Waziri Nchemba: Hata mimi ni binadamu tu, ninakosea

Waziri Nchemba: Hata mimi ni binadamu tu, ninakosea

Kijogoodi

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,361
Reaction score
2,373
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba wakati akibanwa maswali na wananchi huko Sirari amesema yeye pamoja na viongozi wenzake serikalini ni binadamu tu kama wengine hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani hivyo ameomba kusamehewa kwenye hili swala la tozo na ameunda timu ya kupitia upya namna tozo zinavyokusanywa na kuumiza wananchi.
🤣
 
CCM ni wazoefu wa kutengeneza tatizo halafu wanajifanya wameliona na watalitatua tatizo husika...hili dubwasha tusipolikalisha pembeni Watanzania tutaendelea kulizwa sana. 🙁
 
Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba wakati akibanwa maswali na wananchi huko Sirari amesema yeye pamoja na viongozi wenzake serikalini ni binadamu tu kama wengine hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani hivyo ameomba kusamehewa kwenye hili swala la tozo na ameunda timu ya kupitia upya namna tozo zinavyokusanywa na kuumiza wananchi.

View attachment 2355228
Nimerudia clip hiyo zaidi ya mara tatu, Amesema wao ni binadamu, hivyo hufanya makosa.

Kauli hii ni ya kiungwana na ya kujishusha, hongera kwake.

Bt hakuna mahala amesema anaomba MSAMAHA. Hajaomba msamaha Bado, hivyo aombe radhi hadharani.

Akumbuke pia hata akiomba radhi, tunaweza msamehe, lakini hatutoruhusu aendelee kukalia kiti hicho sababu ameichafua sana TAASISI ya URAIS Kwa kauli zake za KILEVI.
 
Mh Waziri na kushauri uwe wakili mwema wa Kristo Bwana katika kutumikia Watanzania. Hiyo nafasi uliyopata Neema ya Mungu kuipewa ni nyeti sana. Ombea akili, fahamu na ulimi wako kila itwayo leo.Kukiri mapungufu na kuomba toba kwa Mungu ni kitendo cha kishujaa na ujasiri. Sirikali yenu iangalieni bando kasi yauishaji wake inatia mashaka mengi kwa sisi watumiaji. Mungu wa Mbinguni ashukuriwe kwa kuingilia kati kuhusu bei ya mafuta huko duniani.
 
Waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba wakati akibanwa maswali na wananchi huko Sirari amesema yeye pamoja na viongozi wenzake serikalini ni binadamu tu kama wengine hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani hivyo ameomba kusamehewa kwenye hili swala la tozo na ameunda timu ya kupitia upya namna tozo zinavyokusanywa na kuumiza wananchi.

View attachment 2355228
Akikosea na kukubali kakosea, aende Burunfi.
 
Back
Top Bottom