama wewe Maranya
 
Anamaanisha nini huyu mgonjwa? Yaani hii nchi tuna shida sana misomi yetu ni mipumbavu tu sijui kwa nini? huyu naye anatuambia umaskini wetu unatokana na Ars kupenda siasa? Upumbavu mtupu! wakishabikia ccm hawasemi!! Huyu naye ni walewale.

Ni akili na misemo ile ile ya CCM, Siasa ndo dira ya nchi, angalia mafisadi wote ndo wanasiasa na ndo waloshika (nchi) mpini wa kisu na kupindisha utawala wa sheria, na kama utawala wa sheria hauheshimiki/haupo maendeleo hayawezi kuja. PRO-fesa tupe mikakati siyo bra bra za ccm, naona nawewe umeanza kuoza kama hao ccm wenza, maana huo usemi wako unatia ualakini
 
hii kauli ya huyu mmjomba imekaa kichama na siyo kiserikali. kweli kuna haja ya kuwatazama upya hawa watu wanaoitwa mawzairi hasa upatikanaji wao!!! tufike mahali waziri awe anafanya apllication kabisa kama anataka kuongoza wizara fulani coz utendaji wao unatia mashaka!!! jamaaa ameongea pumba sana.
 
Siasa ni muhimu kwa maendeleo ya jamii.
Jamii isiyojihusisha siasa itakuwa maskini na dhaifu daima!
Mawazo ya waziri yanaweza tu kutolewa na mkoloni au mnyonyaji ambaye anawadanganya watawaliwa wenye mawazo duni ili kudumisha ukoloni wao.
Anachotakiwa waziri awaambie wananchi ni jinsi gani washiriki katika siasa kudhibiti wizi wa rasilimali za nchi, kuongeza pato la taifa na kuhakikisha tunawatumia wageni kwa faida yetu badala ya wao kutumia utajiri wetu kujiendeleza.
Ni muhimu kila mtanzania awe na mtazamo wa kupambana na ukoloni mamboleo ambao sasa hivi viongozi wengi wamegeuka kuwa mawakala.
Kiongozi mzuri anayefaa kwa watanzania ni yule anayepinga kwa nguvu zote ukoloni mamboleo ambao unaongeza na utaendeleza umasikini wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Hata hivyo, wakati huu tunahitaji siasa za vitendo zaidi kuliko siasa maneno!
MAENDELEO YA MTU MMOJA MMOJA NA TAIFA KWA UJUMLA YATAPATIKANA KWA VITENDO NA SIYO KWA MANENO!
 
Back
Top Bottom