Waziri Nchemba: Hata mimi ni binadamu tu, ninakosea

Waziri Nchemba: Hata mimi ni binadamu tu, ninakosea

Wachache wananeemeka, tozo zinamla maskini
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Kwanini alirudiarudia kujitutumua kwenye runinga kutuambia tuhamie Burundi, binadabu hukosea akajirekebisha, yeye hakujirekebisha sasa Tanzania inakwenda kumfundisha kwa vitendo vinginevyo ahamie kusikojulikana
 
wewe hukosei bali unafanya kwa maksudi.kama ni issue ya tozo wengi walilalamika sana lkn ukaweka pamba masikioni ni kuisifia sana bajeti yako kuwa ni ya wananchi.Leo yako wapi?shida mkipewa madaraka viongozi wengi wa tanzania na afrika kwa ujumla mnajisahau mlikotoka.
[emoji38][emoji38]
 
Tozo hutozwa kwa kutumia huduma fulani na yule mtoa huduma hiyo, hizi tozo za Mwigulu ni za nini?

Tunalipa Kodi zote stahiki hizi tozo za Mwigulu ni zuluma tu.

Mwigulu na ccm woooote ni wezi wakubwa sana ! Laana ya Mungu iko siku itawapiga!
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Zamani iliendaje, Wezi kwenye ubora wao. Ni dhambi kubwa sana kuiba na unayemwibia anajuwa kuwa unaiba lakini anakuangalia tu. Daaah siku atakapoamua anayeibiwa, wezi chapu watabanana Airport kwenda kuleeeeeeee walako baita wanapoenda kuomba misaada.
 
[emoji1][emoji1]
 
Waziri mwenye dhamana kubwa kama yeye hawezi kuongea maneno mepyesi kama hayo.
 
Pale alipoondolewa na kurudishwa na Magufuli alitakiwa kuanzia pale abadulike kwanza akumbuke alikotoka kabla hajawa Mbunge na Uwaziri.
Lakini kwa kuwa hakuyataka haya hakuwa na haja ya kuomba msamaha hata ongea yake aiashirii msamaha kwani uliotoka kwa mwamba msamaha inajulikana hii ni kutoka moyoni.
Iliyobaki ni yy tu aombe rehema kwa Mungu ili Mama abakishe ktk hiyo nafasi aliyopo vinginevyo akaendeleze biashara zake na kutumikia wananchi wa jimbo lake kwani hiyo ndo kazi aliyoimba na akapewa kwani uwaziri ni matokeo na bahati ya mtu.
 
Back
Top Bottom