Waziri Nchemba: Hata mimi ni binadamu tu, ninakosea

Rais Samia kumuacha mwigulu ofisini ni kuwadhalau watanzania, ili kutibu mioyo ya watanzania na kurudisha imani ya watanzania kwake mwigulu amtafutie shughuli nyingine ya kufanya sio wizara ya fedha. Maana wizara ya fedha ni wizara inayotakiwa kuna na mtu asiye na mihemko kama mwingilu, alishauriwa mwanzo akapandisha mabega sasa anawaomba radhi watanzania kama hakuna mtu asiyekosea. Alifanya kwa kujua watanzania hawana uwezo wa kumfanya kitu chochote.
 
Behind the seen:
6C3909B1-5FBC-45E5-8ADB-A607B4FD2183.jpeg
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Sasa sisi tunaokaribia nchi ya ahadi laiyotutaka twende , tusubirie neno lingine toka kwake au tuendelee na safari!! 😭
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Makusanyo ya Kodi na tozo za kinyanganyi wapi wapi !? 😤😢😢
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

Ajiuzulu basi kama ni kweli
 
Nimerudia clip hiyo zaidi ya mara tatu, Amesema wao ni binadamu, hivyo hufanya makosa.

Kauli hii ni ya kiungwana na ya kujishusha, hongera kwake.

Bt hakuna mahala amesema anaomba MSAMAHA. Hajaomba msamaha Bado, hivyo aombe radhi hadharani.

Akumbuke pia hata akiomba radhi, tunaweza msamehe, lakini hatutoruhusu aendelee kukalia kiti hicho sababu ameichafua sana TAASISI ya URAIS Kwa kauli zake za KILEVI.
Yeye hajaifaua Taasisi ya Urais, Taasisi ya urais imejichafua yenyewe kwa kumuacha aendelee kuwa kwenye hicho kiti ilhali dhamana ya kumtoa muda wowote inayo.

Kwahiyo kama ni kutafuta wa kulaumiwa kwenye hii damage basi ni mama yenu SHH, au laasivyo tukubaliane kwamba SSH hana uwezo wa king'amua mambo kisomi ndiomaana Mwigulu alifanya alivyofanya.
 
Kwenye Urais safari hii tumepigwa,WATEULE wanamwongoza MTEUZI!!
Watanzania tumwombe sana Mungu atuepushe na kikombe hiki!
Haya hutokea pale ambapo tu, WATEULO wamemzidi ujanja na akili MTEULE kitu ambacho ni lazima tukubaliane navyo tu.
 
Tozo hutozwa kwa kutumia huduma fulani na yule mtoa huduma hiyo, hizi tozo za Mwigulu ni za nini?

Tunalipa Kodi zote stahiki hizi tozo za Mwigulu ni zuluma tu.
Ni dhuluma kwakua anaichukua bila mhusika kuridhia, na kwamba anaichukua bila ya kutoa huduma yoyote inayostahili kulipiwa kupitia hizo tozo, yani anakata tu kwakua kaamua kukata.

HUO NI WIZI waziwazi.
 
Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba amesema yeye pamoja na viongozi wenzake Serikalini ni binadamu kama wengine, hivyo lazima watafanya makosa kwenye maamuzi fulani kuhusu #Tozo.

Amesema “Katika kugusanagusana kuna maeneo tunakosea, sisi ni binadamu kwani tutashindwa kukosea? Hata ninyi kwenye familia zenu kuna siku mnakosea.”

Ameongeza “Katika kutekeleza kuna maeneo tutakosea, hata juzi Chama kimetupa maelekezo ya kuangalia utaratibu wa utozaji, lakini isiondoe mantiki ya ukusanyaji, nchi haiwezi kwenda bila makusanyo.”

wewe hukosei bali unafanya kwa maksudi.kama ni issue ya tozo wengi walilalamika sana lkn ukaweka pamba masikioni ni kuisifia sana bajeti yako kuwa ni ya wananchi.Leo yako wapi?shida mkipewa madaraka viongozi wengi wa tanzania na afrika kwa ujumla mnajisahau mlikotoka.
 
Back
Top Bottom